Wizara ya miundombinu Katibu mkuu akaidi agizo la serikali

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,938
3,825
Katibu mkuu kiongozi ametoa waraka kwa makatibu wakuu wote wa wizara" KUONGEZA MUDA BODI ZA WAKURUGENZI WA MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI ZILIZOMALIZA NA ZINAZOTARAJIA KUMALIZA MUDA WAKE" ili kunusuru ubadhlifu unaoweza kutokea pale mashirika yanapokuwa bila usimamizi. Wizara ya miundombinu tofauti na wizara nyingine mpaka sasa haijatekeleza agizo hilo kwani viongozi wa wizara hiyo wakishirikiana na menejimenti za mashirika yaliyochini yake yananufaika sana kuhujumu mali wakati wa ombwe hili la usimamizi hususani shirika la ndege la Taifa ATCL ambako mali zinauzwa kiholela na wizara inafumbia macho!!
 
Shirika la ndege la ATCL limehujumiwa sana [hata na watendaji wa serikali] kiasi kwamba ni vema serikali ikasalimu amri na kulifungilia mbali badala ya kuwatia hasara wananchui kwa kutoa ruzuku kila mwezi kwa marubani na wafanyakazi wengine wanaopokea mishahara minono bila ya kufanya kazi!! Hizo fedha zingeweza kutumika kuwanunulia madawati wanafunzi wanaokalia matofali shuleni kwao!!
 
TEMESA pale wanaiba kama nini, hebu angalieni huyo jamii anaitwa Chief Excutive jamaa anatafuna hela kama nini. I watching him closely nitaleta report very soon hapa jamvini.
 
Back
Top Bottom