Wizi huu hapana jamani

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Mwaka jana nilitaka kujiunga na masomo ya degree ya kwanza kupitia Central Admission System, kwa kuwa mimi nina stashahada nikapitia Nacte website. Moja ya mashariti ya kuomba kupitia mtandaoni ni kuwa na namba ya siri inayoonesha umelipia ada ya 50,000 kupitia M PESA. Last year nililipa 50,000 lakin mpaka muda wa maombi unaisha mtandao wao uligoma kufunguka kabisa wakawa wameiba hiyo 50,000 yangu, najua siko pekee yangu wengi tuliibiwa kwa mtindohuo.

Mwaka huu nilikusudia kuanza mchakato huu mapema, nimelipa 50,000 nyingine na kupewa hiyo M PESA code number cha ajabu mpaka sasa mtandao wa CAS haufunguki katika upande wa wenye diploma. Sasa nauliza wahusika, najua wengine mnapita huma jamvini, kwa nini mmeamua kutuibia? cha ajabu hata namba za simu mlizotoa kwenye admission guide book ya 2014/2015 mkipigiwa hampatikani 24hours, hivi kwa nini mnakuwa na tabia za wizi wa kihuni kama huo? nimetumia lugha ya hovyo kwa sababu nishakwazika na kwa ubabaishaji huu Tanzania tusahau kabisa maendeleo.
 
pole mkuu ila punguza jazba kwani umewatumia sms nacte, tcu au humu jamvini? usiwake sana
 
Pole mkuu hata mm nimeshaibiwa 50000 ya kwanza nasubiri waniibie safari hii nitakwenda mpaka walipo tuelewane
 
poleni sana wadau, hata mimi nataka ni apply mwaka huu, so najiandaa kuibiwa, duh, wacha tuone.
 
tupe ufaulu wako f4 na f6,na masomo yako.

Kipaumbele ni science, si kulialia ilhali hujasoma guidebook..
Na unashauriwa usiombe kama huna vigezo.
Kama unataka endelea waofa hela za supu na beer go on apply.
 
poleni sana wadau, hata mimi nataka ni apply mwaka huu, so najiandaa kuibiwa, duh, wacha tuone.

Kanunue vocha NBC haisumbui.jana nimeshuhudia jamaa aliye lipa kwa M shiling akishindwa kabisa kutuma maombi kwa masaaa takribani 5 Anajibiwa refference number ni batili lakini wamemtumia wenyewe baada ya kulipa kwa mpesa
 
ukiwasiliana nao kwa namba za simu walizotoa kwenye guide book yao mara nyingi hawapatikani, ukituma e mail hawajibu au wanajibu majibu yasiyotosheleza. Kama wewe ni mhusika kawaambie wakubwa wako au wenzio, hatutaki mifumo ya wizi kama hii. kama mnataka digitali boresheni quality yake
 
Kanunue vocha NBC haisumbui.jana nimeshuhudia jamaa aliye lipa kwa M shiling akishindwa kabisa kutuma maombi kwa masaaa takribani 5 Anajibiwa refference number ni batili lakini wamemtumia wenyewe baada ya kulipa kwa mpesa

Mkuu wanaotumia vocha ni form six tu, diploma wao lazima walipe kwa m-pesa, Hata hivyo ni kawaida kwa mtandao kusumbua ivo kama upo Dar nenda nacte watakusaidia vizur kabisa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom