Wizi atcl:david mattaka na wenzake waongezewa mashtaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi atcl:david mattaka na wenzake waongezewa mashtaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Mar 17, 2012.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake wawili wanaoshitakiwa kwa kuagiza magari yaliyotumika kinyume na utaratibu, kutumia madaraka vibaya wamesomewa mashitaka mapya sita yakiwemo ya kuliingizia shirika hasara ya Dola za Marekani 143,442.75 (Sh milioni 243).

  Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Osward Tibabyakoma alisoma mashtaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Tibabyakoma alidai kuwa kesi hiyo imekuja mbele ya mahakama kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali na kuomba kuwasomea mashitaka mapya kwanza.

  Akisoma mashitaka hayo alidai kuwa Mattaka, Elisaph Ikomba na William Haji wanadaiwa kati ya Machi na Julai 2007 jijini Dar es Salaam walikula njama na kutumia vibaya nafasi zao za kazi kwa kutangaza zabuni ya kuagiza magari ya aina mbalimbali 26 bila idhini ya Bodi ya Zabuni ya ATCL.

  Ilidaiwa kati ya Julai 2007 na Agosti 2007 kwa kutumia madaraka yao vibaya waliagiza magari hayo kwa kutumia Kampuni ya magari ya DALMOUK yenye makao makuu yake nchini Dubai na walinunua magari hayo kwa niaba ya ATCL kwa Dola za Marekani 809,300 (zaidi ya Sh bilioni moja) kutoka kampuni hiyo kinyume cha sheria ya ununuzi wa mali za umma.

  Washitakiwa hao wanadaiwa pia kati ya Julai 2 na 23 Agosti mwaka 2007, Dar es Salaam kwa kutumia madaraka yao vibaya waliidhinisha malipo ya magari hayo yaliyotumika bila kuwa na mkataba kati ya ATCL na kampuni hiyo iliyouza magari na kusainiwa na pande zote mbili.

  Mwendesha mashtaka huyo alidai katika shitaka la mwisho washitakiwa kati ya Julai 2007 na Desemba 2011, Dar es Salaam wakiwa waajiriwa wa ATCL kwa kushindwa kuwa makini walinunua magari 26 yaliyotumika bila kuwa na bajeti iliyotengwa kwa kununua magari hayo na kusababisha ATCL kupata hasara ya Dola za Marekani 143,442.75.

  ATCL iliingia hasara kulipa gharama za kuyatunza magari hayo baada ya kushindwa kulipa kodi na kulipa deni benki pamoja na riba.

  Hata hivyo, washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo na Hakimu alikubali wadhaminiwe kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini watakaosaini dhamana ya shilingi milioni 38, kuwasilisha mahakamani kiasi hicho cha fedha au hati ya mali yenye thamani hiyo.

  Washitakiwa walitimiza masharti kwa kutoa hati zenye thamani zaidi ya kiasi hicho cha fedha lakini upande wa serikali uliomba kuzithibitisha hati hizo Wizara ya Ardhi ili kujiridhisha. Kesi hiyo imeahirishwa na itapangiwa tarehe nyingine ya kuwasomewa washitakiwa maelezo ya awali.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"][TABLE]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Unahisi hii ni siasa za jk na wenzake kama kesi za epa na unaamini aitaishia kupiga kalenda?kama ndio sema
  n
  kama siyo andika
  s
   
 3. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  wembe ni ule ule aminia CCM mafisadi wote lazima watinge kortini
   
 4. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hii Nchi Kama Haijalaaniwa Sijui!! Matakka ni Mtu alishaonyesha Tabia zake Halisi siku Nyingi ya kuwa yeye hana uwezo mwingine Zaidi ya Kuiba na kufilisi Mashirika ya Umma!! Mkapa akampumzisha!! Akaja mwingine akampa Promotion!! Je Ina maana watu Hawakujua kuwa Nyoka hawezi Kubadilika na kuwa Mjusi!! Sasa Naona wa Kushitakiwa ni Waliompa madaraka na sio yeye Matakka!! Kwani Tabia Yake Inajulikana siku nyingi!! Naona hii ni sinema kama ya Abunuwas!!!
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kama David Mattaka anahema na mahakama kwa uvunjaji wa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004, basi BLANDINA NYONI na mwenzie Deo Mtasiwa nao waanze kupiga jaramba kwa kununua sare toka Mariedo bila kufuata utaratibu.
   
Loading...