Wizara ya Mambo ya Ndani: Atakayesema kuna njaa tutamkamata na kumwajibisha

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
WANASIASA WANOENEZA TAARIFA KUHUSU NJAA KUKAMTWA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameonya kuwa watu wakiwemo wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo za kuwepo kwa baa la njaa, ni kosa na wachukuliwe hatua ikiwemo kukamatwa.

Masauni amesema bado kuna watu wanajichukulia mamlaka ambayo sio yao na kueneza uongo kuwa kuna njaa nchini, hilo ni kosa kwa kuwa kwa kueneza propaganda hiyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

“Hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema nchi hii ….. mtu anapofanya kosa lazima achukuliwe hatua …… Jeshi la Polisi liangalieni hili,” alisisitiza.

Masauni alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana mkoani Rukwa ambako Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alimhakikishia kuwa mkoa huo hauna njaa, bali una ziada ya kutosha.

“Nyie wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa (Zelothe) amethibitisha kuwa hakuna njaa mkoani hapa lakini sio hapa tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia kuwa hawana njaa,” alisema Naibu Waziri Masauni na kuongeza: “Sasa wapo wanasiasa uchwara wanaeneza propaganda kuna njaa, sio mamlaka yao kutangaza kuwa kuna njaa, kueneza uongo kama huo ni si sawa kwa kuwa kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa,” alisisitiza.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe alimweleza Naibu Waziri Masauni kuwa hali ya kiusalama katika mkoa huo ni shwari ambapo amani na utulivu umeshamiri kwa kuwa una chakula cha kutosha.

[HASHTAG]#Habarileo[/HASHTAG].
 
Huyo waziri wa chakula juzi alikuwa anajikanganya peke mwenyewe kwa hoja za Tundu Lisu kwenye kipindi cha DW.

Eti nchi haina njaa ila ina tishio la njaa mara waziri mkuu hakusema serikali ina tani 1.5 Milion bali hizo tani ni nakisi ambayo ipo kwa wakulima .

Mara nchi ina uhaba wa chakula kwenye baadhi ya maeneo na wala sio ncho nzima kwa sababu mvua zilichelewa kunyesha mwaka jana .

Kwa kifupi ni kuwa nchini njaa ipo tusitumie nguvu nyingi kupinga uwepo wa njaa bali tutafute suluhisho kama la jirani zetu wa Kenya.
 
Kwani njaa mpaka mtu aseme si itaonekana tu, kwani kumwagiwa upupu mpaka mtu aseme nimemwagiwa upupu si ataonekana tu mtu anavyojikuna. Nyie serikali endeleeni kujidanganya is matter of time ukweli utajulikana.
Tembeleeni maduka ya rejareja muone jinsi unga unavyonunuliwa, wengine ndiyo wanaweza kununua unga na wapiga kura wenu wa vijijini wanauwezo wa kununua huo unga?
 
Ostrich.jpg
Tabia za Mbuni hizi
 
Na kweli mheshimiwa mpk wafe ukawa wote. Wakianza kufa ma sisi em tutaomba uturuki watuletee maisis maana ndo wenye chakula
 
Back
Top Bottom