Wizara ya michezo na TFF impe tuzo ya heshima daraja la kwanza Salim Bakhresa kwa mchango wake mkubwa kwenye michezo

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,352
9,810
Greetings Wana JF!

Kwa kila mpenda michezo nchini Tanzania atakubaliana na mimi kuwa Kampuni tanzu ya Azam (especially Azam TV) inayomilikiwa na Salim Bakhressa, ina mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya michezo nchini.

Tukianzia upande wa soka, Azam TV imefanikiwa kuleta mapinduzi makubwa sana ya soka, kwa kuonyesha live mpira wa miguu, imesaidia kiwango cha soka letu kupanda maradufu, kwasababu mpira sasa unachezwa kwa uwazi na zile 'janjajanja' zilizokuwepo zamani kipindi mpira unachezwa gizani hakuna tena, wachezaji wamekuwa wakijituma ili wapate kuonekana katika soko la ndani na nje ya nchi, hivyo kuongeza ubora wa ligi, pia imesaidia makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi kuu (Vodacom, NBC, KCB, GSM nk) ili yajitangaze, hivyo kusaidia kuboresha maslahi ya wachezaji na vilabu kupitia udhamini wao wa mabilioni.

Kwa kudhamini moja kwa moja ligi kuu kupitia Azam TV kwa kutoa sh Bilioni 265 kwa miaka 10 kwa timu zote zinazoshiriki ligi, imezipa unafuu ya hali ya juu vilabu kwa kuvipatia milioni 500 kwa kila club kwa mwaka, lakin pia zawadi kubwa kwa washindi wa kwanza, pili na tatu. Udhamini huu umeenda kupunguza njaa kwenye vilabu, kusaidia club katika mishahara ya wachezaji, posho, kambi nk...hii umefanya mpira sasa hivi uchezwe hasa maana kila mchezaji ana uhakika wa kulipwa na kula vizuri muda wote. Na yale mambo ya kuuza mechi kwa timu kubwa ili kupata fedha kidogo za kupoza makali hamna tena.

Azam kwa kuanzisha timu ya mpira wa miguu, imeleta changamoto mpya katika mpira wa Tanzania, kwani ule ufalme wa timu 2 za Simba na Yanga umepata changamoto mpya. Timu ya Azam imekuwa mfano wa namna gani vilabu vinatakiwa vijiendeshe kisasa.

Pia Kwa kujenga miundombinu ya viwanja vya kisasa vya kuchezea na mazoezi na football academy,amesaidia sana kukuza mpira wa nchi hii. Sasa hivi ukiangalia wachezaji wengi wanaocheza ligi kuu na madaraja ya chini, wengi wa wachezaji hao wamepitia katika academy ya Azam, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika timu za ligi na kimataifa kwa ujumla.

Azam TV pia imeshiriki kwa kiwango kikubwa sana kuinua michezo mingine kama ndondi na kick boxing kwa kudhamini mapambano mbalimbali ya kimataifa na ya ndani kwa kupitia kipindi chao maarufu Cha Vitasa. Ambapo imetoa ajira na hamasa kubwa kwa vijana wanaocheza michezo hiyo.

Hivyo, ni muda muafaka sasa serikali kupitia wizara ya michezo na TFF, kuacha 'roho mbaya' na kuutambua mchango wa Mzee Salim Bakhressa wakati bado yupo hai. Maana mchango wake katika kuinua michezo nchini hii ni mkubwa mno mno, pia amechochea ajira nyingi maelfu rasmi na zisizo rasmi kupitia udhamini wake na uwekezaji wake wa Azam TV, sasa hivi Kuna vijana maelfu nchini kote wamejiajiri kwa kupitia 'vibanda umiza' wakionyesha mpira na kupata pesa za kuendeshea familia zao.

Inabidi apewe nishani ya heshima na Rais wa nchi na kuingia kwenye rekodi kama mtu mwenye mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya michezo nchi hii wakati bado akiwa hai. Sio mpaka mtu afe ndo muanze unafiki wa kumuenzi, wakati akiwa hai mlimchukulia poa na kukaa kimya.

Nawasilisha
 
Akiboresha mazingira kwa kuweka vifaa vya kisasa kama kamera bora na ku fix zile replay mbovu pamoja na kutafuta ma broadcaster ambao wanauzoefu wa ku-operate kwenye indusrty hiyo itapendeza sana

Yaani mchizi akiamua kuwaajiri let say wazungu wawe specialized kwenye kucheza na camera au kama baadhi ya wadau walivyo suggest kwamba ikibidi atume team iende huko ligi za wenzetu ku gather experience kwa kujifunza some skills, itakuwa bomba sana

Akifanya hayo, sio tu atahitaji tuzo bali atakuwa ameongeza vionjo kwenye ligi ya bongo na kuwavutia wadau wengi nje ya nchi kufatilia na ndio fursa kwake ku supply hivyo ving'amuzi pande zote ulimwenguni.
 
Tunashukuru sana Azam kwa kuonyesha mpira zile chupri chupri za kusema sisi ni timu tunayoongoza kwa makombe ya ligi kuu hamna
 
Kiukweli AZAM aka Bakhresa ameipaisha Sana ligi yetu. Wasipompa hata udokta wa heshima basi hata mkoa mmoja waupe jina Lake.
 
Kabla ya kumwambia tajiri Bakhresa kuboresha ubora wa CAMERA zake na wataalamu ni LAZIMA kwanza TFF waboreshe ubora wa viwanja kama hatuwezi kuwa na viwanja vya nyasi halisi basi tuwe hata na viwanja vya nyasi bandia kama vile amani au gombani.

Michuano ya MAPINDUZI imeweza kutuonesha kuwa timu kutoka zanzibar zibatandaza sana mpira wa chini hili ni kutokana na kuwa wanacheza ligi yao kwenye viwanja bora kabisa vinavyowezesha wachezaji kuweka mpira chini sio kama viwanja vya bara vya kirumba, mabatini, al Hassan Mwinyi, Manungu,jamuhuri, Dodoma, Nelson mandela, sokoine n.k viwanja vinavyotumika katika ligi yetu asilimia 80 havikidhi vigezo.

Ni wito wangu kwa serikali na wadau wa michezo kuanza kuboresha viwanja hivi viwe na sehemu nzuri ya kuchezea kama ilivyo kwa viwanja vya Mkapa,uhuru na Azam complex
 
Pia Azam waache kupanga ratiba za Mechi kwa lengo la kufinya watazamaji Viwanjani ili badala yake Waangalie mpira kupitia visimbuzi vya Azam. Ratiba zizingatie furaha ya wengi kwenda Uwanjani kuangalia mechi Live na si kutukomoa sie mashabiki.
Vinginevyo azam Wameipata Ligi yetu thamani sana
 
Back
Top Bottom