Wizara ya Mazingira, NEMC, anzisheni kampeni ya kupanda miti kutumia teknolojia ya "Air Pots" kuinusuru nchi na jangwa linalotunyemelea

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Air Pots ni Vyungu (Container) maalumu vya kupandia mimea mbalimbali ambavyo huwekewa vishimo vidogovidogo kuzunguka chungu, lengo ikiwa ni kuruhusu mizizi ya mimea kuweza kutafuta mwanga na hewa.

Teknolojia hii huwezesha Mmea kukua bila kipangamizi na hata kufikia ukubwa wa kutosha kama ambavyo ungekuwa umepandwa ardhini.

Tumekuwa na kampeni za mara kwa mara za upandaji wa miti ambapo binafsi sikumbuki kma nimewhi kusikia mrejesho juu ya maendeleo ya Miti hiyo, ila wala sina shaka kudhani ya kuwa zaidi ya asilimia 90( kama sio yote) ya miti hii hufa kwa kukosa uangalizi.

Kwa kutumia teknolojia hii tunaweza kuanzisha Vitalu jirani na chanzo cha maji na ikapewa uangalizi mpaka itakapofikia ukubwa wa kutosha ndio ikabebwa na kuhamishiwa sehemu iliyokusudiwa.

Mti 3.png
Mti 2.png
 
Umefikiria gharama za kukodi fuso kubeba limti likubwa kama hilo? Mi nadhani tupande tu ardhini na tulipe gardeners wa kuiangalia kama kweli tupo serious, blvijana wengi hawana ajira, wapewe hizo ajira za kuangalia miti
 
Michongoma na miashoki haihitaji uangalizi sana na inavumilia ukame, chukua mbegu za miti hii na unaposafiri ukifika sehemu isiyo na miti ivurumishe, itaota na wanakijiji watashangaa.
 
Linapokuja suala la Mazingira hakuna gharama, maana gharama ya ukame wala huwezi kuithaminisha.

Ipandwe Miti elfu moja kwenye Kitalu itunzwe ikishaweza kujitegemea ibebwe ipelekwe sehemu zisizo na miti, zilizoharibiwa na sisi wenyewe Binaadamu.

Tukiona ni gharama sasa itafika wakati hata tukiwa na huo uwezo tutakuwa tumechelewa.
 
Umefikiria gharama za kukodi fuso kubeba limti likubwa kama hilo? Mi nadhani tupande tu ardhini na tulipe gardeners wa kuiangalia kama kweli tupo serious, blvijana wengi hawana ajira, wapewe hizo ajira za kuangalia miti
Wabkngo hawawezi na hawatoweza kamwe kupanda miti na kuitunza

Ova
 
Michongoma na miashoki haihitaji uangalizi sana na inavumilia ukame, chukua mbegu za miti hii na unaposafiri ukifika sehemu isiyo na miti ivurumishe, itaota na wanakijiji watashangaa.
Mzee sijui kama unachosema umewahi kujaribu.

Ni kweli hii Miti ina uvumilivu wa kustaajabisha, haswa hizi Bougainvellia...lakini kuanzisha sio kazi rahisi kama unavyojaribu kuelezea, hii ikishakamata ndio itakushangaza.

Kuna mahali tumepanda eneo ambalo Jamaa wa Tanesco wanadai ni kwenye eneo lao, basi huwa wanakuja wanafyeka, kuna wakati wakachoma na moto kabisa lakini wapi bado na jua lote linavyowaka ile mimea inachipua na kumea upya.
 
Nchi hii hakuna kabisa viongozi wenye vision, kama wafungwa wangetumika kupanda miti, angalau kwa kuanzia kila mfungwa kupewa target ya kupanda miti 1,000 kwa wiki ndani miaka10 nchii hii inakuwa ya green kama lilivyo kuwa eden,

lakini mi viongozi imelala tuu siyo ma creative yanajali matumbo yso tuu
 
Mzee sijui kama unachosema umewahi kujaribu.

Ni kweli hii Miti ina uvumilivu wa kustaajabisha, haswa hizi Bougainvellia...lakini kuanzisha sio kazi rahisi kama unavyojaribu kuelezea, hii ikishakamata ndio itakushangaza.

Kuna mahali tumepanda eneo ambalo Jamaa wa Tanesco wanadai ni kwenye eneo lao, basi huwa wanakuja wanafyeka, kuna wakati wakachoma na moto kabisa lakini wapi bado na jua lote linavyowaka ile mimea inachipua na kumea upya.
Unachokisema mimi nakuelewa vizuri
Miaka ya 99-2000 nakumbuka nlikuwa nashiriiki sana matukio ya kupanda miti,nlijiunganga kwenye roots&shoots
Binafsi nlipanda miti mingi tu
Sema hko wengine tuliingia kimchongo tu tulikuwa tunavizia mambo yetu
Ilinlichogundua wabongo kwenye upandaji miti,utunzaji ni zero kabisa

Mjini kwenyewe kuna sehemu nyingi miti inahitajika,wao wanataka kujenga tu sehemu kubwa

Huwa nikipita Yard ya Mbao nikakuta imejaa au Semi inapakua mzigo huwa najiuliza maswali mengi sana.

Hapo sijazungumzia Lori au Pikipiki zinazopita kila kukicha zikiwa na wastani wa Gunia tatu mpaka nne za mkaa.
 
Back
Top Bottom