Wizi maeneo ya Goba, polisi tusaidieni

mkuzi

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
1,627
1,457
Kumekuwa na ongezeko la wimbi la uwizi maeneo ya Goba kuanzia njia panda ya kinzudi kuja kwa maeneo ya Mwaikambo mpaka Kunguru huku Mbezi Goba.Wanaiba sana vifaa vya magari na wanawapa sumu mbwa na wizi wa kupora pikipiki yaani watu Amani imepungua na taarifa isiyo rasmi kuwa kituo cha polisi Goba hufungwa saa 12 jioni.

Tunaomba msaa da wa polisi kwa doria naamini mwenyekiti wa serikali za mtaa taarifa anazo ila sijajua plan yake ikoje,na wakazi wa maeneo haya tujipange tufanye maeneo haya kuwa salama ,Polisi ingilieni kati suala hili msaada wenu ni muhimu najua polisi mnasoma kwani wengi ni members humu
 
Kumekuwa na ongezeko la wimbi la uwizi maeneo ya Goba kuanzia njia panda ya kinzudi kuja kwa maeneo ya Mwaikambo mpaka Kunguru huku Mbezi Goba.Wanaiba sana vifaa vya magari na wanawapa sumu mbwa na wizi wa kupora pikipiki yaani watu Amani imepungua na taarifa isiyo rasmi kuwa kituo cha polisi Goba hufungwa saa 12 jioni.Tunaomba msaa da wa polisi kwa doria naamini mwenyekiti wa serikali za mtaa taarifa anazo ila sijajua plan yake ikoje,na wakazi wa maeneo haya tujipange tufanye maeneo haya kuwa salama ,Polisi ingilieni kati suala hili msaada wenu ni muhimu najua polisi mnasoma kwani wengi ni members humu
Polisi post zote zinafungwa saa kumi na mbili mkuu.
Hii nadhani ilikuja baada ya kipindi kile vituo vingi vilikua vinavamiwa kama vile stakishari.
Ila walitakiwa watafute njia mbadala ya kupambana na hawa waalifu wa kuvamia vituo badala ya kuwakimbia nankufunga kabisa.maana jamaa watakua wanatamba mitaani.
 
Kamwambie Raisi wa mioyo yenu fisadi Lowasa awaletee Polisi awasaidie!
 
Sidhani kama wazee wa intelijensia watakuja...jaribuni kuwaambia kuna mikusanyiko ya chadema/UKAWA huko for quick response.
 
Mkuu hutakiwi kuwaomba msaada polisi wawalinde ninyi na mali zenu hapo Goba kwani ni wajibu wao kisheria na wanalipwa mishahara kila mwisho wa mwezi kwa ajili hiyo. Kwa wewe kuwapa taarifa inatosha. Isipokuwa kama utaona wanapotezea taarifa yako wasiliana na mamlaka za juu yao kwa hatua zaidi(eg Waziri wa mambo ya ndani).
 
Kama kuna amewahi kutapeliwa maeneo ya goba kesho unaweza kwenda polisi kawe kumtambua mhusika amekamatwa huwa anajitambulisha jina la SAIDI Anatembela pikipiki
 
Pole mleta mada. Koment za watu wengine humu zinatia kichefuchefu. Hamna msaada wowote utakaopata kutoka kwa mtanzania ama Polis. Wewe jilinde na muombe Mungu.

Kwa taifa lolote liweze kuendela na kupiga hatua ya dhat kwanza ni usalama wa raia na utawala wa sheria kwa bahat mbaya hiv haviko kwetu
 
Polisi post zote zinafungwa saa kumi na mbili mkuu.
Hii nadhani ilikuja baada ya kipindi kile vituo vingi vilikua vinavamiwa kama vile stakishari.
Ila walitakiwa watafute njia mbadala ya kupambana na hawa waalifu wa kuvamia vituo badala ya kuwakimbia nankufunga kabisa.maana jamaa watakua wanatamba mitaani.

Kumbe police post wanafunga vituo mapema kuliko zahanati? nilikuwa sijui jamani. Tumeachwa tujitegemee kiulinzi
 
Ndio maana mie nilijenga huko nikakimbia kukaa baada ya kuona ile bar ya six pale kisauke Goba Kulangwa kila siku inavamiwa
 
Na usiku wa jana tena wameiba kwa jirani vifaa vya gari duu
 
Hata mchana police post ya goba haipo active..
Nyuma tu ya kituo kuna kijiwe kikubwa cha bangi...lakin ilibid zije defender kutoka kawe kuwakamata hao wauza bangi
 
kama kawa wimbi la wizi limeibuka tena Goba ,kuna wezi maarufu walikuwa jela wametoka Shaban na Noel ,ole wao sasa haitakuwa jela itakuwa kuzimu
 
Back
Top Bottom