Wizara ya Nishati, tunaomba TPDC waajiri watu waliosoma fani za mafuta kwa usawa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,281
8,196
Kwako Wizara ya Nishati,

Rejea Tangazo la ajira za shirika letu la mafuta, TPDC. AJIRA MPYA -

Shirika limetoa ajira nyingi za kutosha lakini kuna baadhi ya fani za mafuta hazijatajwa kwenye Tangazo hilo ilihali watu wa fani hizo wanaweza fanya kazi hizo.

Tunazo fani nyingi za mafuta na gesi Tanzania kama ifuatavyo.

Oil and gas accounting,
Oil and Gas Law,
Petroleum Engineering,
Petroleum Geology,
Petroleum Chemistry,
Oil and Gas Engineering,

Tulitegemea fani hizi zote zionekane kwenye Tangazo. Watu washindane kwenye usaili tu. Ujuzi na maarifa yapimwe huko.

Fani hizi zote zilianzishwa na serikali ili kuinua uchumi wa mafuta na gesi katika taifa letu. Tunaomba zinapotokea nafasi za kazi fani zote za mafuta na gesi zihusishwe kwenye mchakato wa ajira.

Huu sasa ndio muda wa kuwatumia vijana wetu kwenye sekta ya mafuta na gesi.

Ahsante.
 
Connection haiihitaji specific academic proffesion. Ni kuwa na connection tu ndo kikubwa.

hata kama nina bachelor in arts naweza nkapiga kazi TPDC , ni connection tu
Hapana connection kazi zote zinapitia utumishi. Mtihani unafanyika anayefaulu ndio anachukuliwa
 
Back
Top Bottom