Wizi hotel ya millenium sea breaze hotel bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi hotel ya millenium sea breaze hotel bagamoyo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpambanaji K, Dec 4, 2010.

 1. M

  Mpambanaji K Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi nilikuwa hoteli ya kitalii ya millenium sea breaze hotel bagamoyo nikitafuta booking kwa ajili ya mkutano. Nilikutana na vikundi vikundi vya watu waliokuwa wamehuzinika kwa mgeni mmmoja kuvunjiwa chumba chake na kuibiwa kila kitu-fedha,laptop na mengineyo.

  Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja amabye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za usalama wake, wizi katika vyumba vya millenium hoteli sasa ni kitu cha kawaida kabisa. Anasema wiki iliyopita tu kuna mzungu mmmoja aliiibiwa kila kitu na sasa kuna kesi zaidi ya tano za wizi wa vyumbani usiku. kwa mujibu wa mfanyakazi mwingine, cha kusikitisha ni kuwa uongozi wa hoteli unaonekana kutojali kwa kuwa kuna kigogo wa serikali anayewalinda

  Kwa mjibu wa mfanyakazi huyo, taarifa za matukio hayo yote yapo polisi. TAKE CARE.
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Kaaz kwelikweli hapo kwenye red! Utafika muda watajali tu, habari zikienea na wateja kufahamu usalama mdogo ulio hapo hawatafikia tena! Wewe ukiona mwenzio kaibiwa jaribu kuongea na meneja au mkurugenzi kama anapatkana, ukiona hawatoi ushirikiano wa kutosha iogope hiyo "gesti" kama ukoma! Wamiliki wengi wa mahotel wanashindwa kutambua umuhimu wa usalama wa mali yoyote ya mteja (hata iwe shati tu!), mteja hawezi kusubmit kila kitu kwenye safebox ya mapokezi! Hoteli ya kweli hata ukisahau siraha, novel, saa, sh 100 House keeper ataziwasilisha na kuwekwa kwenye "lost and found book" na mteja atapigiwa simu kufahamishwa! Wakati mwingine kukubali hasara kunaepusha hasara, mtu kapoteza say 2 laptops=5,000,000-ukimwomba radhi, ukaongea naye na kumuomba mgawane hasara (2,500,000) utakuwa umetunza uaminifu!
  MTEJA NI MFALME!
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Jamani mbona mwenye hoteli ni mtu wa kuheshimika sana!
  Kaajiri makanjanja au wanataka kumharibia jina
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Jamani mbona mwenye hoteli ni mtu wa kuheshimika sana!
  Kaajiri makanjanja au wanataka kumharibia jina
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  bad news... labda tunasubiri mameneja toka kenya na walinzi toka south sudan
   
 6. M

  Mpambanaji K Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  bad news indeed, habari ni kwamba wafanya kazi wa ndani pamoja na walinzi wa getini wanashirikiana. wizi wote amabo umetokea zaidi ya mara 7 sasa unaffanyika kwenye executive rooms, bila shaka ndio kwa wanaohisiwa kuwa na fedha na vitu vingine vya thamani. habari zinasema kuwa juzi ameibiwa muhadhiri wa chuo kikuu cha dsm aliyekuwa anaratibu mkutano mmoja hapo hotelini.

  Habari za kipolisi na hapo ndani hotelini zinasema kuwa polisi kila kunapotokea hujaribu kuchukua hatua stahili za kisheria, lakini mara kwa mara hukwama kwa sababu wafanya kazi wengi wana undungu na JK.
   
Loading...