Wizara ya Mambo ya Nje ina bahati wa kutoa maraisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Mambo ya Nje ina bahati wa kutoa maraisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 26, 2012.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kati ya marais wa nne wa Tanzania, wawili (BWM na JMK) wamepata kuwa waziri wa mamno ya nje. Usipo mhesau Nyerere ambae ndiyo raisi wa kwanza wa nchi unagundua kwamba maraisi wawili kati ya watatu wamesha wahi kutumikia nafasi hiyo. Kuelekea uchaguzi wa 2015 moja ya majina yanayo tajwa tajwa kutaka kumrithi JK ni Bernard Member (waziri wa sasa wa mamno ya nje) na Asha Rose Migiro (aliyepokewa wizara hiyo na Member). Swali langu ni je kuna uhusiano wowote wa kuwa waziri wa wizara hii na uraisi?

  Inaweza ikawa ni bahati mbaya tu lakini pia ina wezekana kuna sababu ndani yake.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Formula hiyo ni ya CCM..........wakiingia CHADEMA haitafanya kazi
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mataifa ya nje husaidia sana kwenye kampeni za uraisi katika mataifa masikini. Kwa kweli kugombea uraisi si kitu cha lelemama lazima uwe na fedha za kutosha. Na kwa vile mataifa hasa ya magharibu huwaweka watu ambao wao wanawajua ili kulinda maslahi yao, huwasaidia katika kampeni kwa njia ya fedha. Kwa hiyo kimsingi mawaziri wa mambo ya nje huwa jikoni
  Hii ndiyo sababu mpaka hasa ya kupata maraisi kutoka wizara ya mambo ya nje.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Inawezekana mkuu. Mimi nime notice tu hicho kitu na kuanza kujiuliza kwamba imetokea tu au kuna uhusiano wowote kati ya hiyo nafasi na kujiandaa na uraisi.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu kwa maoni yako. Ila kingine mimi nilicho kuwa nahisi ni kwamba wizara hii haideal moja na wananchi. Kwa maana ya kwamba wizara ya mambo ya nje haimaffect mwananchi wa kawaida kama vile labda wizara ya nishati au wizara ya ujenzi nk. Kwa maana hiyo mtu akiwa waziri ya mambo ya nje hadeal sana na mamno yatakayo muharibia na wapiga kura.
   
Loading...