Wizara ya Nishati na madini toeni ufafanuzi; kwanini soko la shaba (copper) limepaa maradufu?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,394
Kuna malalamiko mengi sana juu ya soko la shapa kupaa!

Gharama ya mauzo na manunuzi ya shaba (copper) imepaa sana kwa zaidi ya 45%-55% ya bei ya awali je tatizo ni nini?

Nani anafahamu kwa nini soko la madini hayo limepaa sana?

Shida iko wapi? Wenye majibu tafadhali
 
Bei ya shaba inategemea na soko la London Metal Exchange (LME). Huenda Demand ya Copper imekuwa kubwa au Supply imekuwa ndogo. Au gharama za uchimbaji zimekuwa juu.
Mamlaka watusaidie kutoa ufafanuz
 
Mamlaka watusaidie kutoa ufafanuz
Hakuna anayeweza kukusaidia katika hili. Hata kama shaba inaokotwa jalalani, lazima iuzwe kwa bei (FOB prices) zilizoainishwa na soko la Ubadilishanaji metali la London. Serikali haipangi bei ya shaba, hata Serikali ya Zambia ambako Shaba inachimbwa, haina say juu ya bei ya shaba. Say wanayo mabeberu.
Screenshot_20210625-193700.jpg
 
Hakuna anayeweza kukusaidia katika hili. Hata kama shaba inaokotwa jalalani, lazima iuzwe kwa bei zilizoainishwa na soko la Ubadilishanaji metali la London. Serikali haipangi bei ya shaba, hata Serikali ya Zambia ambako Shaba inachimbwa, haina say juu ya bei ya shaba. Say wanayo mabeberu.
Oooh hivyo!?
 
Kuna malalamiko mengi sana juu ya soko la shapa kupaa!

Gharama ya mauzo na manunuzi ya shaba (copper) imepaa sana kwa zaidi ya 45%-55% ya bei ya awali je tatizo ni nini?

Nani anafahamu kwa nini soko la madini hayo limepaa sana?

Shida iko wapi? Wenye majibu tafadhali
yaani bei kupaa ndiyo tatizo au fursa?
 
Nahitaji kununua Madini ya Shaba kuanzia Tani1 kwenda mbele. Mwenye kujua wapi inapatikana kwa wingi. Tafadhali naomba majibu
 
Back
Top Bottom