Wizara yatahadharisha ongezeko Wagonjwa wa Figo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema tatizo la ugonjwa wa figo nchini linaongezeka na takwimu zinaonesha Tanzania ina wagonjwa 600,000.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dk Linda Ezekiel, aliyasema jana wakati akizungumza na HabariLEO kuhusu maadhimisho ya wiki ya kuzuai magonjwa yasiyoambukiza.

Dk Linda pia ni mratibu wa magonjwa ya figo wa Wizara hiyo.

Alisema chanzo kikubwa cha magonjwa ya figo ni kisukari, shinikizo la juu la damu, homa ya ini, maambukizi ya Ukimwi na maambukizi ya magonjwa mengine ya bakteria hususani UTI.

Kwa mujibu wa Dk Linda idadi ya wagonjwa wa figo nchini inaongezeka. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 0.1 ya idadi ya watu barani Afrika wana magonjwa ya figo.

Kutokana na takwimu hizo, Dk Linda alisema kwa kuwa idadi ya watu Tanzania inafikia takribani watu milioni 60, idadi ya wagonjwa wa figo nchini wanafikia 600,000.

Alisema takwimu za hospitali hazitoi picha halisi kwa kuwa wagonjwa wengi wanaokwenda hospitali wanakuwa katika hatua ya kupata huduma ya kusafishwa figo.

“Mwakani Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na WHO, watafanya utafiti mkubwa nyumba kwa nyumba kwa maeneo yatakayochaguliwa ili kuangalia kuna mfumo gani wa maisha ikiwemo uvutaji wa sigara, aina ya vinywaji anavyotumia, aina ya mazoezi anayofanya, shughuli anayofanya na lishe ili kubaini mambo yanayomweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa ya figo,” alisema Dk Linda na kuongeza:

“Pia kujua kama mtu yeyote kwenye kaya husika ana tatizo la shinikizo la juu la damu, kisukari, uzito uliozidi au maambukizi, kwa kuwa vitu vyote hivi vinaweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya figo.”

Kazi ya figo
Kwa mujibu wa Dk Linda alisema, kazi kubwa ya figo ni kuondoa vitu visivyohitajika mwilini kwa njia ya mkojo kwa kuwa taka zikizidi mwilini zinamfanya mtu kuwa na kichefuchefu au kuwa na usingizi sana au kuwa na hali ya kuchanganyikiwa.

Alisema figo pia ina kazi ya kutengeneza kemikali muhimu kwa ajili ya kuongeza chembechembe nyekundu za damu.

Dalili za ugonjwa
Dk Linda alisema, figo zikishindwa kufanya kazi zinasababisha upungufu wa damu.

Dalili nyingine ni mtu kuvimba uso, tumbo na miguu, pia figo husaidia madini ya kalsiamu kufyonzwa mwilini kwa ajili ya kuimarisha mifupa na misuli, hivyo figo zinaposhindwa kufanya kazi husababisha mifupa na misuli nayo kuathirika.

Alitaja dalili nyingine ya magonjwa ya figo ni mtu kutopata mkojo kabisa au anaweza kutoa mkojo ambao hauna uchafu kwa kuwa figo inakuwa haina uwezo wa kuchuja taka.

Hatua za ugonjwa
Dk Ezekiel alisema kuna hatua tano za mtu kuugua magonjwa ya figo kwa kuzingatia umri, uzito na kipimo cha damu ambacho mgonjwa anafanyiwa ili kujua kiwango cha uchujaji wa figo kwa dakika.

Alisema figo ina uwezo wa kuchuja mililita 125 za damu kwa dakika, hivyo hatua ya kwanza ya ugonjwa wa figo ni uwezo wa figo kuchuja mililita 60-80 za damu kwa dakika, hatua ya pili ni mililita 45-60, hatua ya tatu ni mililita 45-30, hatua ya nne mililita 30-15 na hatua ya tano ni chini ya mililita 15.

“Hatua ya kwanza mpaka ya tatu ya ugonjwa wa figo inaweza kudhibitiwa vizuri kwa kuwa zipo dawa nzuri, lakini pia mgonjwa hapaswi kula vyakula vyenye mafuta mengi, kudhibiti uzito, kutokunywa pombe na kuvuta sigara,”alisema Dk Linda.

Alisema vipimo vya magonjwa ya figo vinapatikana kwenye hospitali zote za Mikoa, Kanda na Taifa.

Gharama za tiba
Alisema gharama ya matibabu ya figo ni kubwa kwa kuwa kupandikiza figo nchini ni Sh milioni 30 na endapo mgonjwa ataenda nje ya nchi gharama zinakuwa mara tatu zaidi.
 
Huko mashenzini tunakoishi mtu atajuaje kuwa anaanza kupata tatizo la figo ie ni dalili gani za mwanzo.
 
kwahiyo kumbe lile swala la figo kuuzwa bei nzuri doctor anakazia kabisa.
 
Hivi hata hivi vinywaji vya kemikali tunavyonyeeshwa na hawa tunaowaita mabilionea hapa nchini, vipi salama kweli? Maana sijawahi kuviona wenyewe wakivitumia
 
Duuuh....Kumbe Hadi shinikizo la damu pia linasababisha magonjwa ya Figo..Noma sana
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema tatizo la ugonjwa wa figo nchini linaongezeka na takwimu zinaonesha Tanzania ina wagonjwa 600,000.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dk Linda Ezekiel, aliyasema jana wakati akizungumza na HabariLEO kuhusu maadhimisho ya wiki ya kuzuai magonjwa yasiyoambukiza.

Dk Linda pia ni mratibu wa magonjwa ya figo wa Wizara hiyo.

Alisema chanzo kikubwa cha magonjwa ya figo ni kisukari, shinikizo la juu la damu, homa ya ini, maambukizi ya Ukimwi na maambukizi ya magonjwa mengine ya bakteria hususani UTI.

Kwa mujibu wa Dk Linda idadi ya wagonjwa wa figo nchini inaongezeka. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 0.1 ya idadi ya watu barani Afrika wana magonjwa ya figo.

Kutokana na takwimu hizo, Dk Linda alisema kwa kuwa idadi ya watu Tanzania inafikia takribani watu milioni 60, idadi ya wagonjwa wa figo nchini wanafikia 600,000.

Alisema takwimu za hospitali hazitoi picha halisi kwa kuwa wagonjwa wengi wanaokwenda hospitali wanakuwa katika hatua ya kupata huduma ya kusafishwa figo.

“Mwakani Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na WHO, watafanya utafiti mkubwa nyumba kwa nyumba kwa maeneo yatakayochaguliwa ili kuangalia kuna mfumo gani wa maisha ikiwemo uvutaji wa sigara, aina ya vinywaji anavyotumia, aina ya mazoezi anayofanya, shughuli anayofanya na lishe ili kubaini mambo yanayomweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa ya figo,” alisema Dk Linda na kuongeza:

“Pia kujua kama mtu yeyote kwenye kaya husika ana tatizo la shinikizo la juu la damu, kisukari, uzito uliozidi au maambukizi, kwa kuwa vitu vyote hivi vinaweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya figo.”

Kazi ya figo
Kwa mujibu wa Dk Linda alisema, kazi kubwa ya figo ni kuondoa vitu visivyohitajika mwilini kwa njia ya mkojo kwa kuwa taka zikizidi mwilini zinamfanya mtu kuwa na kichefuchefu au kuwa na usingizi sana au kuwa na hali ya kuchanganyikiwa.

Alisema figo pia ina kazi ya kutengeneza kemikali muhimu kwa ajili ya kuongeza chembechembe nyekundu za damu.

Dalili za ugonjwa
Dk Linda alisema, figo zikishindwa kufanya kazi zinasababisha upungufu wa damu.

Dalili nyingine ni mtu kuvimba uso, tumbo na miguu, pia figo husaidia madini ya kalsiamu kufyonzwa mwilini kwa ajili ya kuimarisha mifupa na misuli, hivyo figo zinaposhindwa kufanya kazi husababisha mifupa na misuli nayo kuathirika.

Alitaja dalili nyingine ya magonjwa ya figo ni mtu kutopata mkojo kabisa au anaweza kutoa mkojo ambao hauna uchafu kwa kuwa figo inakuwa haina uwezo wa kuchuja taka.

Hatua za ugonjwa
Dk Ezekiel alisema kuna hatua tano za mtu kuugua magonjwa ya figo kwa kuzingatia umri, uzito na kipimo cha damu ambacho mgonjwa anafanyiwa ili kujua kiwango cha uchujaji wa figo kwa dakika.

Alisema figo ina uwezo wa kuchuja mililita 125 za damu kwa dakika, hivyo hatua ya kwanza ya ugonjwa wa figo ni uwezo wa figo kuchuja mililita 60-80 za damu kwa dakika, hatua ya pili ni mililita 45-60, hatua ya tatu ni mililita 45-30, hatua ya nne mililita 30-15 na hatua ya tano ni chini ya mililita 15.

“Hatua ya kwanza mpaka ya tatu ya ugonjwa wa figo inaweza kudhibitiwa vizuri kwa kuwa zipo dawa nzuri, lakini pia mgonjwa hapaswi kula vyakula vyenye mafuta mengi, kudhibiti uzito, kutokunywa pombe na kuvuta sigara,”alisema Dk Linda.

Alisema vipimo vya magonjwa ya figo vinapatikana kwenye hospitali zote za Mikoa, Kanda na Taifa.

Gharama za tiba
Alisema gharama ya matibabu ya figo ni kubwa kwa kuwa kupandikiza figo nchini ni Sh milioni 30 na endapo mgonjwa ataenda nje ya nchi gharama zinakuwa mara tatu zaidi.
Ugonjwa wa figo ni mbaya sana kuliko Covid-19 lakini WHO wamekomalia Covid-19 tuuu!!
 
Back
Top Bottom