Wizara ya Michezo ipige marufuku mashabiki maarufu wa Simba na Yanga kushangilia Taifa Stars

avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,750
2,000
Imeibuka tabia ya watu kujifanya wao wanaujua zidi mpira ama kwa kutoa kauli tata za kukatisha tamaa timu yetu ya Taifa, wachezaji na makocha pale kwa bahati mbaya inapokosa matokeo mazuri

Kuna watu ambao huonekana kwenye michezo ya Simba na Yanga wakiongea hovyo huku ama wamejipaka mdude gani sijui mara wamevaa mavitu ya ajabu

Watu hawa wanaibuka kwenye timu ya taifa na kuanza kutoa maneno ya kashfa kejeli na yenye kukatisha tamaa kwa benchi la ufundi na wachezaji.

Mathalani mechi ya kwanza na Benin waliwatukana sana wachezaji na benchi la ufundi kana kwamba walitaka matokeo yawe vile

Tulikuwa tunacheza na timu hevyweight yenye ma-pro waliokamilika kila idara hivyo hata kwa pale tulijitahidi sana. Ukitaka kujua uzito wa hizi timu za magharibi waulize Kenya walichokutana nacho kwa mali

Niishauri wizara, media zote za online tv ziwapuuze watu hao na walazsiwape nafsi ya kuongea maneno ytakayoharibu morari ya wachezaji. Wachezaji wetu wanacheza kufa na kupona tuache maneno ya kejeli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom