Wizara ya Utalii ni kaa la moto, kunani? Uchambuzi huu hapa…

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
276325164_311817421020424_2019938553811014678_n.jpg


Mabadiliko madogo ya mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, jana Machi 31, 2022 yamemuweka Waziri Pindi Chana kwenye wizara yenye “moto”.

Wizara hiyo yenye historia ya “kuwakaanga” mawaziri kwa kashfa na wengine kushindwa hata kumaliza mwaka mmoja si nyingine ni ya Maliasili na Utalii.

Pindi ambaye alikuwa balozi wa Tanzania nchini Kenya amekwenda kushika kijiti kilichoachwa na Damas Ndumbaro.

Historia inaonesha kuwa mawaziri wengi walioshika nafasi ya uwaziri kwenye wizara hiyo wengi hawakuvuka kigingi cha miaka mitatu isipokuwa Zakhia Meghji aliyeupiga mwingi kwa miaka takriban minane.

Lakini Ndumbaro, Hamis Kigwangalla, Lazaro Nyalandu, Khamis Kagasheki hawakuweza kufurukuta katika wizara hiyo na kujikuta waking’olewa.

Wengine ni Ezekiel Maige (2010-2012), Shamsa Mwangunga (2008-2010), Jumanne Maghembe (2007-2008), Anthony Diallo (2005-2006), Zakhia Meghji(1997-2005), Juma Ngasongwa (1995-1996), Juma Omar (1993-1995), Abubakar Mgumia (1990-1993) na Marcel Komanya (1989-1990).

Arcardo Ntagazwa (1987-1989), Getruda Mongela (1985-1987), Paul Bomani (1984-1985), Geogre Kahama (1983-1984), Ali Hassan Mwinyi (1982-1983), Isaack Sepetu (1980-1982).

Wengine ni Solomon Saibul (1975-1980), Hosnu Makame (1970-1975), Dereck Bryceson (1965-1970) na Tewa S. Tewa (1962-1965).

Inaonekana kwa mbali mawaziri wa zamani walimudu lakini hawa wa sasa hawajaonesha maajabu, wewe unafikiri tatizo ni nini hebu mpe ushauri waziri mpya Pindi Chana anatokaje kwenye mtego huu?



Chanzo: Global Publishers
 
Kuna wizara ngumu kuliko Mambo ya Ndani? Nilitazama historia ya Mawaziri wake, Ukitoboa miaka 3-4 wewe ni mwanaume! Nadhani inafuata hii ya Maliasili.
George Kahama19611962(Republic of Tanganyika)
Oscar Kambona.png Oscar Kambona19621963
1Lawi Sijaona19631965Julius Nyerere
2Job Lusinde19661967
3Saidi Maswanya19671973
4Omary Muhaji19731974
5Ali Hassan Mwinyi 2.jpg Ali Hassan Mwinyi19751976
6Hassan Moyo19771978
7Salmin Juma19791980
8Abdalla Natepe19801983
9Muhidin Kimario19831989
Ali Hassan Mwinyi
10Nalaila Kiula1990
11Augustino Mrema19901994
12Ernest Nyanda1995
13Ali Ameir Mohamed19951999Benjamin Mkapa
14Muhammed Seif Khatib20002002
15Omar Mapuri200321 December 2005
16John Chiligati6 January 200616 October 2006Jakaya Kikwete
17Joseph Mungai16 October 200613 February 2008
18Lawrence Masha13 February 200828 November 2010
19Shamsi Nahodha28 November 20107 May 2012
20Emmanuel Nchimbi7 May 201220 December 2013
21Mathias Chikawe.jpg Mathias Chikawe20 January 20145 November 2015
22Charles Kitwanga.jpg Charles Kitwanga14 December 20152016John Magufuli
23Mwigulu Nchemba.jpg Mwigulu Nchemba20161 July 2018John Magufuli
24Hon Kangi Lugola.jpg Alphaxard Kangi Ndege Lugola1 July 201823 January 2020John Magufuli
25George Simbachawene23 January 2020[2]9 January 2022John Magufuli
Samia Suluhu
26Hamad Masauni10 January 2022incumbentSamia Suluhu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom