Wizara ya Nishati apewe Waziri anayeaminika na watu wengi ili hata akisema lipo tatizo aaminike

Januari hafai hata kuwa katibu kata....huyu dogo pale alipomsengenya JPM ambapo yeye na wenzake walidukuliwa alionyesha wazi kuwa yeye ni msaliti...tukio Lile ni sawa na uhaini...
 
Kuna kikundi maalum cha kuwachafua baadhi ya Mawaziri.
Mawaziri wanao lengwa kuchafuliwa na kufanyiwa figisu ni;
1. January Makamba.
2. Mwigulu Nchemba

kila kukicha ohh....Makamba........ohhhh Mwigulu.

Hao Mawaziri wanafaaa sana ktk Wizara hizo na kwa uwezo wa Mungu wataendelea kuhudumu ktk wizara hizo hadi 2030.
 
anuary si Waziri asiyeaminiwa na wengi hata michango ya watu iwe mitaani ama humu mitandaoni ukweli huo unajidhihirisha.
Huu ni ukweli kwa 100% january hajawahi kuaminika na hawezi kuaminika. Chunguzeni mienendo yake alipokuwa Mazingira namna alivyokuwa akihujumu juhudi mbalimbali za serikali ktk kutokomeza mifuko ya plastics
 
January si Waziri asiyeaminiwa na wengi hata michango ya watu iwe mitaani ama humu mitandaoni ukweli huo unajidhihirisha.

Sasa ili kuwe na kuaminika tena kwa matatizo yahusuyo Nishati nikuombe Rais Samia teua Waziri mwenye japo chembe ya kuaminika na wengi wetu awe Waziri wa Wizara hiyo.

Bado wapo watu katika baraza lako wenye ushawishi kwa wananchi mfano mzee Lukuvi ni mmoja ya Waziri mwenye kauli inayopokelewa na wengi na ni mtu anayeaminika na watu japokuwa naye ni mwanadamu na mapungufu yake.

Kumpa January nishati ni kumchonganisha na watu tu hali itakayomfanya awe na stress zaidi.

Nashauri,January atafutiwe Wizara nyepesi kwa sababu hata yeye ni mwepesi.

Acha Bla bla wananchi wanataka maji na umeme - Wilson Mahera
 
Sidhani kama kuna mtu anayeaminika ndani ya CCM. Ndani ya CCM wamejaa watu wanafiki, waongo, wadanganyifu, wevi na uchafu wa kila namna.

Leo hii, ndani ya CCM, kuanzia Rais, mawaziri, wabunge, madiwani mpaka wenyeviti wa Serikali za mitaa, yupo hata mmoja anayeweza kusema alichaguliwa na wananchi kwa mchakato safi, wa wazi na wa haki kabisa?

January na Nape, ndio waliwekwa kuwa viongozi kwaajili ya kuiba kura kumpa Magufuli 2015, Kalemani hakuchaguliwa na wananchi bali na marehemu, sawa na walivyo wote wanaoitwa wabunge wa bunge hili la sasa.

Sasa, unataka kuniambia huwa kuna mwizi anayeaminika?

Tunaongozwa na chama na viongozi wanaoamini katika wizi, unafiki na uwongo. Je, utakwepa vipi uchafu wa kila aina nchini? Vyovyote utakavyofanya, utakuwa unatafuta unafuu katika uchafu, lakini huwezi kupata kilicho safi.
Dawa ni moja tu,kukata mapembe.
Rais na heshima hiyo tu.
Mwenyekiti wa Chama awe nitofauti na Rais.
Mashariti haya yazingatiwe.
1.Mwenyekiti awe mjumbe mwalikwa kwenye vikao vya chama.
2.Kama alishatumikia nafasi ya urais hataruhusiwa kugombea uenyekiti wa chama.
3.Nafasi ya Katibu Mkuu isailiwe miongoni mwa wanachama.
4.Katibu mwenezi na utandawazi iteuliwe na Katibu mkuu.
5.Miaka 5 watia nia ya urais wapeleke majina na siyo jina moja lichukue fomu.
6.Rais ahojiwe na chama pale inapotokea kama ya sabaya.
7.Iwe marufuku vikao vya vyama kufanyikia Ikulu.
8.Waziri mkuu apendekezwe na chama rais akamuapishe tu.Pia waziri mkuu awe anahojiwa na chama Mara kwa Mara.
 
Mpeni ushauri ndugu waziri arekebishi wapi ambapo mnaona hapajakaa sawa achana na mambo ya kutenguliwa kwanza. Akikataa ushauri wenu ndipo mpige debe la utenguzi!!!
 
Hiyo combination ya picha kwenye avatar yako...inaonyesha unaweza kutufuaa. Ha ha haaaa!
Sure mkuu huwa naWaza niingie msituni niwakomboe watanzania kutoka kwenye mikono ya wanyonyaji weusi. Bora hata ya mkoloni mweupe Mana huduma muhimu zilikuwepo.
Nikifa huku nawapigania ni thawabu kubwa Sana kuliko kufia kwenye kidonda Cha ke.
Nchi yetu Ina raslimali kibao afu mpaka mchango wa ujenzi wa shule sh 2000 unasumbua wazazi
 
January si Waziri asiyeaminiwa na wengi hata michango ya watu iwe mitaani ama humu mitandaoni ukweli huo unajidhihirisha.

Sasa ili kuwe na kuaminika tena kwa matatizo yahusuyo Nishati nikuombe Rais Samia teua Waziri mwenye japo chembe ya kuaminika na wengi wetu awe Waziri wa Wizara hiyo.

Bado wapo watu katika baraza lako wenye ushawishi kwa wananchi mfano mzee Lukuvi ni mmoja ya Waziri mwenye kauli inayopokelewa na wengi na ni mtu anayeaminika na watu japokuwa naye ni mwanadamu na mapungufu yake.

Kumpa January nishati ni kumchonganisha na watu tu hali itakayomfanya awe na stress zaidi.

Nashauri,January atafutiwe Wizara nyepesi kwa sababu hata yeye ni mwepesi.
Kigogo amewekwa hapo kimkakati. Hata mpigie kelele vipi KIGOGO hatolewi.
 
Back
Top Bottom