Wizara za Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi; Viwanda na Biashara zinahitaji Mawaziri Wabunifu!

Musoma

Senior Member
Oct 12, 2010
137
221
Ukizitazama Wizara nilizozitaja hapo juu kwa makini utabaini kuwa Mafanikio katika Serikali ya Rais John Pombe Magufuli yatategemea sana ufanisi katika Wizara hizo! Hizo ndizo Wizara zenye fursa nyingi ambazo zikipata Viongozi makini wenye maarifa, ubunifu na uthubutu basi zinaweza kabisa kubadili maisha ya Watanzania na Uchumi wa Nchi yetu! Mfano tunaposema Tanzania hatujitoshelezi kwa Sukari,Mafuta ya Kula n.k ,hapo tunazungumzia fursa mpya za ajira na vyanzo vipya vya mapato ya Nchi. Leo zao la Pamba ambalo linaweza kutoa ajira zaidi ya Milioni kadhaa katika mikoa zaidi ya 14 hapa Nchini limeachwa kufa bila mipango yoyote ya maana! Ginners (Wenye viwanda vya kuchambulia pamba/Ginneries) wamefilisika kutokana na uzalishaji mdogo wa pamba ya kuendeshea viwanda hivyo.Nenda Chato Ginnery ,Bulamba Ginnery,Sangu Ginnery ,Nyakabindi Ginnery n.k Viwanda (Ginneries) ziko under- utilized kwa kuwa hakuna uzalishaji wa kutosha ktk zao la pamba! Halafu bado kuna watu wanashangilia "comedy" za eti Waziri kuvamia machinjio ya mbuzi usiku wa manane kuona ni mbuzi wangapi wanachinjwa bila vibali! Mambo madogo madogo ambayo yanaweza kusimamiwa na Halmashauri za Miji na Majiji tu ! Kwenye Viwanda na Biashara,Waziri hana vision,ni porojo nyingi tu! Kama vile mara tumepata soko la mihogo tani milioni sijui mia ngapi Dubai,Oooh mara mambo mazuri yanakuja kaeni mkao wa kula! Hopeless! Tunahitaji Strategic "Industrial Development Masterplan" inayosimamiwa na "Industrial Guru" as a Minister ! Hatutaki Mawaziri wa Masifa ya kipuuzi na Porojo tu!
 
Miaka mitano ya Magufuli imeshaisha tayari. Hakuna jipya litakalokuja.

Mjiandae kupiga kura tena 2020.
 
Viongozi ni walewale ambao wameshindwa kuwa wabunifu miaka yote leo ndo wakulete jambo jipya?
 
Sijui viongozi wetu wanakwama wapi, mbona mifano ni mingi sana, au bado kila mtu anawaza vilevile chukua chako mapema
 
Back
Top Bottom