Wizara ya miundo mbinu wizi mtupu;katibu atetea ubadhirifu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Ubadhirifu zaidi wagundulika Miundombinu




Na Muhibu Said



26th November 2009


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni





headline_bullet.jpg
Waliotafuna bn 2.6/- za Temesa wasambaza uongo
headline_bullet.jpg
Wadai fedha zilizoliwa ni Sh. milioni 800 tu



Chambo(8).jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo.



Wizara ya Miundombinu, imekiri kuwa, kuna ufisadi wa malipo hewa uliofanywa na baadhi ya watendaji kwenye Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) wa wizara hiyo, lakini ikasema taarifa zinazosambazwa kuhusu suala hilo zinapotosha umma.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Omar Chambo, alitoa ufafanuzi huo alipozungumza na Nipashe ofisini kwake jana na kusema ripoti inayosambazwa mitaani kuhusu tuhuma hizo, ni ya bandia na kwamba, ripoti halisi inafanyiwa kazi na kuongeza kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa wote watakaobainika kuhusika na malipo hewa kwenye wakala huo.
Kauli hiyo ya Chambo, imetolewa siku chache, baada ya kusambazwa ripoti inayotaja ufisadi wa Sh. milioni 800 katika wizara hiyo, huku taarifa za awali kutoka chanzo chetu wizarani hapo zikionyesha kuwapo zaidi ya Sh. bilioni 2.6 zilizolipwa kwa madeni hewa.
Chambo alisema ripoti hiyo inayosambaa na kuonyesha ufisadi wa Sh. milioni 800 na kuchafua baadhi ya watendaji makao makuu na kuficha watuhumiwa wa ufisadi, ni ya uongo na kuongeza kuwa hata wajumbe wa tume waliotajwa hawajulikani.
“Hakuna ripoti kama hiyo, ni ya uongo kwa sababu hata majina ya watu wenyewe waliotajwa kama wajumbe wa timu hiyo hayajulikani yapo ofisi ipi,” alisema Chambo na kuongeza:
“Mimi ndiye Katibu Mkuu, ambaye nilipaswa kulipa hiyo tume kama kweli ingekuwepo, lakini sijawahi kulipa watu kama hao kwa ajili ya uchunguzi, kwa hiyo nasisitiza ni ya uongo na ripoti yangu haijatoka.”
Alipoulizwa kuhusu matokeo ya uchunguzi wa tume yake, alijibu kwa kifupi: “Bado inafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.”
Alipoulizwa kuhusu taarifa kwamba, uchunguzi huo alioagiza umeibua malipo hewa ya Sh. bilioni 2.6, alijibu: “Hadi sasa ripoti sijaipata siwezi kusema chochote, wacheni sheria ifanye kazi yake.”
Chanzo cha habari kutoka wizarani hapo, kililidokeza kuwa ripoti hiyo kiliyoiita kuwa ni ya “bandia” wakati ikisambazwa, uchunguzi halisi ulioagizwa na ofisi ya Katibu Mkuu, ulikuwa bado.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, watu walioisambaza ripoti hiyo walifanya hivyo kwa lengo la kupunguza makali ya ufisadi wenyewe, ambao unaelezwa ni mkubwa zaidi, huku wakiwashambulia na kuwahusisha baadhi ya watu, akiwamo Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme wizarani hapo, John Ndunguru, ambaye hahusiki.
Chanzo hicho cha kuaminika kilibanisha kwamba, Ndunguru ndiye alishiriki kikamilifu kufanyika uchunguzi huo wa Temesa ambayo ilipewa fedha na wizara ilipe madeni, lakini ikazembea na kushindwa na kwamba, siku zote amekuwa hataki masihara katika mambo yanayohusu rushwa.
Kilieleza kuwa Ndunguru, hakuwa akifurahishwa na utendaji mbovu, ambao wakala huo ulikuwa ukifanya kuhusu malipo ya madeni.
“Ndunguru na Chambo, si watu wa kuchezea, asikudanganye mtu. Hawa ndio wametaka kufanyika uchunguzi huo baada ya kuona Temesa kuna malalaiko,” kilisema chanzo hicho.
Kilieleza kuwa Ndunguru hana njaa ya kula fedha za umma Sh. milioni 4, kwani ni mtu mwadilifu, ambaye amefanya kazi kwenye idara hiyo kwa muda mrefu, hayuko tayari kuvumilia maovu na wala hana harufu ya ufisadi, bali baadhi ya watu tu ndio wanaotaka kumchafua kwa sababu wanazozijua wao. “Namjua Ndunguru na Chambo, wote hawana utani katika mambo ya kazi, wanaweza kuwa marafiki zako lakini ukiuka taratibu labda kwa kufanya ufisadi, ujue hawakusamehe."
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Ndunguru na Chambo tangu wote wakae katika nafasi zao wameweza kuziba mianya ya rushwa ndiyo maana baadhi ya watu wasiopata mianya hiyo wameamua kuwachafua kwa kuwapiga majungu na kuwapakazia taarifa za uongo.
“Hii taarifa wanayosema ni ya waziri ni uongo mtupu, waziri mwenyewe mpole wanamsingizia tu hawajatumwa wamekaa wakaamua kujilinda uchafu wao kwa kuchafua watu waadilifu ambao sisi tunawategemea kama nguzo ya wizara,” kiliongeza chanzo hicho.
Uchunguzi wa kina wa Nipashe umebaini kwamba taratibu za kisheria zinazoendelea sasa zinahusu uchunguzi ulioagizwa na Chambo ambao taarifa zake pia zilifika Ikulu kwa Rais Kikwete.
Imethibitika kwamba kiasi cha fedha kinachochunguzwa ni Sh. bilioni 2.6, ambazo zililipwa na wizara kwenda Temesa ili zikalipe madeni, lakini baadhi ya wajanja wa wakala huo wakalipa madeni hewa. Madeni hayo ni ya mwaka 2007/08, ambayo yalishalipwa na wizara kwenda kwa wakala wake huo, lakini yakaingia mifukoni mwa wajanja hao wakishirikiana na vigogo wa Temesa.
Uchunguzi huo umethibitisha kuwa, serikali bado ina mzigo wa kulipa deni la Sh. bilioni 2.5, ambalo wadai halisi wanadai fedha zao baada ya kulipwa malipo hewa, fedha ambazo zilihusu malipo mbalimbali, ikiwamo ya utengenezaji magari katika karakana ya MTDP iliyopo chini ya Temesa.
Wakati ripoti hiyo ya Chambo ikiendelea kufanyiwa kazi, ripoti hiyo ilimtaja Dk. Kawambwa kwamba aliunda tume Juni 8, 2009, ikiwa ni miezi minne baada ya ile ya Katibu Mkuu.
Ripoti hiyo inayotumia jina la Dk. Kawambwa, ambayo pia gazeti hili inayo nakala yake, inataja baadhi ya wajumbe kuwa ni pamoja na Elias Mtemafimbo kama Mhandisi wa Ujenzi Makao Makuu na David Liwali, kutoka Ujenzi Makao Makuu, wizara ambayo kwa sasa haipo kwani ilishavunjwa.
Inaelezwa kuwa wajanja hao, licha ya kutumia jina la waziri kuficha ufisadi huo mkubwa, pia wamejaribu kujificha kwa kutaja baadhi ya watu ambao ndiyo waliosaidia kufanyika uchunguzi huo akiwemo Ndunguru.
Imeelezwa kuwa Ndunguru ndiye alishauriana na Chambo kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi huo kwa Temesa baada ya ofisi ya kuwepo taarifa za madeni licha ya wizara kulipa fedha.
Hata hivyo, wajanja hao walitumia ujanja huo kujificha na kupunguza kiasi cha fedha kilichoibwa kutoka Sh. bilioni 2.6 hadi Sh. milioni 800, huku wakitoa madai ya kughushi kwamba Ndunguru alijipatia Sh. milioni 4 kama malipo hewa.
“Tunamfahamu Ndunguru, ni mtu safi ambaye kamwe hawezi kuhusika na tuhuma za ufisadi, amekuwa akitupa ushirikiano mkubwa katika kushughulikia ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na mambo yote ya rushwa wizarani, nakuhakikishia wanamchafua tu kwa sababu ya utendajikazi wake.”




CHANZO: NIPASHE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom