Wizi Kupitia NMB Mobile, Beware!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Kuna jamaa yangu aliniambia kwamba kuna baadhi ya watu waliibiwa fedha kupitia NMB Mobile Tawi la Tukuyu!

Wizi wenyewe ulifanyika kama ifuatavyo:

Kuna watu ambao hawajui kutumia ATM na mara nyingi huomba msaada kwa mtu aliye karibu. Kuna vijana ambao huwa wanakaa standby kutoa misaada ya aina hiyo. Mwomba msaada huwa anatoa namba yake ya siri (PIN) kwa mtoa msaada. Wakati wa kutoa msaada, Mtoa msaada anamuuliza mwomba msaada kama amesajili akaunti yake kwa ajili ya NMB Mobile! Kama sio, mtoa msaada anachukua taarifa za mwomba msaada (No ya Akaunti na PIN) kisha ananunua line ya simu halafu anasajili namba hiyo kwa NMB Mobile.

Anafanya hivyo kwa watu wengi. Kisha anahamisha salio toka kwenye akaunti husika ya NMB kwenda kwenye akaunti yake ya NMB! Gud news ni kwamba wezi wa namna hiyo walishakamatwa na Polisi kwa kuwa taarifa zao za kibenki zinapatikana kupitia akaunti zao! Ushauri ni kwamba usimpatie mtu YEYOTE PIN yako ili kuepusha usumbufu usio wa lazima! Kesi inaweza kwenda mahakamani na washtakiwa wakaambulia vifungo bila faini ya kukurudishia wewe fedha, si unajua mahakimu wengine vichwa vyao vimekaa tenge? Au mshtakiwa akifungwa miaka 7 jela halafu akitoka ndio aje akulipe fedha yako, kwa kipato gani toka gerezani? In short, a simple mistake through trust can cost you alot! Hav a great day!

Mods naomba, kama inawezekana, thread hii isichanganywe na nyingine ili isipoteze maana yake!
 
Kuna jamaa yangu aliniambia kwamba kuna baadhi ya watu waliibiwa fedha kupitia NMB Mobile Tawi la Tukuyu! Wizi wenyewe ulifanyika kama ifuatavyo: kuna watu ambao hawajui kutumia ATM na mara nyingi huomba msaada kwa mtu aliye karibu. Kuna vijana ambao huwa wanakaa standby kutoa misaada ya aina hiyo. Mwomba msaada huwa anatoa namba yake ya siri (PIN) kwa mtoa msaada. Wakati wa kutoa msaada, Mtoa msaada anamuuliza mwomba msaada kama amesajili akaunti yake kwa ajili ya NMB Mobile! Kama sio, mtoa msaada anachukua taarifa za mwomba msaada (No ya Akaunti na PIN) kisha ananunua line ya simu halafu anasajili namba hiyo kwa NMB Mobile. Anafanya hivyo kwa watu wengi. Kisha anahamisha salio toka kwenye akaunti husika ya NMB kwenda kwenye akaunti yake ya NMB! Gud news ni kwamba wezi wa namna hiyo walishakamatwa na Polisi kwa kuwa taarifa zao za kibenki zinapatikana kupitia akaunti zao! Ushauri ni kwamba usimpatie mtu YEYOTE PIN yako ili kuepusha usumbufu usio wa lazima! Kesi inaweza kwenda mahakamani na washtakiwa wakaambulia vifungo bila faini ya kukurudishia wewe fedha, si unajua mahakimu wengine vichwa vyao vimekaa tenge? Au mshtakiwa akifungwa miaka 7 jela halafu akitoka ndio aje akulipe fedha yako, kwa kipato gani toka gerezani? In short, a simple mistake through trust can cost you alot! Hav a great day! Mods naomba, kama inawezekana, thread hii isichanganywe na nyingine ili isipoteze maana yake!
Thank you for alerting us
 
mambo mengine bana..kama kutumia ATM uwezi si uende ndani ukakae kwenye foleni?kwani lazima uonekane unaingia kwenye ATM?
 
hii taarifa nzuri naipenda jf kwani utapata mambo yote ya kitaifa na kimataifa
 
Yawezekana aliyeibiwa anatokea kijijini,Maana wa Mjini tayari walishasoma hako kamchezo very long!!!!
 
Back
Top Bottom