Wizi kwenye vifurushi vya Tigo kwa sasa ni kero kubwa

stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
870
1,249
Wakuuu siku hizi kuna wizi mkubwa sana kwenye vifurushi katika mtandao wa Tigo, unaweka kifurushi cha 2GB dakika tu wanakuletea text kuwa MB zako zimebaki 50.

Kuweni makini sana na hili suala wamechachamaa sana kuiba MB zetu.
 
Kweli aisee, hata mimi ishu hiyo kwa tigo nimewavulia kofia, ni wezi wajanja sana hawa....

Inabidi TCRA walifanyie kazi hili. Watathmini kama kweli vifurushi vyao vya bando vinaendana na thamani halisi ya pesa wanayotoza
 
Tigo ni wezi sana. Nakumbuka nilikuwa najiunga kifurushi cha GB1 kwa 2000 wiki

Hiyo GB1 wanaigawanya kupitia Facebook na Whatsapp. Hapo unakuta MB za kuperuzi zako wewe kama wewe ni 200MB.

So unaweza ukamaliza MB siku hiyo hiyo, na utatakiwa uweke tena zingne.
 
Hivi TCRA wamelala? Ukinunua Tigo 1 GB unaambiwa 500 MB Facebook, 300 MB Whatsapp, 200 MB ndio internet ambayo utatumia tu kufungua emails na kuisha hapo hapo.

Hivi kwa nini wanapora MB utafikiri kila mtu yupo interested na kutumia Whatsapp na Facebook? Yaani regulatory authority kauchapa usingizi makampuni ya simu yanaibia wananchi yanavyotaka, only in Tanzania.
 
Back
Top Bottom