Wizara ya Uwekezaji ni balaa sijui kama itakuja kusimama

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Ninakumbuka Waziri Angela Kairuki alivyopewa tu Wizara hii basi huyo akachikichia shimoni kutoka siasani. Wizara hii wakati huo ikiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mara baada ya Kairuki kuchikichishwa shimoni ikaonakena kuboresha mambo ya uwekezaji Wiazara hiyo ikavutwa kwa Mh. Rais mwenyewe lakini nako huko ikiwa na Kitila Mkumbo hata haikuonekana inafanya nini.

Hatiamaye awamu ya sita ikarudishwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Kitila Mkumbo akahurumiwa kupewa ya viwanda. Ikiwa kwa Waziri Mkuu akapewa Mambe yule amabaye alishawahi kuwa Mtendaji Mkuu wa TIC lakini nako ikaonekana haizai kabisa yaani imedumaa kwa utasa na mambo ya uwekezaji yakawa ndiyo kama vile yanafanywa na Rais mwenyewe.

Sasa Rais akaona hiyo haitoshi kwa mpigo akamchikishia shimoni Mambe na Kitila wake na kumpa mwanamke na kuirudisha Uwekezaji kule ilipokuwa zamaani yaani Viwanda na Biashara ikiwa imeshakula vichwa vya kutosha inclusive Mama Mwaluko aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hii.

Hakika Uwekezaji ni balaa mnoo! Sijui kama itakuja kusimama!
 
Back
Top Bottom