Wizi fedha za safari za JK kuchunguzwa

Bebrn

Senior Member
Mar 20, 2008
103
23
hvivi kweli tumefikia kiasi hiki cha kuwaona watanzania wote ni wajinga kiasi hiki, membe leo wakati anaongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa fedha za safari ya raisi zilikuwa hazijaibiwa ila wameunda tume ya kuchunguza, sasa hapo anamaanisha nini? kwa walioelewa tu wanaweza kunipa jibu
 
hvivi kweli tumefikia kiasi hiki cha kuwaona watanzania wote ni wajinga kiasi hiki, membe leo wakati anaongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa fedha za safari ya raisi zilikuwa hazijaibiwa ila wameunda tume ya kuchunguza, sasa hapo anamaanisha nini? kwa walioelewa tu wanaweza kunipa jibu

shavu kwa tume
 
Hata mie HUYU MEMBE kanishagaza anakusha pesa kupolwa huku anasema kaunda ume kuchunguza,hawa majamaa walishatuona mabwege tena wakutupwa.
 
Mwenyekiti wa mtaa wangu ntamshauri aunde tume kuwachunguza vibaka wa mtaa wetu,maana kuna kuku amepote.
 
Hivi waandishi wa habari wanakuwaga wapi kuuliza maswali kamka haya? Au waandishi wetu sikuiz ndo style ya kuja kukopi JF na kupaste kwenye Gazeti?
 
hivi kweli mtu unaweza kwenda kuchukua rb kama hakuna tukio? haya na sasa tundaunda tume hata za kuchunguza kama serikali ipo au haipo!!!
 
hvivi kweli tumefikia kiasi hiki cha kuwaona watanzania wote ni wajinga kiasi hiki, membe leo wakati anaongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa fedha za safari ya raisi zilikuwa hazijaibiwa ila wameunda tume ya kuchunguza, sasa hapo anamaanisha nini? kwa walioelewa tu wanaweza kunipa jibu
kumbe tuko wengi tulioona hii kitu. eti pesa ipo salama, ila tume itatuambia nini kilitokea. Hizo ndio akili za viongozi wetu
 
Nilipoona anatoa maelezo nilistaajabu sana, kwani inaonekana dhahiri huyu ni mtu wa kukurupuka .Membe naye ni janga la taifa
 
Nilijiuliza maswali kama hayo jana mengi tuu
Anakanusha kwa nguzu zote tena kw akurudia rudia kuwa fedha hazijaibiwa
Kuna uhamishaji ulifanyika
Je kama hakuna wizi unaunda tume ambayo itakula pesa kuchunguza nini kama una uhakika hakuna wizi uliotokea
maana kama ni kuhamishwa tuu kw afedha ni suala la yeye na watu wa wizara yake kuangalia ni kitu gani kimetokea wakirekebishe na kusema wazi kuwa fedha ipo haijaibiwa
Sijui anamdanganya nani au kukurupuka kukanusha kitu ambacho huna uhakika nacho
 
KAtika wale Mawaziri ambao walipaswa kuondolewa ni pamoja na Membe, kwani naye Wizara yake ina ufisadi na wizi wa pesa za Serikali.

Sijui aliroga kiasi gani hadi CAG hakummulika katika Report yake!!!!! Huyu mtu wa Kusini ni hatari sana kwa mambo ya ........ hata Serikali inarogwa jamani, basi balaa.......


Binafsi jana sikumuelewa Membe kabisa alichokuwa anaongea na Waandishi, na kisha waandishi walikaa kimya au hatujui labda walimuuliza lakini haitakuwekwa wazi hadharani....



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Lazima uchunguzi ufanyike kujua mianya ya uhamishaji wa hizo fedha na kuweza kuwatambua wote walioshiriki kwani nahisi kuna wengine wanahusika na hawajatajwa bado....
La msingi ni kuziba mianya hiyo ya uhamishaji fedha...
Najiuliza hao hazina walitoaje hizo fedha bila katibu mkuu wa wizara kuidhinisha...
 
hvivi kweli tumefikia kiasi hiki cha kuwaona watanzania wote ni wajinga kiasi hiki, membe leo wakati anaongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa fedha za safari ya raisi zilikuwa hazijaibiwa ila wameunda tume ya kuchunguza, sasa hapo anamaanisha nini? kwa walioelewa tu wanaweza kunipa jibu

Tatizo letu kubwa ni hulka kuwa any prob team ikiundwa lazima kuwe na wizi. Pili kuundwa kwa Tume hiyo kwa mujibu wake ni kwa ajili ya kujiridhisha ikiwa taratibu za kiutawala na kifedha zilikuwa zimefuatwa. Hivyo ni mchakato wa ndani na wa siku zote ila kwa sababu tunaishi katika zama za hisia zikatolewa magazetini na ndipo alipolazimika kuzijibu.

Timu imeundwa kuchunguza mazingira ya utoaji wa fedha hizo kubaini mapungufu katika utaratibu ili kufanya marekebisho ya kudhibiti mianya ya aina hiyo huko mbeleni maana inawezekana leo utaratibu umekiukwa kwa nia njema lakini kesho wajannja wakatumia mapungufu hayo kufanya ufisadi.

Katika hili Wizara ya Mambo ya Nje inahitaji pongezi kwa kuwa imeonyesha kuwa mifumo yake inafanya kazi na sio kusubiri hadi ziibiwe ndio uongozi ujue. Hii inamaana Mkaguzi wa Ndani anafanya kazi yake. Na pia hatua ya Waziri na Katibu Mkuu wake kuchukua hatua za haraka za kudhibiti nayo ni ya kupigiwa mfano maana wamechukua hatua kwa wakati. Kama sisi ni mashabiki wa uwajibikaji kama tunavyojipambanua humu ndani ya Jamii forum tunapaswa kupongeza hili na kuwatia shime waendelee hivyo hivyo na Wizara nyingine zifanye hivyo.

Kwa uelewa wangu, hii ndio mantiki ya kuunda timu.
 
Kwa nini anapoteza kodi ya walalahoi kulipa watu ili wachunguze kitu ambacho ana uhakika hakikutokea? Tume ya nini?

Wewe ungependa ziibwe kwanza ndio timu ya uchunguzi ifanyike? Unanikumbusha kesi za ubakaji ambapo inashauriwa mwanamke atulie kwanza abakwe ili awe na ushahidi wa kutosha
 
hivi kweli mtu unaweza kwenda kuchukua rb kama hakuna tukio? haya na sasa tundaunda tume hata za kuchunguza kama serikali ipo au haipo!!!

Acha utani, Rb inachukuliwa unapokuwa na tishio tu nini tukio?
 


images
Monday, 18 June 2012 21:04


Nora Damian

SERIKALI imeanza uchunguzi wenye lengo la kubaini kama maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walifuata taratibu kutoa Hazina Sh3.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na Machi 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais Kikwete kwenda Geneva, Brazil, Adis Ababa na Arusha.

Wiki iliyopita gazeti moja la kila wiki liliripoti kuwa maofisa watano wa wizara hiyo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za rais kutoka benki moja nchini.

Fedha zilizotolewa kutoka Hazina ni Sh 3.5 bilioni wakati zilizokuwa zimepangwa kwa safari hizo ni Sh2 bilioni.Fedha hizo zinadaiwa kutolewa Hazina na maofisa waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali, katika wizara hiyo.

Waziri Membe alisema wakati tukio hilo likitokea, yeye, naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu walikuwa safarini na kwamba nafasi zao zilikuwa zinakaimiwa.“Waliokuwa wanakaimu wali-process (andaa) fedha za safari pamoja na hazina, na fedha zikapatikana tarehe 8,” alisema Membe na kuongeza kuwa;

“Ofisa Masuhuri hakushirikishwa na uchunguzi wa kamati unaendelea ili kujiridhisha kama taratibu zote za kiutawala zilifuatwa,” alisema.

Alifafanua kwamba tayari walifanya uchunguzi uliohusisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na wakaguzi wawili kutoka wizarani hapo.“Hakuna tuliyemshuku ama kumuita mwizi kwa sababu hakuna hata fedha iliyoibwa, zote ziliingia kwenye akaunti ya wizara na nyingine zililetwa wizarani,” alisema.

Waziri huyo alisema uchunguzi wa kamati unaoendelea, sasa unalenga kuangalia kama taratibu zilifuatwa na wale waliokuwa wanakaimu.“Uchunguzi wa kamati utakapokamilika na kubainika makosa yalikuwa wapi utawekwa hadharani,” aliahidi.
Utabiri wake Chadema

Akizungumzia taarifa za kuitabiria Chadema ushindi mwaka 2015, Membe aliwatuhumu watu aliowaita maadui wake kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema wameshiriki kumlisha maneno ya kukitabaria ushindi chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Kuna taarifa za mimi kutabiria ushindi Chadema 2015. Naomba niseme kitu kimoja, kama kuna mtu anajua mimi niliwahi kufanya utabiri ajitokeze. Mimi siyo TB Joshua wa Nigeria, mtoto wa marehemu Shehe Yahaya au (jina la kampuni moja ya kimataifa)...ambao wao kila mara ndiyo hufanya utabiri," alisema Membe huku akionekana kuchukizwa na taarifa hizo.

Membe alifafanua kwamba, ni kweli alikutana na ujumbe wa Chadema nyumbani kwake jimbo la Mtama, mkoani Lindi na kufanya nao mazungumzo, lakini hakuwahi kutabiri kwamba chama hicho kikuu cha upinzani kingeweza kushinda mwaka 2015.

"Nikweli nilifanya mazungumzo na Chadema walipokuja jimboni kwangu Mtama. Tena walikuja bahati nzuri walikuta chakula cha mchana tayari, nikawakaribisha vizuri. Wapinzani si maadui, yaani watu walitaka niwafukuze chakula. Najua kuna watu hawakufurahia kuwaalika Chadema kuja kwangu," alisema Membe na kuongeza;

"Ni kweli niliongea nao. Niliongea nao mambo matatu, kwanza niliwapongeza kwa kujipenyeza hadi vijijini. Niliwaambia, ni vema mmetambua umuhimu wa kufika hadi vijijini maana mwaka 2010 mlilalamika kuibiwa kura wakati vijijini mlikuwa hamjafika. Lakini pia, nikawambia ni vema wametambua umuhimu wa kuanza kufanya siasa kwa kujenga hoja na tatu, nikawambia nyie fikeni vijijini sisi kina Membe hatujaanza kutimua vumbi."

Alifafanua kwamba, anaamini watu wa Chadema waliokuwapo katika mkutano huo ambao ni pamoja na Dk Slaa na Lema hawawezi kuzusha taarifa hizo zilizotolewa na kuongeza, "Nimesoma vizuri Political Science, adui wa kisiasa katika chama siku zote yumo ndani ya chama hicho. Kwa hiyo hata hili naamini limetoka kwa baadhi ya maadui ndani ya CCM na kwa Chadema ni maadui wa Chadema."

Kuhusu APRM

Katika hatua nyingine, Membe alisema taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM), itajadiliwa mwakani nchini Addis Ababa.

Licha ya waziri huyo kukiri kwamba Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000 za ada, alisema hiyo si sababu ya taarifa ya Tanzania kutojadiliwa mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

Rais Kikwete alitarajiwa kuwasilisha ripoti ya Tanzania kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU), utakaofanyika Lilongwe, Malawi Julai 10 mwaka huu, lakini haitafanyika hivyo.
Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa Rais Kikwete amezuiwa kuwasilisha taarifa ya Tanzania kutokana na deni hilo.

“Walitakiwa wajadili taarifa ile halafu walete maswali tujibu ndipo wataandaa taarifa ikajadiliwe,” alisema Membe na kuongeza;

“Watu wa APRM hawajaja, hivyo itajadiliwa katika mkutano wa Addis Ababa mwaka 2013,” alisema.
Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000 deni ambalo ni malimbikizo ya ada ya dola 100,000 kila mwaka, kwa miaka minane mfululilizo tangu mwaka 2005.

“Mara kwa mara tumekuwa tukiwakumbusha Hazina kuhusu deni hili na si kwamba ndilo limezuia,” alisema.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom