Wizara ya michezo ifungwe

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Dunia nzima iko DAEGU , KOREA sisi tuna kila jumuia lakini hatishindi kitu sasa kama hakuna pesa za kuwaandaa wawakilishi wetu huko bas bora wizara ifungwe na kama ikiwa wazi bas tusishindane for 10 years kisha ndio tujaribu tena

Haiwezekani hawa watu wanatengewa pesa kila kukicha halafu matunda hatuyaoni

I mean Botswana juzi wamepata dhahabu, kenya wanashiriki kwenye 4X4 sasa sisi we are no where to be seen

na kama sikosei chama cha Olympiki Tanzania wanajiandaa na dili la kwenda london kwenye Olympics za 2012 na we all know hawatorudi na chochote sasa ili kuepusha hizi aibu zisizokwisha kwa nini tusifocus na ndani badala ya kutaka mambo ambayo hatuyawezi?
 
Tatizo siyo wizara ila sera ya michezo ndiyo kikwazo. Nchi yetu bado haijakubali kwamba michezo ni ajira na ni hadi hapo itakapogundua ndiyo tutarajie mabadiliko.
 
Hebu fatilia bajet ya wizara ya michezo uone kama itakwamua michezo?. Sera za nch ni kikwazo ktk maendeleo ya michezo.
 
Tatizo siyo wizara ila sera ya michezo ndiyo kikwazo. Nchi yetu bado haijakubali kwamba michezo ni ajira na ni hadi hapo itakapogundua ndiyo tutarajie mabadiliko.

Mkuu nani anatunga sera? Siyo wizara kweli? Kama ni wizara basi tatizo ni la wizara.
 
Tatizo siyo wizara ila sera ya michezo ndiyo kikwazo. Nchi yetu bado haijakubali kwamba michezo ni ajira na ni hadi hapo itakapogundua ndiyo tutarajie mabadiliko.

Sawa kabisa mi nadhani ilikuwa tu ni kurekebisha na kuboresha sera zaidi Mwl.Nyerere kwa kiasi fulani katka mfumo wake esp michezo hilo alilitambua mapema sana ila wakaja hawa wakina mungai bila kuwa na sera za maboresho na hoja za kujenga hizo sera za michezo wao ndio wakaurowanya kabisa sector ya michezo, walishindwa kabisa hata kuiga mifumo ya wenzetu walio endelea wanawezaje kuboresha michezo na watu wengine wanasomaa kwahili wangelitizama leo hii Michezo ndani ya nchi hii ingekuwa ajira safi mwakumbuka hata kipindi chanyuma timu za mikoa nadhani zilikuwepo Rock City tulikuwa na Pamba,Toto, Lumumba,RTC, na hata timu za makambuni kama Bora na mabenk sasa sijui kulitokea ukilitimba gani hapo virubu vingi vikafa hata kuvifufua leo sijui kama Pamba jamani ilikuwa imejitosheleza ikafaa
 
I still stand by msimamo wangu kuwa tujipe Ban ya 10 yrs kwanza then after that ndio tufkirie kucheza nje ya nchi
 
I still stand by msimamo wangu kuwa tujipe Ban ya 10 yrs kwanza then after that ndio tufkirie kucheza nje ya nchi

Wala haiitaji ban ya miaka 10 hata tukijipa ban ya miaka 20 kama hatuujui nini cha kufanya ikiisha hiyo miaka 20 bado tutakuwa pale pale.

Nimewai kuandika thread hii kwenye jukwaa fulani . Sehemu ya nilichoandika ni
wakuu Salaaam

Nchi kama China kabla haijafikia ilipo leo makampuni makubwa ya kwanza yalichochea maendelo ilikuwa ni ya jeshi. BAE ya UK ambayo ni kampuni iliyoajiiri waingereza wengi ni kampuni ya Jeshi. Tunajua Majeshi ni one of the wing ya serikali

Nini nachotaka kusema ?
Ni kujidangaya kuwa tupata maendeleo kwa serikali kukaa pembeni eti kuwa kigezo cha biashatra huria na uchumi huria. Tunaweza tusiwe na uwezo wa kuwa na viwanda kama China au UK lakini kuna fursa ya mazingira na vijana wetu tunaweza kutumia kwa kutumia jeshi .

JWTZ, JKT au serikali wanaweza kufanya nini ?

Michezo mbali mbali ina nafasi kubwa ya kuzalisha nyota lakini tumelalala. Kwa nini
  • JWTZ au JKT Kigamboni isianzishe chuo cha kuongelea. Kuna vijana nawaona wanakimbiza na viongozi wa fery sababu wanapenda kuchezea maji. Vijana wale ujuzi wao ukitumiwa mapena wakapata wakufunzi wazuri Tanzania itakuwa mbali kimchezo.
  • JWTZ JKT Mkoni Arusha ianishe kituo cha mafunzo na mazoezi ya riadha ambapo wanafunzi wa shule mbali mbali za primary na sekondary wanaweza kuhudhuria kwa muda fulani na
  • JWTZ JKT Mwanza au Zainzibar wanaweza kushirikiana na wavuvi. Kule kun watu wanapiga kasia . Pia Kandaya ziwa Kuna watu pia wanaendesha basikeli kama kina armstrong
Hii ni mifano michache nimetoa

Michezo ni chanzo ajira nzuri inayoweza kuinua maisha ya watu hata ambao hawana elimu kubwa na vile vile kuitangaza Tanzania. Tatizo tulilonalo hakuna taasisi ya kuweza kutambua na kuwandeleza watu wenye vipaji fulani vinavyoweza kuwasaidi watu wa kawaida na kuitangaza nchi katika dunia.

Serikali isisishie tu kujenga vyuo vikuu tu nchii hii haitajengwa na wavaa tai tuuuuu. Serikali iangalie uwezekano wa kuwapa uwezo watu wa matabaka ya kati na chini na wale ambao hawakuendelea na elimu. chanzo https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/149058-jwtz-jkt-je-hii-haiwezekani.html


Ssa utaona sisi waafrika na watanzania kipimo chetu cha cha mtu mwenye mafanikio ni usomi wa shule degree . Ajira nzuri inayolipa ni siasa. Lakini form four leaver wa kenya akishinda mbio za 800 au 3000 au 10,000 pesa anayopatani income na inakatwa kodi Anatangaza hata nchi. Sasa utaona hata kila collegege inataka kuwa chuo kikuu. Yaani tumejiset na sera zetu ni mafanikio yanapatikana kwa kazi za kalamu tu

Tanzania Kuna watu wana vipaji tayari. Mi sioni hata katika leve ya africa wale wasukuma waendesha baikeli kwa nini washindwe kuwa top 3. Ni training ndogo tu. inatakiwa .Sasa Rais Jk alimpa nini yule kijana aliyemtembelea kutoka Geita hadi Dar??!!! may be alimlipia nauli ya ndege kurudi na cheque. Wakati alichotaiwa ufanya ni kumtafutia training ya mezi kadhaa ili Akapeperushe bdenera kwenye Tour za mashindao ya baiskeli mwaka huu France, Spain South africa. Hapo ndio huwa nashangaa watu wanamzunguka rais wanamshauri nini.

SO kinachotakiwa ni vipaji vya watu kuendelezwa mapema. Sio tunamjua mbulu fulani anakimbia vizuri akiwa tayari ana age 30.

Miaka ya zamani tuliweza kushinda kidogo kwenye meichezo mbali mbali na medali sababu ya vipaji lakini sayansi na teknolojia ya sasa kushinda michezo sasa unahitaji vitu viwili kipaji na tekniki.

So kinachotakiwa
  • wambulu wenye vipaji vya kukimbia waibuliwe na wajulikane mapema wapewe tekniki za kukimbia na wakufunzi wataalam
  • wasuk-uma wanojua kuendesha basikeli (kule zinaitwa daladala) wapewe tekniki ya cycling
  • Kuna watoto kigamboni wanafukuzana n askari sabu ya uogela wajengewe sehemu amabapo watakutana na walimu wa kuwapa tecnique za kuogelea kila week enn au likizo. Kuna
  • Kule ukerewe, Zanzibar, kigoma kuna watu wanapiga mbizi bila vifaa so wakipewa tekniki kidogo tu wanakuwa waogeleaji wazuri
Binafs naona Jeshi letu JWTZ. au JKT sehemu mbali mbali linaweza kuanzisha center au club za michezo( Kuogele kukimbia.. Kuendesha baiskeli, kupiga kasia etc ) . na ziwe wazi kwa raia na wanafuzi na shule na kuwe na program maluma wakufuzi amabo wanweza kuwa wajeshi kuwafudisha watu.

Kisiasa kuna watu ukiwaaambia kwa nini JWTZ kigamboni waizaizishe club ya uongela kwa jili y wanafunzi utaambiwa usalama. Ukiuliza mbona kuna sehemu JWTZ ina club za pombe na bia ziko accesible kwa raia na usalama upo wanaishidwa majibu ...... Ni mawazo kama haya ndo yametufikisha hapa....
 
I still stand by msimamo wangu kuwa tujipe Ban ya 10 yrs kwanza then after that ndio tufkirie kucheza nje ya nchi

Wazo zuri ila nitatofautiana na wazo lako la kujipa ban! Wizara ya michezo haina tofauti na wizara zingine kwa umuhimu. Nikimaanisha kuanzia ngazi ya familia hadi kitaifa, wizara hii kwa ulewa wangu mdogo ndo inatakiwa kuhamasisha watu wapende michezo kwa ajili ya afya zao. Nani asiyejua umuhimu wa michezo katika afya zetu? lakini basi, je inafanya vya kutosha tukiachilia mbali hiyo kazi ya kujali watu na afya zao, zaidi ya kujipangia pajeti na kuimalizia pale pale jengo la wizara?

Mi napendekeza waziri awajibike kwa aibu tunazozipata, siyo kisiasa ni kututia aibu kama taifa. Apewe mwingine, naye akileta mchezo tunamwajibisha mpaka atakapopatikana mwenye kuwa na vision itakayoturudishia hamasa ya kufuatilia team zetu.
 
Dunia nzima iko DAEGU , KOREA sisi tuna kila jumuia lakini hatishindi kitu sasa kama hakuna pesa za kuwaandaa wawakilishi wetu huko bas bora wizara ifungwe na kama ikiwa wazi bas tusishindane for 10 years kisha ndio tujaribu tena

Haiwezekani hawa watu wanatengewa pesa kila kukicha halafu matunda hatuyaoni

I mean Botswana juzi wamepata dhahabu, kenya wanashiriki kwenye 4X4 sasa sisi we are no where to be seen

na kama sikosei chama cha Olympiki Tanzania wanajiandaa na dili la kwenda london kwenye Olympics za 2012 na we all know hawatorudi na chochote sasa ili kuepusha hizi aibu zisizokwisha kwa nini tusifocus na ndani badala ya kutaka mambo ambayo hatuyawezi?

huu ni mtazamo wako, hata mke wako hujamshirikisha. tungemlaumu bure mama wa watu.
we unazungumzia wizara wakati maisha ya wananchi yamekuwa mbaya kupindukia, mfumuko wa bei umefikia zaidi ya asilimia mia moja! kweli mungu ana watu wengi sana wenye vichwa vya aina nyingi.
 
mtazamaji umesema kweli........tz wengi wetu tunaamini kuwa nchi hii inajengwa na wavaa tai tu...halafu unajua nini nchii kwa sasa kuna watu kibao hawafanyi kaz sasa kama nchi hatuna mipango madhubuti ya kuwasaidia hawa watu....maneno meeeeengi matendo hakuna hilo ndo tatizo....kama ulivyosema kwa sasa kila college inalilia kuwa univesity..yaani kila mtu analilia kuwa na degree utadhani nd njia pekee ya kujenga nchi............so hata tukijipa ban ya miaka 50 kwa mwendo huu hatuwezi kufka popote.............

inasikitisha sana
 
kuna makundi kibao yanaweza kuifikisha nchiii hii mbali.mbona kuna wengien wanategemea utalii na mabenki na uchumi wao uko juu..sisi tuna ila kitu lakini hakuna maendelea kazi kuomba vyandarua tu.
 
No wonder wanariadha wa nchi zingine huchukua uraia wa nje ili kukamilisha dreams zao

sisi tuko ovyo sana
 
Back
Top Bottom