May 26, 2019
Taarifa kwa Umma Hotuba itakayosomwa na kambi ya Upinzani Wizara ya Nishati
Hotuba ya Mh. John Mnyika waziri kivuli wizara ya Nishati bajeti 2019 / 2020 ikitangulia ile ya serikali ambayo wizara itaisoma May 28, 2019.
Ndani ya wizara ya Nishati kuna sekta muhimu tatu za Umeme, Gesi na Mafuta . Mh. John Mnyika mbunge wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, Tanzania kupitia CHADEMA akiwa waziri kivuli anasimamia wizara hiyo muhimu kabisa inayosimamia mradi wa bwawa la umeme wa Stiegler's Gorge , Gesi ya Mtwara na utafutaji Mafuta ya petroliamu
Source : Kwanza TV
Rasimu ya hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu bajeti ya wizara ya Nishati anayoifafanua kwa umma wa waTanzania kupitia waandishi wa habari ina kurasa 80.
Hotuba ya kambi ya upinzani ktk kuiangazia Stiegler's Gorge ripoti za upembuzi yakinifu zilizopo serikalini zinaonesha mradi huo utachukua miaka 9 mpaka 12 kumalizika wakati awamu hii ya tano inadai itachukua miezi 36 yaani miaka 3 tu kukamilisha ujenzi kunako mwaka 2022. Kambi ya upinzani inataka watanzania waelezwe ni miujiza gani itatumika kukamilisha mradi huo ndani ya miaka 3 na wala siyo miaka 9 mpaka 12.
Maana gharama mtambuka za kweli ikiwa mradi utachukua miaka 9 hadi 12 kumalizika basi bajeti ya mradi huo mkubwa wa nguvu za umeme wa bwawa la maji unaweza kuitia matatani nchi kifedha.
Serikali kukosa fedha toka wadau wa maendeleo kutokana na mradi wa umeme wa bonde la Rufiji kutishia kuharibu ekolojia na mbuga kubwa ya wanyama ya Selous.
Mh. John Mnyika anamnukuu waziri wa serikali ya CCM kuwa Mradi wa umeme wa Rufiji (Stiegler's Gorge) tayari umepewa mabilioni ya shillingi.....
Kambi ya upinzani inataka serikali itoe maelezo kwanini mradi wa gesi umetoswa wakati uligharamiwa kwa dolari za kimarekani bilioni 2 kupitia mkopo kujenga bomba la gesi linalotumika kwa kiwango cha uwezo wa asilimia 6 tu ya uwezo wake wa kusafirisha gesi toka Mtwara hadi Dsm.