Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi yapiga marufuku wafanyakazi 'kuchat' ofisini

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,939
9,959
Nineona kwenye gazeti Waziri Prof. Mbarawa akiwapiga marufuku wafanyakazi wa wizara yake kuchat ofisini saa za kazi.

Hapa namuunga mkono Waziri huyo kwani kuna wakati unaweza kwenda ofisi ya serikali ukakuta mtu anachat na ukimuongelesha wala hakusikii yeye yupo busy kuchat tu. Hii iwe kwa ofisi zote za umma.

Ngoja siku nipite pale ferry nikute wanachat, fasta namtumia waziri wao taarifa ili awatumbue.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ''Kuchati'' katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.

Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.

Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.

Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.
 
Viongozi wa kitanzania wanafurahisha sana! Na kwa huyo Profesa ndiyo kichekesho zaidi. Yaani badala ya kuliangalia hilo suala kwa upana zaidi, yeye kaliangalia kwa uwezo wa macho yake kuona.

Tatizo la utendaji maofisini (haswa kwenye ofisi za serikali) moja ya dawa yake ni kuwa na performance based contracts. Ukiweka indicators na milestones ambazo mfanyakazi kwenye ofisi ya serikali anapaswa kuzitimiza (na kama mazingira ya kazi yapo sawa na serikali kama mwajiri inawajibika ipaswavyo), hakika hutakuta mfanyakazi huyo akichat wakati wa kazi. Bila ya hivyo, hizi zimamoto hazitofanikiwa kamwe.

Walazimishe wafanyakazi kufanya kazi kweli kupitia mikataba yao, na pale wasipofikia malengo, mkataba uwe wazi kuwa kufukuzwa ndiyo mwisho wake.
 
Nineona kwenye gazeti Waziri Prof. Mbarawa akiwapiga marufuku wafanyakazi wa wizara yake kuchat ofisini saa za kazi.

Hapa namuunga mkono Waziri huyo kwani kuna wakati unaweza kwenda ofisi ya serikali ukakuta mtu anachat na ukimuongelesha wala hakusikii yeye yupo busy kuchat tu. Hii iwe kwa ofisi zote za umma.

Ngoja siku nipite pale ferry nikute wanachat, fasta namtumia waziri wao taarifa ili awatumbue.

Come on Prof. ! ! !

Sasa hilo linahitaji tamko la Waziri kweli? Au ndio yaleyale ya kutumia nguvu nyingi pasipo sababu na mwishowe unaishia kudharauliwa

Kwani Katibu Mkuu wa Wizara Hajaweka Working Policy ya Wizara?

Sasa haya matamko ya waziri kama huyu yanapimwaje utekelezaji wake?

Mtu anaibuka tu ili aonekane mtumbua majipu anaanza kusema sijui "Marufuku ...."

Hebu Waziri ashughulike na Maswala ya Kisera amwachie Katibu Mkuu maswala ya kiutendaji maana huku ni kama kujidhalilisha na kudhalilishana tu tena matumizi mabaya ya raslimali watu.
 
Ukiweka indicators na milestones ambazo mfanyakazi kwenye ofisi ya serikali anapaswa kuzitimiza (na kama mazingira ya kazi yapo sawa na serikali kama mwajiri inawajibika ipaswavyo), hakika hutakuta mfanyakazi huyo akichat wakati wa kazi. Bila ya hivyo, hizi zimamoto hazitofanikiwa kamwe.
....Na unapompa mtu ajira ya kudumu(permanent and pensionable) madhara yake ndio hayo
 
Walazimishe wafanyakazi kufanya kazi kweli kupitia mikataba yao, na pale wasipofikia malengo, mkataba uwe wazi kuwa kufukuzwa ndiyo mwisho wake.
Nadhani huyu Waziri ni muumini wa Performance Contracts. Kuna siku nilimsikia kwenye TV akisema ataingia mikataba na Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Idara chini ya Wizara yake wataingia mikataba na Makatibu Wakuu.
 
Come on Prof. ! ! !

Sasa hilo linahitaji tamko la Waziri kweli? Au ndio yaleyale ya kutumia nguvu nyingi pasipo sababu na mwishowe unaishia kudharauliwa

Kwani Katibu Mkuu wa Wizara Hajaweka Working Policy ya Wizara?

Sasa haya matamko ya waziri kama huyu yanapimwaje utekelezaji wake?

Mtu anaibuka tu ili aonekane mtumbua majipu anaanza kusema sijui "Marufuku ...."

Hebu Waziri ashughulike na Maswala ya Kisera amwachie Katibu Mkuu maswala ya kiutendaji maana huku ni kama kujidhalilisha na kudhalilishana tu tena matumizi mabaya ya raslimali watu.
working policy ndio kitu gani mkuu? au ulitaka kusema company policy?
 
Mkuu Nguruvi3 huwa anazungumzia sana suala la mfumo.

Hapa najaribu kufikiria hicho ulichokieleza kina-fit kivipi na suala la mfumo bora!
Mkuu hapa sikjakuelewa maana aliyeandika bandiko ni Nzi

Je, ulikusudia kusema alichokieleza Nzi kina fit vipi na hoja yangu ya mfumo au ulikusudia kutaka maoni kuhusiana na alichoandika Nzi?
 
Sisi huku ofisini, tumekubaliana whatsapp iwe locally official communication tool baada ya kujiridhisha kuwa kila mmoja ana smartphone. Sasa aje mlugaluga kupata huduma halafu aanze kulalamika eti ninachat muda wa kazi
 
Tutachati tuu maana hamna jinsi kama shuleni walitukataza lakini bado tukawa na simu sembuse kazini ,,,,,
Angeangali njia mbadala na siyo ishu za simu
 
Mkuu hapa sikjakuelewa maana aliyeandika bandiko ni Nzi

Je, ulikusudia kusema alichokieleza Nzi kina fit vipi na hoja yangu ya mfumo au ulikusudia kutaka maoni kuhusiana na alichoandika Nzi?

Nilichokuwa nataka kusema ni kwamba, alichoandika Nzi kina fit vizuri sana na hoja yako ya mfumo na ndo maana nikakutaja.

Na hilo swali lilikuwa rhetorical tu.
 
Nilichokuwa nataka kusema ni kwamba, alichoandika Nzi kina fit vizuri sana na hoja yako ya mfumo na ndo maana nikakutaja.

Na hilo swali lilikuwa rhetorical tu.
Nimeelewa, ahsante

Alichokieleza Nzi kina mantiki. Nadhani hapo US unajua Silicon Valley wana Gym ndani,
Siku hizi si ni kila corporate ina Gym na watu wanakwenda kwa wakati wao.

Unafahamu watu wanafanya kazi wakiwa majumbani kama wapo ofisini

Ninaposikia waziri akiongelea ku chat nashangaa kidogo.

Waziri anatakiwa aangalie nchi kwa maana wizara nzima si wafanyakazi wa wizara.

Kazi ya kuangalia wafanyakazi ni ya leads, Head and supervisors

Muhimu si uwepo wa mtu ofisini, ni results. Nadhani unatambua hapo kazini kwako au ulipowahi kufanya kazi, supervisor wako ndiye kila kitu.

Kuna sehemu hukutani na CEO au Director pengine kwa miaka.

Hilo ni kutokana na ukweli kuwa mfumo mzima umetengeneza kuhakikisha kila mtu anakuwa responsible na ana deliver

Nzi kaeleza vizuri, milestones na indicators utapata results nzuri tu.

Ukiwa na contracts itakuhakikishia uwajibikaji, contract inamweleza mwajiriwa hatma yake.

Kwa vile wenzetu wana mifumo mizuri, wana Gym makazini hawahangaiki na chat, wao wanasoma namba tu na jinsi mtu anavyo perform au ku-deliver

Na Kwavile mfumo wetu ni wa hovyo, waziri anayetakiwa kuangalia miradi kama ya ujenzi wa bomba la mafuta , bomba la gesi, kufufua reli, kufufua sekta ya anga n.k. anafanya kazi za supervisor kuangalia nani ana chat. Hivi hapa si tatizo la mfumo kweli!!

Kazi ya katibu mkuu ni pamoja na kuangalia utendaji mzima wizarani. Ni kuhakikisha anapata matokeo kulingana na malengo.

Kazi za waziri ni kuangalia shughuli za wizara kwa akiunganisha kazi za vitengo

Waziri akiangalia wanao chat, K/mkuu/mkurugenzi au mkuu wana kazi gani?

Hapa tuna maana moja, kinachohitajika ni mfumo unaombana mtu awe responsible
 
Ndio safi
NA ikibidi ajira ziwe hivi
Unalipwa kwa kufanya kazi sio kuajiriwa
 
wanachart mbona! harafu wanacomment hapa
Wengine hakuna kazi za kufanya yangu asubuhi to 9:30 daily. Mabosi kwenye roho mbaya wanawapa watumishi madeski yasiyoendana na kisomo chao. Computer moja meza moja watumishi 6. Yale Yale ya Nida. Naona Redundancy irudi. Kuna watu wanalipwa Mishahara ya Bure serikalini
 
Ehee hapa umeleta hoja nzuri.
Hivi wale 600 wa NIDA waliajiriwaje ikiwa mfumo mzima wa ajira ulikuwa unafanya kazi?

Hivi nani alipima utendaji wao kiasi cha kutoweza kuona nani anafanya nini?

Yote hayo yanakuja katika suala moja, mfumo mzima mbovu ndio maana hauwezi kubaini uozo

Ukimsikiliza mkurugenzi wa NIDA ameeleza vizuri sana kwa namba kuhusu input na output
Nadhani anachokitaka ni kuhakikisha kila mmoja ana shea ya kazi kulingana na ujira

Ukishatoa shea watu wakawa responsible hayo mengine yanajisimamia

Ukiwa na mfumo ulioajiri watu 600 bila kujua wanafanya nini, unawezaje kulaumu chat ?
 
Mkuu Nzi na Nguruvi3 mmenikumbusha ya google. Sijawahi ona working evironment iliyo free kama ya google.

Lakini hakuna kinachofeli.

Mfanyakazi mmoja wa google alisema, "...kila mmoja anajua wajibu wake, na kitu kifanyike kwa wakati gani. Hakuna wa kukufuata."

Nawazaga tu...tungekuwaga na freedom ya kufanya kazi kama ile sijui kama wabongo tungeiweza ama tungei abuse.
 
Back
Top Bottom