Wizara ya Mifugo & Uvuvi wekeni viwango samaki wa maji baridi hasa Sato

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Inaelekea kuna rushwa nyingi au kutokufahamu wa Serikali kwenye hii Wizara ya Uvuvi. Lakini kuwa wanaofaidika sana na elimu ndogo kwa raia wa Tanzania

Watanzania wakiona samaki wa sato wananunua kwa kujiaminisha wanatoka ziwa Victoria. Tatizo kubwa ni kwamba huu sio ukweli. Samaki wengi wa sato wanatoka kwenye mabwawa ya kienyeji, ya kisasa kama yule mwekezaji wa Arusha na China. Samiaki za ziwa Victoria ni chache sana na zina gharama zaidi.

Kitu kibaya ni kwamba samaki wa mabwawa ambao wana viwango vya chini na wengine wana mercury nyingi sana sio wazuri kwa afya. Lakini samaki wengi kutoka China wanalishwa mabaki ya nguruwe ili wakuwe haraka. Maji ya mabwawa ya kienyeji hayazunguki hivyo mercury iko juu sana.

Lakini kwenye soko samaki wote wanacganganywa na watu wa serikali wametulizwa na hawa wafanyabiashara.

Imekuwa kama zile machine za ku bet serikali inajisahaulisha kama kwasababu ya rushwa tena kutoka nje ya nchi.

Ushauri wangu ni shauri familia yako kutumia samaki wa baharini tu mpaka serikali itakapoweka utaratibu mzuri. Inawezekana kabisa unakula samaki wa mabwawa au kutoka China

 
Back
Top Bottom