Wizara ya Maliasili, Vigogo jinsi wanavyokwamisha maendeleo ya Watanzania - Part I | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Maliasili, Vigogo jinsi wanavyokwamisha maendeleo ya Watanzania - Part I

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Apr 30, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wizara ya Maliasili na Utalii ingeweza kuleta ufanisi mkubwa sana unaoweza kuwainua Raia wa Tanzania na kuleta unafuu wa maisha kwa watu wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi za wanyamapori na misitu ambao kwa sasa wanapata hasara badala ya faida. Fwatilia….


  1.Sekta-Misitu
  Tanzania ina ardhi yenye ukubwa wa 94.5 Milioni hekta, kati ya hizo 38 % sawa na 36 Milion hekta ni misitu na woodland. Misitu ipo katika makundi makuu mawili Reserved forests (12.5Milion hekta) na Unreseved forests (19 milion hekta) zilizobakia ni uoto wa woodland. Hadi mwaka 2006, deforestation rate ilikuwa ni hakta zaidi ya 130,000 hekta kwa mwaka, hii ni hatari. kwa rate hii miaka 100 ijayo misitu itakuwa ipo kwenye edge ya extinction.

  Sekta hii imeshindwa kurealize na kuprovide benefit kwa watanzania kutokana na uvunaji holela wa misitu unaosababishwa largely na upungufu wa doria pamoja na RUSHWA ILIYOKITHIRI. Wafanyabiashara wakuu wa mbao au magogo ni either viongozi au ndugu za viongozi wanaotumia vyeo vyao/vya ndugu zao kulihujumu taifa. Ndugu zangu, biashara yoyote haramu haiwezi kufanywa na mtu wa kipato cha chini/ordinary citizen na ikafanikiwa. Ukiona biashara hiyo imefanikiwa jua kuna kigogo wa Taifa hili ndiye anayeisimamia Biashara hiyo.

  Nini cha kufanya, kwanza kabisa ni kuhakikisha sera zetu za misitu zinaandaliwa in such a way that, wananchi wanaokaa maeneo yaliyojirani na misitu ndio wanakuwa wafaidika wakuu wa misitu hiyo kama vile ilivyo kwenye sera ya Madini ambapo vijiji husika vinapewa gawio. Inawezekana sasa hivi utaratibu huu umeandikwa kwenye sera zetu ila haufutwi. Kuna tafiti nyingi na takwimu za kisayansi zinazoweza kutumika kumconvince Rais kutekeleza mpango huu. Kwa kufanya hivyo naimani wananchi ndio watakuwa walinzi wakuu wa rasilimali hizi na hivyo kupunguza gharama za doria na enermity iliyopo kati ya serikali na wananchi wake.

  Imagine katika kipindi kati ya mwaka 2003-2005, Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa Tanzania ilisafirisha jumla ya cubic meter za magogo 19,300 kwenda China. Katika kipindi hicho hicho, Takwimu za China zinaonyesha kuwa Waliingiza jumla ya cubic meter 108,505 toka Tanzania. Hii maana yake ni kwamba magogo ambayo yalisafirishwa kwenda China bila kuwepo kwenye Takwimu za Tanzania ni 89,189 cubic meter. Je ni fedha kiasi gani zimepotea hapo? Takwimu hizi zinapatikana TRAFFIC-Monitor wa Illegal Trade. Fedha hiyo ingetosha kujenga madarasa 10,000. Kikubwa kinachotakiwa kudhibiti hali hii ni kusisitiza uadilifu, kudeal na maofisa wala rushwa, kuweka system yenye uwazi na kusimamia kikamilifu rasilimali hii na kuwapa fursa wanavijiji kulinda na kufaidi matunda ya ulinzi. Aidha, wananchi wapate faida za misitu sio kwa kuwajengea tu social infrastructure bali wapate economic gains.


  2. Payment for ecosystem services scheme

  Hii ni mechanism inayowapa incentive wananchi wanaoishi maeneo ambayo yanatoa ecosystem services kama vyanzo vya maji, vyanzo vya oxygen na carbon sink etc. Scheme hii imeshauriwa na wanasayansi kuwa ni nzuri katika kuwapa motisha wananchi maskin wanaoishi maeneo yanye utajiri mkubwa wa misitu na vyanzo vya maji. Kwa mfano, serikali ina-institute utaratibu huu na kuwawezesha wananchi wanaoishi maeneo yenye utajiri mkubwa wa bioanuai kama wananchi wa matombo wanaokaa chanzo cha mtu Ruvu, mto ambao unawaweka mjini wakazi wa Dar Es Salaam na vitongoji vyake. Serikali ingetoa kauli tu kuwa katika bili za maji, kama ilivyoamua kuwa EWURA wapate asilimia flani, Mimi nadhani badala ya kuwapa EWURA hiyo asilimia, Fedha hiyo ingewaendea wananchi wa Matombo na vitongoji vyake ili kuwapa motisha wasimamie kikamilifu chanzo hicho cha mto ruvu (Kimboza Forest Reserve) na kuwatoa kwenye lindi la umaskani.

  Ikumbukwe kuwa wananchi hawa wanakatazwa kulima kwenye milima uluguru kwa ajili ya kuilinda bioanuai, sasa kwanini Serikali isiwafkirie watu hawa kama ilivyowafkiria watu wa Geita na Nyamongo kwenye madini? Kama serikali ingefwata ushauri huu ambao wataalam wamekwisha uona unafaa, wananchi wangekuwa na ari ya uhifadhi na kila wilaya ingekuwa na chanzo cha mapato. Kuna ugumu gani kwa serikali kupitisha sera ya aina hii ili wananchi wafaidike? Mnafurahia nini kuona wananchi wanafedhaheka kwa dhiki kuu?

  3.Sekta-Wanyamapori

  Sekta hii inapotential kubwa sana ya kututoa hapa tulipo kwenye kuwa omba omba wa kwanza duniani hadi kuwa watoa misaada wakuu duniani. Rasilimali ya wanyamapori haiwasaidii wananchi zaidi ya kuwatia umaskini wananchi. Ni kweli ipo misaada wananchi wanapewa na TANAPA, NCAA na WD lakini misaada hii bado haijaweza kuwapa motisha ya kutosha wananchi kuwafanya waache ujangili na wasaidie uhifadhi. Sababu kubwa ya michango hiyo kuwa midogo inawezekana ni ufinyu wa budget za Mashirika hayo au ni uchezeaji wa hela zinazokusanywa na mashirika hayo.

  a) Ufinyu wa fedha zinazokusanywa

  Hili ni lakujitakia, Bei za wanyama wetu kupitia uwindaji wa kitalii ni ndogo sana. Bei hizi zimekuwa zikipandishwa kwa kuongeza kiasi kidogo sana kwa sababu ya Rushwa. Akitokea waziri anataka bei za wanyamapori wanaowindwa zipande, waziri huyo atapigwa vita na wala hatodumu kwenye wizara hii. Lakini tujiulize, je ni kwa faida ya nani bei hizi zipo chini? Wapo wawindaji wanaokubaliana na kupanda kwa bei kwa maana wanaona bei tunazowatoza ni dhuruma kwa wananchi wa Tanzania. Ila wapo wawekezaji ambao ukitangaza tu ongezeko la bei watatoa mlio kwa kigezo cha kumuumiza mzawa etc na mwisho wa siku bei hizo zitapanda kwa $5.

  Huu ni unyonyaji/uhujumu uchumi. Hivi lengo la Tanzania ni kuua wanyama wengi na kupata fedha kidogo au ni kuwinda wanyama wachache na kupata fedha nyingi?? Tutapata hasara gani kama tukangeweka bei ya juu ili waje matycoon 50 tu kwa mwaka na tukapata hela ambazo zingelipwa na wawindaji wababaishaji 500 ndio tuzipate???Are we really for the quality experience kweli kama sera zetu zinavyotabanaisha???

  Hapa pia vigogo wa Taifa hili ndio wameweka mizizi. Utaskia vitalu vya watu wa NEC-CCM, Watoto wa Kawawa, Mwinyi, Ndugu wa Mkapa, Sokoine, Ndugu wa flani na flani. Kwa hiyo kimsingi wanapokataa bei zisipande, wanaokwamisha haya ni viongozi wetu na si vinginevyo. Mimi nadhani wananchi tukomae kuliokoa Taifa hili mana viongozi wetu hawana nia njema, wapo kwa ajili ya maslahi yao na si vinginevyo.

  Imagine bei ya Simba kwenye auction ya Safari Club International mwaka juzi ilikuwa ni $ 150,000 kuwinda South Africa. Simba wa Tanzania ana nini kinachompunguzia ubora hadi serikali isione hasara kumuuza kwa $ 4000???kwanini tembo wetu, chui wetu wauzwe kwa bei ya hasara kwenye uwindaji? Sisi tupandishe bei, wasipo kuja wanyama wetu wataendelea kuongezeka. After all, uwindaji ni mchezo wa matycoon wa nchi zilizoendelea, wao matycoon wanalipa hela nying sana kwa ma agent na kwa wenye makampuni ya uwindaji. Sisi kama taifa ndo tunaoingizwa mkenge na hawa wanaojiita outfitters ambao kimsingi ni familia za Kawawa, Sokoine, Mkapa na vigogo wengne , We unadhani kama hakuna wanachopata kwanini wamiliki wa vitalu ni wao wenyewe vigogo??? Si waachie wengine kama wao wanaona ni biashara ya hasara??Hatukatai wazawa kufanya biashara ya uwindaji, wafanye biashara kwa kufwata kanuni na kulpatia mapato stahili sio ujanja ujanja na kuwaibia watanzania kwa kukwepa kodi na kutumia majina yao kutunyonya. Wanaoongoza kuendesha seka ya Utalii South Africa ni wazawa ila wanalipa kodi zote stahiki na sio ujanja ujanja. Lakini pia wananchi tujiulize, Mbona kwenye madini Serikali inawapendelea zaidi wawekezaji kutoka nje???Iweje kwenye uwindaji neno uzawa ndo limesurface zaidi???Chanzo cha hizi double standards ni Rushwa tu na kutaka kumiliki rasilimali za nchi wao na familia zao.

  Wataalam walipendekeza hunting blocks zitolewe kwa Auctioning, ili watu washindanishwe na anayetangaza dau kubwa apewe kitalu. Utaratibu huu ungeliingizia taifa fedha nyingi sana na kufanya tasnia ya uwindaji iwe juu. Lakini kwa kuwa vigogo ndio wanataka wamiliki vitalu hivyo kwa kulipa fedha kidogo wakaona utaratibu huu uachwe kwani walijua wangefanya auctioning, wasingepata vitalu hivi wananvyomiliki sasa hivi. Tulipoteza mapato mengi sana, wanaweka kigezo cha uzawa ili wao na familia zao wagawane rasilimali zetu kwa bei chee.Chukueni rasilimali zetu, fedha zetu na mapato yetu mtulipe. Haipo hivyo. Kampuni ya Kawawa ilinyimwa kitalu kwa kushindwa kulipa kodi na michango mingine katika uwindaji, wagawa Hunting blocks wakamnyima kawawa kitalu Maige akawapa kinyemela. Yaliyotokea wote mlisikia bungeni. Kampuni ya malagarasi inayomilikiwa na Dk. Leakey pia inaubabaishaji huo huo pamoja na nyingine nyingi za wazawa. Wanataka kuendesha biashara hizi, uwezo hawana, taratibu hawazifuati, wakinyimwa vigogo wana wakingia kifua wanawapa tena. Tutafika kweli??? Nchi hii sio yenu peke yenu jamani, tupo watanzania 40 milioni, hivyo mnavyoyafanya haya mjue mnawafanyia dhuruma watu milioni 40.

  Kuna tatizo lingine kubwa sana kwenye viwanja vya kujenga mahoteli ndani ya mbuga zetu, Huko pia ndio kichekesho. Kwani mtu anapewa kiwanja bila kutoa tsh hata moja. Jamani hata shamba la huko Kazuramimba/Mbekenyela ni lazma utoe kiasi fulani. Iweje viwanja katika maeneo haya muhimu vitolewe bure????Kigogo anapewa kiwanja, then anaweza kumuuzia mtu mwingine kwa mamilioni au kumpangisha mwekezaji mwingine ndo aendeshe biashara. Akianza kuoperate ndio anaanza kulipa mapato ya serikali. System ya kukusanya mapato hayo ipo very porous na kuna alot of leakages za mapato ya serikali. Viwanja hivi pia vimegawiwa kwa vigogo wale wale, familia ya Meghji ni moja ya wanufaika. Hivi kwa nini utaratibu wa serikali usifwate katika kugawa viwanja hivi???kwann wasitangaze watu wakashindanishwa ili kupata mwekezaji bora na sio bora mwekezaji???Kwann tukubali wanufaika wa rasilimali za nchi yetu wawe ni watu hao hao wachache ilhali taifa linapata hasara na lina watu zaidi ya 40m ????

  b) Uchezeaji wa fedha katika mashirika ya uhifadhi TANAPA, NCAA, WD/TWPF

  Mashirika yanayosimamia uhifadhi yamekuwa yakifanya matumizi holela na ya anasa kanakwamba mashirika haya yanamilikiwa na nchi Tajiri sana. Ukiangalia taratibu za utendaji kazi wa mashirika haya utagundua kuwa almost chote wananchopata, wanakifaidi wenyewe. Kwa utaratibu huu hatuwezi kufika. Kama wale waliopo kwenye madini wakila chote, TRA wakila chote wanancho kusanya, bandari wakila chote hakika hatutofika. Kwa bahati mbaya serikali imekaa kimya ikiangalia haya yakitokea. Mali hizi ni zetu sote, wananofanya kazi ktk mashirika haya wanawawakilisha wananchi wengine walio maeneo mengine. Kila kinachokusanya, inapaswa kitumike wisely, after all mkumbuke biashara ya utalii ni fragile business hivyo sustainability yake bado ni questionable.

  Utakuta Tanzania inapeleka maafisa 15 kwenye maonyesho ya utalii Marekani, Kati ya hao watu watano kutoka Bodi ya Utalii TTB (SHIRIKA LENYE DHAMANA KUTANGAZA UTALII TANZANIA) watu 10 Kutoka TANAPA, WD na NCAA. Hivi huu sio uchezeaji wa hela? Sio dublication ya efforts? Kwani TTB wanaenda kutangaza vivutio gani kama sio hifadhi za Taifa, Ngorongoro na game reserves/uwindaji??Kama vipi basi muende kwa rotation ili kupunguza lundo la watu huko nje.

  Serikali inalifahamu hili ila inalifumbia macho, Ona budget za mashirika haya kwenye kusafiri nje ya nchi kwenye maonyesho ya utalii. Takwimu/Tafiti zinaonyesha watalii wanaokuja nchini hawaji kutokana na watangazaji hawa wa Tanzania, yaani sio matangazo au mahudhurio ya TTB/Tanapa/NCAA inayowafikia wateja huko nje, Wataje/watalii wengi wanapata information za Tanzania kupitia maagent wa kubwa wa utalii Duniani, TTB/TANAPA/NCAA wanajua hili ila ndo kwanza wanabeef up budget zao za kwenda kutangaza utalii nje ya nchi. Takwimu zingetumika kukataza wafujaji hawa wa nchi yetu kwenda kufanya shopping ulaya na kwingineko, at least ningeelewa kuwa watu hawa wanakwenda Training ya conservation genetics na masomo mengine ambayo technologia yake haijafika bado hapa nchin. Hali haipo hivyo. Ona budget za mashirika haya kwenye ununuzi wa magari ya kifahari.

  Wakati Pinda anadanganya taifa kuwa atasitisha ununuzi wa mashangingi kwa viongozi wa serikali, Huko Tanapa Mkuu wa hifadhi anapewa shangingi, Huko ngorongoro mkuu wa kitengo anapewa V8. Hivi tutafika kweli kwa ulifist huu? Kwanini hizo hela tusizielekeze kwenye kupambana na ujangili ambao unacause additive mortailty to legal hunting? We need to change.

  Naomba kwa leo niishie hapa, toa mchango wako wa nini kifanyike kwenye sekta hii ya maliasili ili wote tufaidi urithi huu tulioachiwa na mwenyezi mungu. Next time ntaiangalia sekta ua Utalii, katika wizara hii ya Maliasili
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Patriote, that's patriotism!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeipenda hii kitu yako jinsi ulivyoiandika. Ina taarifa zilizoshiba haswa ila ningependa kujua sources ya information zako maana katika sekta ambayo ni nyeti sana kwa ustawi na maendeleo ya jamii yetu ya kitanzania, sekta ya Maliasiri na Utalii ipo juu kidogo lakini inakabiliwa na tatizo kubwa sana la kutokuwa na taarifa ambazo ziko sahihi.
   
 4. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Source zipo nyingi, from government reports (Takwimu za misitu, Wamiliki wa vitalu). Kuhusu uvunaji haramu wa magogo source ni TRAFFIC-Tanzania, Int'l NGO inayodeal na monitoring of illegal trade of natural resources zetu. Mengine ni from scientific articles na uzoefu tu.
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kinacho niudhi ni mali asili kukamata mikaa njiani halafu waiuza hio mikaa badala ya kuzuia kukata miti hovyo
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Imetulia, ngoja ni-digest nirudi. Patriote asante sana
   
 7. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ingependeza sana kuzuia mkaa wakati nchi imeshaprovide alternative/nishati mbadala. Lakini hakuna nishati mbadala halafu unazuia mkaa. Hapo si kutwanga maji kwenye kinu???halafu unamzuia mwananchi wa kawaida kutumia mkaa wakati waziri akitoka bungeni, kwenye gari lake anabeba mkaa. Huo c ubabaishaji????Vita dhidi ya uharibifu wa mazingira haipiganwi kikamilifu.
   
 8. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Yani mzee umepita umo umo uwezi kuamini sekta hii ambayo ni nyeti kwa ustawi Taifa hili lakini imekuwa ni nyeti kwa faida ya Wajanha wachache na sio ka faida ya Taifa kwa kuanzia wale wanaoishi karibu na maliasili zetu hizo.Tena panapo uma sana ni pale kwenye board ya utalii TTB.

  Yaaani ukitizima mfumo wa kutanganza vivutia utalii vyetu huko nje umekaa kwenye sura ya kisemina semina na ujanja ujanja wa kimichongo ya ulaji na si kimasoko ya kutangaza Taifa[Business Strategy ] yani watanzania tunamaliasili mara kibao zaidi ya Kenya lakini ukituweka kwenye soko la dunia kujitangaza tunaonekana tu masikini wa maliasili na kenya ndio matajiri kushinda sisi.

  Najisikia kulia na mara zote tulisistahiki kuwa kinala wa utalii Africa lakini,unajiuliza hivi na shule zote za biashara na masoko [CBE na Mzumbe] mbona tunaoenakana tuko kichovu tena tusio na plan za kutia hamasa hata wananchi wa Taifa hili kujua kuwa nao pia wana haki ya kuhamasishwa kuwa watalii [Internal Tourist] wa kutembelea vivutio hivyo.Ni kazi ya bodi hiyo kuwajenga Watanzani kuanza kuwa na utamaduni wa kupenda maliasiali zao na hivyo kuwa na utamaduni wa kupenda maliasili zao na wao kuwa ndio watangazaji wa kwanza pale wanapokuwa kwenye diaspora.

  Mimi ni mmoja wa vijana waliojifunza maliasili na kuwa mwanachama wa Maliasili hai kwenye shule za Sekondari miaka ya tisini na 1995.Mpango huo ambao kimaajabu umekuwa wa kimasalahi ya show off nawaona kwenye maonyesho ya sabasaba wakitoka hapo imetoka!!!

  Ebu pata picha watoto wadogo shule zote Tanzania kuanzia shule za chekechea,shule za msingi,shule za sekondari na vyuo vikuu,kesho wakiwa wamejengwa kuipenda na kuilinda maliasili yao wao hao ndio watakuwa watalii, walinzi na watangaza utalii huo wa ndani na nje ya nchi.Kwa ujumla TTB sijui wanafanya kazi gani!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Usitegemee mabadiliko yeyote hata kama utawashauri maana nchi hii ni ya vigogo,watoto wa vigogo, ndugu wa vigogo, marafiki zao na wote waliokaribu nao "HAKUNA KIONGOZI WA NCHI/WIZARA ASIYEJUA NINI KINAFANYIKA NDANI YA WIZARA HII ; NI SHAMBA LA BIBI MANA UKIINGIA LEO MCHANA UWAZIRI KESHO YAKE WEWE NI MILIONEA MAANA KILA MWIZI ATAKUJA KINAFIKI NA ZAWADI ILI KUKUZIBA MDOMO USISEME KINACHOENDELEA" na inaonesha kuna mkakati maalumu ndani ya mfumo wa utawala na nje ya utawala ili waendelee kuiba rasilimali hizi
  Angalia waliopewa vibali vya kuvuna Teak Longuza/Mtibwa ni haohao nchi hii inanuka na inachocha kusema viongozi wetu mara kwa mara na wala hawasikii na hawaoni

  TAKUKURU ikokaburini na haiwezi kufufuka mpaka tukapofufuliwa(Mfano RICHMOND ni safi na hakuna rushwa baadaye.......)/usalama wa Taifa umezikwa baada kufariki mwalim na vyombo vya dola viko kuzuia maandamano na utegemee nini? Magari yananunuliwa ya washawasha ili kulinda utawala dhalim maana wanajua wanachovuna na kufaidika nayo. TUNAHITAJI KUUNGANA WENYE SHIDA NA MATESO DHIDI YA DHULUMA ZA WATAWALA ILI KUUONDOA UONGOZI DHALIMU ULIOKO MADARAKANI KWA NGUVU KWANI USITEGEMEE MABADILIKO YA HIARI ILA KUPEANA VYEO KIRAFIKI,KIDUGU,KIKABILA NA KIUKARIBU BILA UTARATIBU WA KUTAMAZA MWENYE UWEZO NA USITEGEMEE MABADILIKO YEYOTE KATIKA WIZARA HII KWANI MAWAZIRI WANALETWA KWA MALENGO MALUUM KATIKA WIZARA HII HATA SAA NYINGINE BILA UWEZO/NGUVU YA ANAYETEUA MAANA WAZIRI ANAANDALIWA NA WENYE VITALU/WENYE KUNUFAIKA NA MALIASILI ZETU
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nashauri kwanza mh ezekiel maige aipigwe chini haraka sana maana ame fail katika hili. Pili nashauri waziri ajae aweke sheria kali sana kuhusu swala la misitu
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  yangu macho tu ktika hili, lol!
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Patriote,

  Mkuu NCAA ni balaa kubwa fikiria shirika moja wanamiliki V8 sita bado magari mengine ya anasa kibao ukiwa mkuu wa kiidara kidogo unalamba gari la kifahari kama la waigizaji wa marekani !.NCAA na TANAPA ni mashirika ya umma yanayotengeneza fedha nyingi za kigeni badala ya fedha kulisaidia taifa fedha zinachezewa na wachache.
   
 13. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Huu ndio upuuzi wetu Tanzania; tunakimbilia kuomba vyandarua badala ya kuharibu mazalio ya mbu!

  Kama akili mbovu yetu inakuwa kama ya NYUMBU: full KUKURUPUKA!
   
 14. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  You are very right koingozi,katika wizara ambayo Rais anatumia muda wake mwingi kumchagua mtu atakayelinda na kutetea interests za vigogo ni hii ya maliasili, kwani vigogo ndio wamehamia katika wizara hii na wamafanya rasilimali zilizo chini ya wizara hii kama mashamba yao na familia zao. Uteuzi ataofanya Rais soon pia utareflect hili. Anyway, kwa serikali hii dokozi ya CCM tusitegemee kuokoa maliasili zetu toka kwa wakoloni hawa weusi.

  Pia ndugu usikate tamaa, rasilimali hizi sio za vigogo, ni zetu sote watu 40m. Tuchukulie vigogo wanaonufaika na rasilimali hizi wapo 1000, hivi kweli wanatushinda hawa kuwanyang'anya rasilimali zetu na kuzifanya zitusaidie sote??Kama tuliweza kupiga kelele hadi Mkapa akanyang'anywa Kiwira, inashindikana nini kupiga kelele Meghji akanyang'ang'anywa Kiwanja alichojenga hoteli mbugani ambacho pia hakikutangazwa watu wakashindanishwa???the same kwa vigogo wengine ambao wamepata rasilimali zetu kidhalimu na kwa kutumia vyeo vyao???Tuungane, tunao wabunge wazalendo, tuwape information wao watatusaidia, hii ni short term plan.

  Lakini suluhisho la haya yote ni wewe kuwaelimisha watu wanaokuzunguka juu ya umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura na waeleze kwa nini ni muhimu kwa wao kupiga kura. kama kila mmoja atafanya hivi kwa watu wanaomzunguka. Hakika tutaitoa serikali ya CCM madarakani ili tuanze kujipanga upya. Aidha, shiriki kikamilifu kwenye uandaaji wa katiba ili katiba iwe na ingredients za kizalendo na itayolenga kuwabana wezi wa rasilimali za taifa hili na wale wanaotumia vyeo na madaraka yao kujilimbikizia mali.
   
Loading...