JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Mabadiliko madogo ya mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, jana Machi 31, 2022 yamemuweka Waziri Pindi Chana kwenye wizara yenye “moto”.
Wizara hiyo yenye historia ya “kuwakaanga” mawaziri kwa kashfa na wengine kushindwa hata kumaliza mwaka mmoja si nyingine ni ya Maliasili na Utalii.
Pindi ambaye alikuwa balozi wa Tanzania nchini Kenya amekwenda kushika kijiti kilichoachwa na Damas Ndumbaro.
Historia inaonesha kuwa mawaziri wengi walioshika nafasi ya uwaziri kwenye wizara hiyo wengi hawakuvuka kigingi cha miaka mitatu isipokuwa Zakhia Meghji aliyeupiga mwingi kwa miaka takriban minane.
Lakini Ndumbaro, Hamis Kigwangalla, Lazaro Nyalandu, Khamis Kagasheki hawakuweza kufurukuta katika wizara hiyo na kujikuta waking’olewa.
Wengine ni Ezekiel Maige (2010-2012), Shamsa Mwangunga (2008-2010), Jumanne Maghembe (2007-2008), Anthony Diallo (2005-2006), Zakhia Meghji(1997-2005), Juma Ngasongwa (1995-1996), Juma Omar (1993-1995), Abubakar Mgumia (1990-1993) na Marcel Komanya (1989-1990).
Arcardo Ntagazwa (1987-1989), Getruda Mongela (1985-1987), Paul Bomani (1984-1985), Geogre Kahama (1983-1984), Ali Hassan Mwinyi (1982-1983), Isaack Sepetu (1980-1982).
Wengine ni Solomon Saibul (1975-1980), Hosnu Makame (1970-1975), Dereck Bryceson (1965-1970) na Tewa S. Tewa (1962-1965).
Inaonekana kwa mbali mawaziri wa zamani walimudu lakini hawa wa sasa hawajaonesha maajabu, wewe unafikiri tatizo ni nini hebu mpe ushauri waziri mpya Pindi Chana anatokaje kwenye mtego huu?
Chanzo: Global Publishers