Wizara ya nishati na madini yatuliza hofu za wawekezaji

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wizara ya Nishati na madini imekanusha kuwa itatwaa leseni za Muwekezaji wa Dutwa na na yule wa Accacia kama ilivyoagizwa na rais Magufuli.

Wizara imesema haitakuwa na haraka KUWANYANG'ANYA lesseni wawekezaji hao na hivyo KUTULIZA hofu iliyokuwa imetanda na minong.ono ya hapa na pale.

Kamishina wa Madini Ally Masaje amesema watakutana na wawekezaji hao ili waone NJIA MBADALA ili kila mmoja afaidike pasipo KUUMIZA upande wowote.
Alisema sheria za madini ni lazima zitazingatiwa.
 
a.

Halafu unategemea hawa watu wazalishe? Hivi kwa nini suala la uwekezaji linaonekana jepesi kama kucheza ngoma za wakati wamavuno? Mtu kaasikia mkuu wa nchi ametamka kwamba lesseni zao zimefutwa. Kuna mwingine mwenye uwezo wa kuwa na kauli juu ya hiyo? Halafu kwa kuwafanya kama wagonjwa wa ukimwi kwamba wanafairjiwa "kula vizuri" utaishi tu, wanaambiwa maneno hayo kwama "Hatutakuwa na haraka ya kukunyan'ganya lesseni", !. Hii ni sawa na mtu anayesubiri utelezaji wa hukumu ya kifo. Anaweza kufanya jambo lenye tija kwa kesho yake?

Naomba tuwe serious jamani.

MKUU KESHAWAFUTIA LESSENI, WADOGO TEKELEZENI. ACHENI KUWAPOTEZEA WATU MUDA KWA KUWAHADAA HUKU MKIJUA HAMNA UBAVU WA KUBADILI LOLOTE.

FUTEN LESSENI, LIPENI FIDIA, AU WAENDE MAHAKAMANI, MKASHINDANE KWA SHERIA HUKU MKITOA PICHA HALISI KWA WAWEKEZAJI WENGINE
 
Wizara ya Nishati na madini imekanusha kuwa itatwaa leseni za Muwekezaji wa Dutwa na na yule wa Accacia kama ilivyoagizwa na rais Magufuli.

Wizara imesema haitakuwa na haraka KUWANYANG'ANYA lesseni wawekezaji hao na hivyo KUTULIZA hofu iliyokuwa imetanda na minong.ono ya hapa na pale.

Kamishina wa Madini Ally Masaje amesema watakutana na wawekezaji hao ili waone NJIA MBADALA ili kila mmoja afaidike pasipo KUUMIZA upande wowote.
Alisema sheria za madini ni lazima zitazingatiwa.
Hawa hawamjui Rais wangu hawa. Amri ilishatolewa wanyang'anywe leseni pawekwe maji hiyo ni amri halali bhanaa
 
Ila huyo kamishina ni ngunguri kwelikweli.
Ananikumbusha waziri(mteule) mpya wa ulinzi wa marekani,
Trump anasema tutafanya kazi na Russia kuleta amani kule syria,yeye anasema Russia ni adui yetu namba moja
 
Inaonekana kuna mvurugano mkubwa serikali ni,huyu anaagiza hiki,yule anapinga,
 
Nahisi ngumi zitakuja kupigwa maofisini,kama agizo linatoka ofisi kuu,inapingwa na afisa tu
 
Ila huyo kamishina ni ngunguri kwelikweli.
Ananikumbusha waziri(mteule) mpya wa ulinzi wa marekani,
Trump anasema tutafanya kazi na Russia kuleta amani kule syria,yeye anasema Russia ni adui yetu namba moja

Jamaa anaitwa Mad dog Mattis...nasikia hajawai kuwa na demu waka kuoa...yeye muda wote anawaza vita tu halafu anaipenda nchi yake kuliko....linapokuja suala la maslahi ya marekani humwambii kitu.
 
Back
Top Bottom