Wizi fedha za safari za JK kuchunguzwa

Nilijiuliza maswali kama hayo jana mengi tuu
Anakanusha kwa nguzu zote tena kw akurudia rudia kuwa fedha hazijaibiwa
Kuna uhamishaji ulifanyika
Je kama hakuna wizi unaunda tume ambayo itakula pesa kuchunguza nini kama una uhakika hakuna wizi uliotokea
maana kama ni kuhamishwa tuu kw afedha ni suala la yeye na watu wa wizara yake kuangalia ni kitu gani kimetokea wakirekebishe na kusema wazi kuwa fedha ipo haijaibiwa
Sijui anamdanganya nani au kukurupuka kukanusha kitu ambacho huna uhakika nacho


Sidhani kama angelazimika kutoa taarifa kwenye media kama media isingekuwa imeandika tena taarifa ya uongo.tunapenda sana kusikia wizi umefanyika. Kamati ikiundwa na Bunge baada ya pesa kuwa imeshaibiwa halafu kamati hiyo ikatumia mil 500 kuchunguza pesa ambayo imeshaibiwa tunafurahia. Serikali ikiunda timu kupitia mifumo yake kwa lengo la kubaini mapungufu na kuboresha mifumo yake ili kuzuia mianya ya wizi tunalalamika. Hii ndio tanzania.
 


images
Monday, 18 June 2012 21:04

Nora Damian

SERIKALI imeanza uchunguzi wenye lengo la kubaini kama maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walifuata taratibu kutoa Hazina Sh3.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete ndani na nje ya nchi.

Alifafanua kwamba tayari walifanya uchunguzi uliohusisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na wakaguzi wawili kutoka wizarani hapo."Hakuna tuliyemshuku ama kumuita mwizi kwa sababu hakuna hata fedha iliyoibwa, zote ziliingia kwenye akaunti ya wizara na nyingine zililetwa wizarani," alisema.

Waziri huyo alisema uchunguzi wa kamati unaoendelea, sasa unalenga kuangalia kama taratibu zilifuatwa na wale waliokuwa wanakaimu."Uchunguzi wa kamati utakapokamilika na kubainika makosa yalikuwa wapi utawekwa hadharani," aliahidi.

Sasa uchunguzi wa nini kama hakuna pesa iliyoibwa?
 
membe kama kweli fedha hazijaibiwa kwa mujibu wa taarifa yako tume ya nini hii inaonyesha kabisa kuwa fedha unajua zilipo kwa nini usiwaambie wananchi wazalendo wa taifa hili kuwa fedha zipo mahali flani na kama unasita pengine kulinda usalama wako kwa nini usipitie kwa watu wengine ili isijejulikana ya kuwa aliyelitoa suala hili siyo wewe na kama unaunda tume kushughulikia suala hilo hao watu watakao teuliwa ni vigezo gani vitakavyotumika isije ikawa ni danganya toto
 
Yaani kama kila safari inagharimu bilioni mbili au zinazokaribia ni kwanini cdm wasilalamike? Coz kama anatumia bilioni 2 kutafuta bilioni moja na nusu tena za kuahidiwa kwa masharti hiyo si ni biashara kichaa? Mambo mengine si mpaka cdm waseme; huu ni uhujumu uchumi kabsaaa!
 
mimi nimeshangazwa na kiasi kinachotumika kwa ziara tatu tu,tena moja ni ya ndani ya nchi!wastani wa sh.1.666 bilioni kwa kila safari.
 
membe kama kweli fedha hazijaibiwa kwa mujibu wa taarifa yako tume ya nini hii inaonyesha kabisa kuwa fedha unajua zilipo kwa nini usiwaambie wananchi wazalendo wa taifa hili kuwa fedha zipo mahali flani na kama unasita pengine kulinda usalama wako kwa nini usipitie kwa watu wengine ili isijejulikana ya kuwa aliyelitoa suala hili siyo wewe na kama unaunda tume kushughulikia suala hilo hao watu watakao teuliwa ni vigezo gani vitakavyotumika isije ikawa ni danganya toto

Vigezo gani wewe wataka vitumike kwenye kuchagua tume? tume inahusisha taasisi nyeti kama usalama wa taifa na takukuru....unataka vigezo gani wewe
 
Jamani Waziri Membe anasema kinachochunguzwa ni utaratibu uliotumika kuzitoa fedha zile Hazina kuzileta Kwenye account ya Foreign Affairs na baadaye kiasi cha fedha kikatolewa kwenye account na kuzileta fedha hizo Wizarani bila viongozi wa Wizara kujua. Kwa hiyo tume iliyoundwa ili inangalia kwa nini pesa ilitoka hazina bila consent ya Viongozi wakuu wa Wizara. Sambamba na hilo anataka kujiridhisha kama utaratibu haukukosewa na kama Kilichotokea hakijawahi kutokea kabla huko nyuma.


Namushangaa Sheba na Kalebe kwa kushindwa kuelewa tafsri ya kawaida ambayo Waandishi wote wa habari wameelewa mpaka wakaamua kuandika kwenye magazeti hayo. mpaka sasa hakuna aliyeleta hata ushahidi wa tape kumuonyesha Waziri huyu akiisifu Chadema kushinda uchaguzi wa 2015. Nashauri mpate wasaa wa kupitia magazeti na taarifa za kwenye television kuhusu kauli ya Membe
 
Nawaambia ukweli hizo hela zimeibiwa na wajanja hamuoni hata rais Kikwete siku za karibuni amepunguza kusafiri safiri kwenda nje.Pesa zimeibwa ndo maana tume imeundwa ila Membe kaamua kuwadanganya watanzania.
 
Tutofautishe vitu hivi - kuna kuiba tena kwa makusudi, kuna kukiuka taratibu pasipokudhamiria, kuna kughafirika, kuna kusingiziwa, kuna kutoaminiana, kuna kufitiana.n.k.Sasa mimi hapo sijui kipi kilitokea.
 
Pia jamani na hawa waandishi wanoitwa kny press conference wawe wanakuwa critical kuuliza maswali haiwezekani eti waziri anakana hakuna wizi wakati huo huo anaunda tume kuchunguza wizi halafu hamna mwandishi hata mmoja wa kumbana waziri kumuuliza maswali ya kwa nini anaunda tume ifanye kazi gani kama anaona hakuna wizi?
 
Kama safari 4 tuu katumia 3.5bill ni sawa na 875millions kwa safari moja!
N bado mnasema Tz ni nchi maskini basi mna matatizo ya kuset vipaumbele!
 
Nchi hii kila mtu amekuwa mwizi? Ukiona mpaka hela ya safari ya boss inaliwa, ujue hela zinaliwa kweli kweli. Halafu hao jamaa ndio wako fore front ya representation ya nchi yetu. Kazi ipo
 
Back
Top Bottom