Wizara ya Sanaa na Michezo iboreshe "customer care" kwa "world class celebrities" wanaoitangaza vyema Tanzania yetu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania?

Hivi kwanini unakuta "a world class celebrity" anakuja kutembelea Tanzania na kuitangaza vema kisha hakuna hata afisa muandamizi kutoka serikalini/wizara husika ya sanaa na michezo ambaye anafunga safari ya kumtembelea ili kutambua tu uwepo wake?

2118360_IMG_20190722_174823_201.jpg

Kama tumeweza kuitangaza vema nchi mpaka celebrity akaweza kufahamu vivutio tulivyonavyo akaja Tanzania, kwanini kwenye kuonesha "courtesy" ndogo kama hii tusiboreshe?

2118348_IMG_20190722_184848_664.jpg

Mimi ninamshukuru sana mzee Dr. Mahiga alifanya vema sana kwa upande wake kwenye ku-handle top foreign diplomats waliokuwa wanazuru nchi yetu. Tazama picha hapo chini.

Tazama picha hapo Chini Dr. Mahiga akiwa na Rais wa Switzerland aliyekuja Tanzania kwa ziara binafsi ya utalii.

IMG_20190722_184817_748.jpg

Hawa celebrities tukiwatumia vizuri wanaweza kutupa ushauri wa mambo mawili matatu ya namna gani tunaweza kuboresha tasnia zetu za sanaa na mchezo, ila technical staff wa TFF/BMT na BASATA wamelala tu.

Mimi yangu macho tu. Jioni njema.

Kwa kumalizia tu nasema, NSSF nipeni fao langu, mtaani maisha magumu sana.

OUR MOTTO
==========
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. JIULIZE UMEIFANYIA NINI LA MAANA NCHI YAKO MPAKA SASA???
 
World Class Celebrities should be handled accordingly
Nimesema hivi: Siyo kila anayekuja anataka uwepo wake ujulikane. Watu maarufu hutalii sehemu mbali mbali duniani na mara nyingine hufanya ziara za binafsi. Nikukutajia watu maarufu ambao wametalii Kenya mwaka jana bila watu kutangaziwa utashangaa. Pia Tanzania huwa wanatalii lakini mara nyingi hawataki watangazwe. Unacho-suggest wewe kitaleta matokeo kinyume.
 
Kwanini unang'ang'ania tu hao ambao hawataki kutangazwa? Vp wale ambao wanataka kutangazwa na wana-post mpaka kwenye social media accounts zao?
 
Kwanini unang'ang'ania tu hao ambao hawataki kutangazwa? Vp wale ambao wanataka kutangazwa na wana-post mpaka kwenye social media accounts zao?
Kwanza badala ya kubishana jieleze vizuri. Ukizungumzia ''customer care'' una maana ya huduma wanazopata. eg hotel nzuri na huduma bora. Kutembelewa na viongozi siyo big deal na usifikiri kila mtu anapenda kuonana na viongozi kama unavyofikiri. Anyways, ngoja niachane na wewe kwa sababu naona upeo wako kwenye haya mambo siyo mzuri.
 
Wote mpo sawa mkuu sema mnaongea katika angle tofauti. Unachokisema ni kweli maana kwa Tanzania ,utalii wetu haujaegemea kwa idadi ya watu bali quality yao na ndio maana unaweza kuona kuwa tunapokea wageni wachache lakini mapato ni makubwa. Kingine ni kweli pia Tz ni moja Kati ya tourism spot ambazo zinatembelewa na watu wakubwa duniani hasa wale wanaohitaji privacy hivyo, kufanya kinyume na unayoyasema ni sawa na kuwafukuza.

Jamaa yupo sawa kwa maana watu wakubwa wanabidi wapewe special care ili watutangaze yaani hata Kama Sio kwa social media bhasi iwe hata kwa word of mouth ambayo ni more effective kutokana na nature ya wateja ambao tunawataka.
 
Wizara ya Sanaa na Michezo inaweza kuwashawishi celebrities kutumia tarehe28 ya kila mwezi kutangaza vivutio vya nchi kupitia social media platforms
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Wizara ya Sanaa na Michezo inaweza kuwashawishi kwa ustaarabu celebrities wetu kutumia tarehe 28ya kila mwezi kutangaza vivutio vya nchi kupitia social.. Search results for query: Wizara kutumia celebrities tarehe 28 kila mwezi
Wao wizara kutangaza na kukuza utalii kimataifa wanafikiria kutumia ma Celebrity wa Ki-Bongo (ki-Kitaa), hawajiongezi kuwa karibu na watu wenye ushawishi duniani kote kwa kutumia lugha kubwa za kimataifa kiingereza/ kifaransa/spaniola/Mandarin, mapokezi , reviews etc
 
Wizara ya Sanaa na Michezo inaweza kuwashawishi celebrities kutumia tarehe28 ya kila mwezi kutangaza vivutio vya nchi kupitia social media platforms
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Wizara ya Sanaa na Michezo inaweza kuwashawishi kwa ustaarabu celebrities wetu kutumia tarehe 28ya kila mwezi kutangaza vivutio vya nchi kupitia social.. Search results for query: Wizara kutumia celebrities tarehe 28 kila mwezi
Upo sahihi sana kaka mkubwa. Ila una kumbukumbu sana aisee. Hii post ni yangu ya zamani sana....
 
The Pan African Conference on: Human - Nature Conflicts
Opening Remarks by Hon Dr. Hamisi Kigwangalla, the Tanzanian Minister for Tourism.

Source : maliasili na utalii online Tanzania
Angalau Dr. Hamisi Kigwangalla uzalendo aliuweka pembeni na kutumia fursa ya kongamano hili kuinadi Tanzania moja kwa moja kwa kutumia lugha kubwa ya kimataifa. Wengine waige amuzi hili ktk makongamano yote ya kimataifa iwe ndani ya nchi au nje.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom