Wizara za TAMISEMI na Elimu liangalieni hili, watu wananyanyaswa

Songwe Yetu

Member
Nov 22, 2021
84
99
MHESHIMIWA UMMY MWALIMU: UNAJUA KUWA WITNESS MAKOTI ALIYEPIGWA NA MWALIMU MKUU NA KUVUNJWA JINO SASA AMESIMAMISHWA KAZI KULE MOROGORO?

Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu!

Amani iwe kwako!

Miezi michache iliyopita, Ofisi ya Haki ya Askofu Mwamakula, ilifichua taarifa za kupigwa kwa Witness Clemence Makoti (pichani) ambaye alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mkuyuni katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Witness alipigwa na Mwalimu Mkuu aitwaye Mussa Hasira na kuvunjwa jino. Baada ya taarifa yetu, Mkuu wa Polisi wa Mkoa Morogoro alitoa taarifa za kushikiliwa kwa Mussa Hasira kwa tuhuma za kujeruhi.

Baadaye, Witness Makoti alihamishwa Kituo. Kabla hajaanza kazi katika katuo kipya, Witness Makoti amesimamishwa kazi katika mazingira ya kutatanisha. Barua ya kusimamishwa kazi iliandikwa tarehe 24 Novemba 2021 na kusainiwa na Lusubilo L Mwaisunga ambaye ni Kaimu Katibu Msaidizi wa TSC katika Wilaya ya Morogoro.

Lusubilo L. Mwaisunga ndiye huyo huyo aliyemwandikia Witness Makoti barua ya Hati ya Mashtaka (Charge Sheet) ya tarehe 24 Novemba 2021 akimtuhumu kwa kosa la kupigana hadharani na mtumishi mwenzake aitwaye Witness Makoti (hili linashangaza)!

Aidha, tarehe 24 Novemba 2021, huyo huyo Lusubilo L. Mwaisunga alimwandikia barua Witness Makoti akimpa Notisi yaani Kusudio la kumchukulia hatua za kinidhamu.

Maelezo ya Witness Makoti yanaonyesha kuwa, alipokwenda Polisi kuonana na Mpelelezi wake ili kuhimiza Kesi yake ipelekwe Mahakamani, Mpelelezi wake alimjibu kuwa anataka kuwasiliana kwanza na Uongozi wa Chama Cha Waalimu huko Morogoro. Alipowasiliana na Uongozi huo, ulimshinikiza Witness asiende Mahakamani kwanza ili kupisha vikao vya Usuluhishi. Witness alitoa siku 14 kwa uongozi huo, lakini kabla siku hizo hazijapita, akaandikiwa barua tatu zilizosainiwa na mtu mmoja ikiwemo ya kusimamishwa kazi.

Pamoja na haki za Witness kuanza kuonyesha dalili za kupotea, Witness ana wasiwasi na hofu pia juu ya usalama wa maisha yake! Kuna hisia kuwa baadhi ya viongozi kule Morogoro wanabebana kwa lengo la kumkandamiza Witness.

Ofisi ya Haki ya Askofu Mwamakula inaishauri Ofisi yako Mheshimiwa iitishe faili husika na kuziona kwa lengo la kuzichunguza barua zote alizoandikiwa Witness. Aidha, tunashauri kuwa Ofisi yako ionane na Witness na kuona nakala za barua alizonazo yeye ili kuondoa uwezekano wa wahusika kuificha Ofisi yako kwa kuasisi barua nyingine zilizogushiwa!.

Kuna hisia kuwa baadhi ya wakubwa ndani ya Uongozi wa Halmashauri, Uongozi wa Chama Cha Waalimu na Jeshi la Polisi kule Morogoro wanashirikiana kutaka kumkandamiza Witness ili kuficha mambo mengi. Ofisi ya Haki ya Askofu Mwamakula imepata kuona nakala zote za barua alizoandikiwa Witness Makoti.

Tunapenda wahusika waelewe kuwa suala la Witness Makoti sasa lina maslahi ya umma, hivyo kufanya jambo lo lote la kutaka kufinya haki zake halitafanikiwa! Inakuwaje mtu aliyepigwa, aliyevunjwa jino, aliyelalamika na jambo likafika Polisi halafu mtu huyo huyo anatishwa asiende Mahakamani na baadaye anasimamishwa kazi na kugeuziwa tuhuma?

Ni jukumu letu kupaza sauti kwa ajili ya wale wote wanaonyimwa haki na kuonewa (Isaya 61:1-3).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Nimeicopy
 
Tena Kama ndo waalimu nashauri viboko vitumike kuwafundisha weledi maana huwa wanatumika kuhujumu uchaguzi kwa kupewa posho ya kuwa karani wa uchaguzi.
 
Miaka 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika bado watanganyika wapo kwenye manyanyaso, udhalilishaji na uonevu chini ya utawala wa mkoloni mweusi (CCM).

Dawa hapa ni kupachimbisha kwa style ya Hamza.

Namshauri huyo mwalimu aliyepigwa mpaka kutolewa jino, naye ikiwezekana ajipange kung'oa jicho la mtu, ili twende sawa.
 
Watu TSC wanakwazaga sana..wapo kukandamiza walimu tu, ishatokea mahala Fulani walimu wamepigna aliyepigwa akaenda polisi wakaenda pale kazini wakamlazimisha aliyepigwa afute kesi.
Sijui kwa nini wako hvyo yaani wanakandamiza sana...

Nampa pole huyo Dada!akifanya masihara atatengezewa zengwe afukuzwe kazi
 
Back
Top Bottom