Wizara ya Utamaduni na Utalii: Nimeandika makala nzuri ya Morogoro, nimepigiwa simu na makampuni tisa ya utalii Arusha wakiuliza namna ya kufika

Mtu kama huyu na ma- degree yake anaitia aibu sana CCM! Huyu hana tofauti na yule Mama Naibu Waziri wa Fedha!
Eti Wizara ya Utamaduni na Utalii!

Mtu kama huyu anavyojipendekeza usijekuta akiteuliwa kuwa DC na kichwa chake "cheupe" hicho!
 
WIZARA YA UTAMADUNI NA UTALII:NIMEANDIKA MAKALA NZURI YA MOROGORO,NIMEPIGIWA SIMU NA MAKAMPUNI TISA YA UTALII MKOANI ARUSHA,WAKIULIZA NAMNA YA KUFIKA MLIMA ULUGURU NA KUPATA HISTORIA YA MOROGORO.

Leo 19:45hrs 13/02/2021

Historia ni somo pana sana kama yalivyo masomo mengine,lakini wote tukubaliane kwamba ili tuweze kujivunia utaifa wetu, somo la historia ni muhimu sana katika kuchochea uzalendo kwa Taifa letu la Tanzania,hivi leo Tindu Lissu ameungana na Wazungu kuipiga vita Tanzania,pengine hajui historia ya Tanzania,pengine hajui kama Mjerumani Carl Peter's Mkono wa Damu,alimkata kata Mangi Meli na kuchukua kichwa cha Mangi Meli wakakiweka kwenye begi wakakipeleka Ujerumani kwa uchunguzi kujua Mangi Meli alikuwa binadamu wa namna gani,pengine hajui kama Kinjekitile Ngwale anachukuliwa kama ishara ya Upinzani dhidi ya Mjerumani,

Pengine Tindu Lissu hajui kuwa Chifu Mkwawa Mkwavinjika Mwamuyinga alizaliwa 1855 na akaitwa Ndesalasi, maana yake "Mtundu au Mdadisi"
Katika utu uzima aliitwa Mtwa Mkwava Mkwavinyika Mahinya Yilimwiganga Mkali Kuvago Kuvadala Tage Matenengo Manwiwage Seguniwagula Gumganga,maana yake: "Mtawala, mtekaji wa nyika,mkali kwa wanaume mpole kwa wanawake asiyetabirika, alieshindikanika, mbabe mwenye nguvu,udongo pekee ndio utakomuweza"Alipewa jina hilo mnamo 1887,baada ya vita na kabila la Wangoni kutoka Songea
Wajerumani walilifupisha jina hili na kumuita Mkwawa,wakilitamka "Mkwava" - lakini sasa linatamkwa Chifu Mkwawa Mkwavinjika Mwamuyinga.

Historia inakufanya ujue ulikotoka, ulipo na unakoelekea, historia inakufanya umjue adui yako na Rafiki yako, Kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu, upeo na kujitambua sioni kama anaweza kuungana na mzungu kuipinga Tanzania na kuitakia mabaya,aidha Taifa lolote kuwafanya watu wake na ikiwezekana ulimwengu mzima kujua historia ya Tanzania si jambo geni na halitaanzia kwetu,wakati tunasoma,tumesoma historia za mataifa,tawala na falme nyingi tu duniani,tumesoma historia za Ulaya, Amerika, Falme za Ottoman,hata sasa kwa wanaoangalia Azam tv,moja ya vipindi vyao vilivyo na watazamaji wengi ni pamoja na tamthilia za kituruki zinazorushwa kuanzia saa nne usiku,

Ukifuatilia tamthilia hizi unaona kabisa waturuki wanavyohifadhi na kusambaza historia ya taifa lao kwa njia za kisasa,kabla ya tamthilia ya sasa "Etugrul"kuna tamthilia iliyojulikana kwa jina la "Sultan" tamthilia hii iliyokuwa ikielezea historia ya Falme ya Ottoman(Ottoman Empire, 13-19 Century),ni moja ya tamthilia iliyofuatiliwa sana hapa Tanzania na nchi nyingine nyingi kama vile Pakistan na kwingineko duniani,lakini wakati sisi tunaangalia tamthilia hizi na kufurahia,taifa la Uturuki linatimiza adhma yake ya kueneza historia yake ulimwenguni kupitia njiaa hii ya kisasa ya tamthilia,

Hivyo basi Taifa letu la Tanzania ni wakati mwafaka kuifanya historia ya nchi yetu ijulikane ndani na nje ya nchi yetu kupitia short filamu au tamthilia za Machifu,mfano historia ya Waluguru,Chifu wao wa kwanza Chifu Msumi,Chifu Lukwele ambae alikabidhiwa Uchifu baada ya kurudi kutoka vita ya kwanza ya Dunia,Chifu Lukwele aliyezikwa katika makaburi ya Kichangani mtaa maarufu na wa heshima ambapo Mbaraka Mwishehe alikaa hapo na bendi maarufu za Moro Jazz na Cuban Marimba zikiwa na studio zake mtaa huo,akafuatiwa na Chifu Kingalu rafiki mkubwa wa Mh Jakaya Kikwete hata alikwenda kumzika Kijijini Kinole,Morogoro Vijijini hadi huyu Chifu Kingalu wa sasa ambae jina lake na kwa heshima ya Chifu Kingalu, Rais John Magufuli amelipa soko kuu la Morogoro,

Watanzania wanaopingana na kuanzishwa kwa historia ya Tanzania na bado wakaenda kujifunza historia ya nchi nyingine hasa za kibeberu,hao wametekwa na kasumba za utumwa, za kudharau kilicho chetu na kutukuza cha wakoloni,tatizo letu kubwa ukienda Morogoro leo hujui wapi uanze kuupanda Mlima Uluguru,uende Bahati Camp,Camp maarufu ya Skauti Tanzania,Uende Morning Site,Uende kwenye jiwe lenye nne ya kirumi,hakuna Makumbusho au mahali maalum panapoelezea historia ya Morogoro mfano Henry Morton Stanley aliishi Morogoro mwaka 1800 maeneo ya Kihonda ilipo sasa shule ya Sekondari ya Kayenzi,uwezi kuona picha za majengo aliyojenga Jasusi Henry Morton Stanley baada ya kupewa eneo na Chifu Simbamweni mtoto wa Chifu Kingo Kisebengo,huwezi kujua wapi ni makao Makuu ya Chifu Kingalu kwa sasa,Wizara ya Utalii na Wizara ya Utamaduni mna kazi kubwa sana ya kufanya.

-Rejea Makala ya kumkaribisha Rais Magufuli,Mkoani Morogoro.

KARIBU RAIS JOHN POMBE MAGUFULI,KARIBU MOROGORO KWA CHIFU KING'ALU MWANA WA CHIFU MSUMI.

Leo 20:30hrs 11/02/2021

Karibu Rais John Pombe Magufuli,Karibu katika Mji wa Kihistoria,Karibu Morogoro,mahali ambapo Safina ya Nuhu ilitia nanga baada ya Gharika kuu iliyoua watu wote duniani,karibu Mkoa wa Morogoro ambao eneo kubwa ni hifadhi za Wanyama wote,Ndege wote,na viumbe vyote vilivyotoka kwenye Safina ya Nuhu na kuifanya mbuga maarufu ya Mikumi,Udizungwa na Julius Nyerere (Selous Game Reserve).Kabila kubwa katika Mkoa wa Morogoro ni Waluguru waliotoa jina kwa Mji wa Morogoro,pamoja na Milima ya Uluguru,

Makabila mengine makubwa ni Wakagulu,Wapogolo,Wandamba na Wakutu,karibu nusu ni Waislam na nusu ni Wakristo,Historia ya Wabunge wa Morogoro inaanzia kwa Amir H Jamal 1965-1985 huyu ndiye Waziri wa muda mrefu katika Wizara ya Fedha,Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere,Wabunge wengine ni Shamim Khan 1985-1995,Luteni Kanali Mazola1995-2000,Eng Oscar Thobias Mloka 2000-2005,Daktari Omar Mzeru 2005-2010,Aziz Abood 2010-2025.

Asili ya neno Morogoro ni mluguru, hii ni baada ya Jasusi Mbobezi Henry M Stanley kushindwa kutamka Mluguru na kuongelea kooni na kutoka sauti iliyosikika "Moro-goro" Jasusi Henry M Stanley alipita katika safu za milima ya Uluguru njia ya Kaskazini Mwaka 1874 akiambaa hadi Mashariki ya milima ya Uluguru,Katikati ya milima ya Uluguru, Henry M Stanley alikutana na jeshi la Simbamweni mtoto wa Kingo Kisebengo, katika mji uliozungushiwa ukuta na kuwa na ngome isiyopenyeka kiurahisi, baada ya kuonekana ni mtu mwema alipokelewa na Mwenyeji wake Chifu Simbamweni,

Jasusi Henry M Stanley aliusifu mji huo uliokuwa chini ya bonde la milima ya Uluguru, akisema mji huo umejengwa kwa mitindo ya kiarabu chini ya bonde la kijani la milima ya Uluguru,yenye misitu minene inayofunikwa na mawingu wakati wote wa Mwaka,Milima iliyopambwa na mito miwili mikubwa inayokwenda kuzaa mto Ruvu, uliounganishwa na utitiri wa vijito vya maji safi na salama, Jasusi Henry M Stanley katika kitabu chake "How I found Livingstone" chapter 4 na 16 anakiri mandhari ya milima ya Uluguru hajapata kuyaona katika eneo lolote alilowahi kufika katika Afrika Mashariki,

Rejea pia kitabu cha Joseph Thomson:'To The Central Africa Lakes and Back' 1881chapter 1 na 5 kinachoelezea Jeshi kali la Waluguru lilikuwa linavaa majani ya mgomba na magome ya miti,Thomson akiwa na Baba yake Keith Johnson wakitokea eneo la masai na Ziwa Victoria,wakiingia pwani katika eneo la Waluguru na wakutu Mwaka 1879 anasema hakuwahi kukutana na Waluguru zaidi zao toka kwa Majeshi mengine ya wambuga hadi pale alipokuja kufahamu walikuwepo wengi katika njia aliyopita lakini walivaa majani ya mgomba na kufanana na majani na miti ya porini,

- Historia ya Chief Kingalu,Kiongozi wa Waluguru.

Historia ya Chifu Kingalu inaanzia kwa Chifu Lukwele wa Choma aliyezaliwa mwaka mwaka 1852 na kufariki mwaka 1971, na kuzikwa katika makaburi maarufu wakati huo ya kichangani mjini Morogoro

Chifu Lukwele ndiyo yule askari mwenye historia ya kupigana katika jeshi la Mjerumani dhidi ya Waingereza na washirika wao, kwenye maeneo kadhaa ya Mashariki ya Kati uko uarabuni, Afrika Mashariki, Msumbiji, Malawi na hatimaye Namibia, na kurejea nchini baada ya vita ya kwanza ya Dunia kumalizika katika muongo wa pili wa karne ya 20.

Chifu Lukwele ambaye jina lake halisi ni Salum Bin Msumi, alikuwa ni mmoja kati ya watoto watatu mashuhuri wa Chifu Msumi wa Kibungo, ambaye asili yake kwa baba ni Mluguru na mama ni Mzulu toka Afrika Kusini.

Chifu Msumi aliyeitawala kibungo juu na kibungo chini katika milima ya Uluguru rekodi yake ya ndoa na watoto inaonesha kuwa ni mtu wa mitala, na alikuwa na watoto wengi, zaidi ya 30 katika milima ya Uluguru Mkoani Morogoro, Mbambabay Mkoani Ruvuma na jijini Lilongwe nchini Malawi.

Watoto mashuhuri wa Chifu Msumi ni Lukwele (Salum), Sonanga, na Mleke maarufu kama Kingalungalu (waluguru wanatamka ‘Chingalungalu' yaani Kigeugeu) au kwa kifupi Kingalu wa kwanza, ikiwa ni jina lake la kupanga kutokana na tabia yake ya Ugeugeu (aliwahi kumgeuka mkwewe chifu magoma, na kisha baba yake mzazi Chifu Msumi na kupigana nao vita kali kwa nyakati tofauti!akitaka kuongoza safu yote ya milima Uluguru)

- Kutokana na ubabe na nguvu jina la Kingalu hilo likawa jina rasmi la ukoo ambalo litatawala Waluguru.

Kutoka ukoo wa Chifu Msumi tunaweza pia kupata makabila mengine yaliyotika katika koo ya Kiluguru kama Wazaramo, Wakaguru, Wakutu na Wakwere, wote wakifuata mfumojike (kwa Kiingereza ''matrilinear'') yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Katika kupata jina la mtoto anayezaliwa, mtoto wa Kiluguru huitwa jina la ukoo wa baba yake, ambao ndio ukoo wa bibi mzaa baba. yaani, Waluguru wana 'mtala' na ukoo. Mtala ni jina la ukoo wa baba ambalo ndilo analoitwa mtoto.

Kwa mfano, mtoto akiitwa 'Kobero' jina hili ni mtala, si jina la ukoo wake, kwani 'Kobero' ni jina analopewa mtoto ambaye baba yake ni 'Mmande'. Hali kadhalika, mtoto akiitwa 'Mkude' jina hili ni mtala wa ukoo wa 'Wamwenda', lakini si jina la ukoo wa mtoto. Hivyo basi, kwa Waluguru baba hutoa jina na mama hutoa ukoo, jina ni la ukoo wa baba, na ukoo ni wa mama!

- Nne ya Kirumi iliyochorwa na Mjerumani katika kilima kimojawapo cha Mlima wa Uluguru.

Alama ya ushindi baada ya kuupanda Mlima Uluguru sasa inaelekea kufutika katika Mwamba
wa kilele cha Lupanga, ni historia nyingine ya kukumbukwa kwa kila aliyepanda Mlima wa Uluguru na kupiga picha katika eneo hilo ambalo linaonekana vizuri ukiwa chini katikati ya Mji wa Morogoro,

Kilele cha Lupanga kinachotiririsha maji kikiwa na mita 2,150 toka usawa wa bahari ni cha pili kwa ukubwa katika Mlima Uluguru wenye urefu wa Mita 2,630. Tukiwa Scout wenzangu wa kutoka shule za msingi na Sekondari miaka ya 1990 ilituchukuwa saa tisa kufika kileleni,

Ilituchukua saa tatu kushuka, lakini kwa wengi huwachukuwa saa 11.30 hadi 12 kupanda hadi kwenye kilele iko cha Lupanga chenye nne ya kirumi na saa tano na nusu hadi sita kushuka, kushika kilele hicho ni kazi kubwa na hatari zaidi kuliko kuupanda!).

Katika eneo lenye nne ya kirumi (alama IV) uwa kazi zaidi kupanda, kwani muinuko wake baadhi ya maeneo hufika nyuzi tisini, kiasi cha kutegemea mashina ya miti na mizizi kukuwezesha kusonga mbele.

Kihistoria eneo hili lilikuwa chini ya Mamlaka ya Utawala wa Choma (kabla ya Ukoloni kuchukua hatamu) kwenye eneo la Uangalizi wa Mndewa (Sub-Chief) wa Kibwe ambaye ni Sayyid (His Royal Highness) Mwande.

Nilipata bahati ya kupitia nyaraka za utawala wa Choma (Royal Achieves) sikupata chochote juu ya maana ya alama hii (IV), japo ninavyofahamu iliwekwa na Wajerumani miaka takriban 100 iliyopita wakati vita ya Dunia ikianza kunguruma,lakini niligundua ilimaanisha ushindi wa kupanda Mlima Uluguru na kufikia kilele iko cha Lupanga.

-Boka, nyoka mwenye vichwa saba, anayepatikana katika milima ya Uluguru.

Nikiwa likizo moja kijijini kwetu Tawa, Matombo, Morogoro Vijijini miaka ya 1990 tuliamka asubuhi na kukuta mto Mmanga umejaa mara mbili zaidi ukiharibu kingo za ukuta, nyumba za watu, mashamba, ukichukua mbuzi, kondoo, kuku na kila kilichoonekana mali ya wanakijiji pembeni ya mto Mmanga uliokuwa ukitiririsha maji yake kuelekea mto Mfizigo ambao ulipeleka maji katika mto Ruvu uliokwenda kuingia baharini,

Tulipouliza waliokaribu na mto walikiri kusikia miluzi, makofi na vigelegele usiku wa manane huku kishindo kikubwa cha mtiririko wa maji kikisikika katika mto Mmanga, baadae wazee wa mila walikiri kupita kwa nyoka aina ya boka mwenye vichwa saba, akimeremeta na kung'aa mithili ya nyota za angani, akiwa safarini kuelekea baharini.

Wazee walitueleza makazi ya nyoka huyo ambayo uwa ni Mlimani na karibu ya vyanzo vya mito mikubwa,mahali anapokaa uwa panabarikiwa sana mafuta, na ithibitisho wa hilo alipita kwe mto usiku basi asubuhi utakutana na harufu ya petrol na mafuta ya taa, ikieleza mahali alipotoka ameacha hazina hiyo ya mafuta.

Kwa watu wanaokaa maeneo hayo mfano kabila la walugulu wanalifaham hilo, Nyoka huyo uwa na maisha ya kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine na katika safari zake inasadikika anatoka milimani na kuelekea baharini kupitia katika maporomoko ya maji na vijito vidogovido.

Kipindi cha masika au mvua kubwa ndio mida anaotumia kwa kipindi cha miaka kumi ndipo hayo yanatokea, katika maeneo hayo karibu na vijiji jirani kuna matokeo ya watoto kuumwa kipindi tuu nyoka huyu anapofanya safari zake,

Mwaka 1984 nyoka huyo alionekana akiondoka kuelekea baharini kwa njia ya moshi baada ya kutiririka na maji yaliyokwenda kutuwama katika bwawa la Mindu,na katika miaka ya tisini ikiwa kina cha maji kimepungua na nguvu ya maji kuwa ndogo alionekana maeneo ya kilima cha Lupanga akichukuliwa na mnyororo mkubwa kuelekea baharini,

Nimalizie kwa kusema ni furaha ya watu wa Morogoro leo kulala na Rais John Magufuli toka alivyofanya hivyo Rais Julius Nyerere,Morogoro ni mji wa Kihistori,ukiwa Kiongozi ni lazima ujue historia ya Morogoro ili uweze kujua ilipotoka Morogoro na inapotakiwa kuipeleka Morogoro,

Kama Mbunge wa Morogoro inamlazimu sana angeliijua Morogoro na kuitangaza historia yake vyema,pengine kwa viongozi wa kawaida (wa kiserikali au kisiasa) hadi wanakufa wengi hawajayajua na kushindwa kuipeleka mbele Morogoro iliyokuwa Mji toka Mwaka 1928 lakini hadi leo 2020 Morogoro bado ni Mji ule ule,

Morogoro ilikuwa Halmashauri Mwaka 1928 kabla ya Dar es Salaam, mpaka leo Morogoro ilitakiwa iwe imeshatoka kwenye Uhalmashauri na kuwa Jiji,

Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanapita hapo Morogoro wanakuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine, Je Morogoro mmeshindea kutengeneza hub iwe kama Kariakoo ndogo mkichukua vitu vyote vya Kariakoo vipatikane hapo!?

Viongozi wa Morogoro walipaswa waitangaze vilivyo kwamba Morogoro ni Kariakoo ndogo na hakuna sababu ya kupita Morogoro kwenda Dar es Salaam kilomita 200 wakati vitu vyote vinapatikana Morogoro,

Tukiweza kuwapata awa Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine,

Tutakuwa tumepata dola, hivyo biashara ya fedha ya kigeni itashamiri Morogoro kubadili dola kuwa shilingi na shilingi kuwa dola, hakuna biashara hapa Kariakoo inayowatajirisha watu haraka kama biashara hiyo ya dola,

Tukiweza kuwapata awa Wazambia,Wamalawi,Wazimbabwe,Wamsumbiji,Wakongo,Waburundi,Warwanda,Waganda,Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu,nguo,mikoba,na bidhaa nyingine,

Tutakuwa tumeleta mzunguko wa fedha hapo Morogoro naamini hakuna kijana atakayekosa kazi,Miaka ya nyuma Morogoro ilipata kuwa hub ya kikazi na kibiashara, People were flocking from all over East Africa coming to Morogoro,

Hii ilisababishwa na Uwepo wa kivutio cha muziki bora katika East Afrika,mziki ulioongozwa na Mbaraka Mwishehe na bendi maarufu kabisa za Cuban Marimba na Morogoro Jazz,

Hii ni changamoto kwa kila kiongozi katika Mkoa wa Morogoro (japo una hiyari ya kuyafanyia kazi au kuyaacha kutegemea na Utamaduni, Jiografia, Mazingira, Wakati, na mipaka ya Kiuchumi).
Kila jambo hufunzwa na falsafa yake, mathalani italeta Maendeleo na tija kwa Taifa la Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Leslie Mbena,
Morogoro.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Huu muda wakuandika upuuzi unaupata wapi?
 
Yaani makampuni ya kitalii yamuulize MATAGA jinsi ya kufika mt. uruguru?
Huyu MATAGA hajui kampuni za kitalii ni taasisi,ina watalamu wa kila kitengo.
 
Bora mabeberu yalitutesa lakini sasa yanatupa msaada,kuliko beberu jeusi linauwa na kupendelea kwao.

"Ww kijana acha kutegemea ajira, jiajiri mwenyewe"
Job Ndugai☝️
 
Back
Top Bottom