Wizi chuo Kikuu cha Dar es Salaam umekithiri

Obi

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
374
79
Kumezuka wimbi la wizi chuo Kikuu cha Dar es Salaam hasa katika maofisi ya wahadhiri. Usiku wa kuamkia leo kuna ofisi moja imevunjwa na mvunjaji kuiba computer yenye thamani isiyopungua 1. 5 million. Sasa najiuliza hao wezi wanatoka wapi? Mamlaka husika (Security Guards) wanafanya nini mpaka mtu avunje ofisi na kuiba? au wenyewe ndio wahusika wakuu? Inashangaza pia chuo kikongwe hakina ulinzi imara na wa uhakika.
Ninashauri Mamlaka ya Chuo hicho kuweka security alarms na kamera ziwasaidie kwa hili
 
Pamoja na Public Procurement Act, vikampuni vingi upande wa service providers ni vya wakubwa?
 
Mkuu

Hii Avanta yako vipi? Imekaa ki-shigongo shigongo!!

Nguli, Geoff, Xspin na Mkuu Masanilo nadhani hawajaiona!
 
Wataiba hata hizo camera na security alarms


Hii kali,

kwanza hao security guards wenyewe njaa kali wataacha kuiba mtu unalinda kitu cha thamani ya mamilioni wakati nyumbani debe la unga umeliacha tupu ukisubiri mshahara wa elfu 40 kwa mwezi.
 
Amani na utulivu vikitawala kwa muda mrefu watu hujisahau na hiyo kumwamini kila mmoja! Hata walizi wetu mida ya usiku huwabidi wasinzie badala ya kukaa macho usiku kucha! Wizi huo ni taarifu tu kwa walinzi wetu popote walipo na hasa wa UDSM kuwa wasibweteke/wakeshe kwani hawajui siku wala saa!!!
 
Back
Top Bottom