Wizara ya Maliasili na Utalii: Kujenga utamaduni wa utalii wa ndani tuanzie hapa

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Kila halimashauri ya mji, wilaya kutenga maeneo makubwa kwa matumizi ya parks.

Idara maliasili ihifadhi uoto wa asili na kushirikiana na halmashauri husika kuwa na mpango master plan, kisha sector binafsi ishiriki kuwekeza kwa ubia pia, migahawa kumbi harusi za wazi nk.

Wizara iratibu zoo ndogo na kuweka wanyama na ndege.
 
Hakuna utalii wa ndani kama hakuna disposable income kamanda.

Huu utalii wa kiingilio cha buku 10 kwa mtu mzima na mtoto buku 5 kwa wabongo hauna tija yoyote kwa taifa.

Lazima tuwe na middle class ya kutosha ndipo utalii wa ndani utakua na maana.
 
Umaskini ni fikra duni, ndio maana tunapendeleza tuwebna maeneo ya karibu na miji yetu.Ndani ya park kuna maeneo ya bure na baadhi mfano zoo,kumbi nk unaingia mfukoni.
 
Maeneo ya bure yakitembelewa na wananchi then yanaleta tija gani kwa uchumi wa taifa.?
 
Unajua multiplier effect kitendo mtu kutoka out atatumia usafiri,pia kule kuna watoa huduma mbalix2 vinywaji nk.
 
Kumbe unaongelea vijisenti?

Hapo sawa.
Kuna faida nyingi sana, sio wote wana fursa kuwa na garden majumbani kwao, recreation , miji inahitaji bafa zone kupumua, kubwa zaidi kuwapa watu furaha na utamaduni kutoka out na baadae culture kuthamini utalii wa ndani.
 
Kila halimashauri ya mji, wilaya kutenga maeneo makubwa kwa matumizi ya parks.

Idara maliasili ihifadhi uoto wa asili na kushirikiana na halmashauri husika kuwa na mpango master plan, kisha sector binafsi ishiriki kuwekeza kwa ubia pia, migahawa kumbi harusi za wazi nk.

Wizara iratibu zoo ndogo na kuweka wanyama na ndege.
Binafsi niongezee tu uwekezaji wa kitalii katika miji yetu ya kitalii! Halimashauri zitenge maeneo maalumu ya maegesho ya magari hii itasababisha watu kutembea zaidi nakuvinjari kwa uhuru, ipigwe marufuku kupaki magari au kupitisha malori katikati ya maeneo yanoyotembelewa na watalii, zitolewe leseni zitakazo ruhusu uwekezaji wa kitalii kama restaurants zenye mapishi tofauti mfano huyu anauza kahawa, chai na Vitafunwa vya kikwetu, anyayefuata anauza vyakula vya Kiswahili anayefuata vya kihindi anauefuata vyakula vya kizungu anayefuata kichina! Kuwe na street kabisa inajulikana kwa mambo ya kiswahili alkasusu unapata mihogo , ndizi za kuchoma uji wa shanga na mazaga yoote ya kiswahili, kuwe na street ya uchoraji na kuchonga vinyago tu, kuwe na mesiums ndogo ndogo, kila jiji husika, ulinzi uimarishwe, kuwekwe gym safi kwa wageni, kuwe na safari clinic kila jiji hii itasaidia kutoa taarifa nzuri zaidi za mbuga zetu, nights club na bars or pubs zenye heshima ya kitalii! Kuwekwe mfumo wa ulipaji mzuri kwenye mageti yakuingilia parks kwa Wazawa sio kila mTanzania ana kadi ya VISA! Yakizingatiwa haya kwa kuanza kila siku sisi niwatalii wa ndani
 
Kuna faida nyingi sana, sio wote wana fursa kuwa na garden majumbani kwao, recreation , miji inahitaji bafa zone kupumua, kubwa zaidi kuwapa watu furaha na utamaduni kutoka out na baadae culture kuthamini utalii wa ndani.
Tutengeneze middle income ya kutosha, hawa maskini wataishia kuchafua mazingira tu boss.
 
Binafsi niongezee tu uwekezaji wa kitalii katika miji yetu ya kitalii! Halimashauri zitenge maeneo maalumu ya maegesho ya magari hii itasababisha watu kutembea zaidi nakuvinjari kwa uhuru, ipigwe marufuku kupaki magari au kupitisha malori katikati ya maeneo yanoyotembelewa na watalii, zitolewe leseni zitakazo ruhusu uwekezaji wa kitalii kama restaurants zenye mapishi tofauti mfano huyu anauza kahawa, chai na Vitafunwa vya kikwetu, anyayefuata anauza vyakula vya Kiswahili anayefuata vya kihindi anauefuata vyakula vya kizungu anayefuata kichina! Kuwe na street kabisa inajulikana kwa mambo ya kiswahili alkasusu unapata mihogo , ndizi za kuchoma uji wa shanga na mazaga yoote ya kiswahili, kuwe na street ya uchoraji na kuchonga vinyago tu, kuwe na mesiums ndogo ndogo, kila jiji husika, ulinzi uimarishwe, kuwekwe gym safi kwa wageni, kuwe na safari clinic kila jiji hii itasaidia kutoa taarifa nzuri zaidi za mbuga zetu, nights club na bars or pubs zenye heshima ya kitalii! Kuwekwe mfumo wa ulipaji mzuri kwenye mageti yakuingilia parks kwa Wazawa sio kila mTanzania ana kadi ya VISA! Yakizingatiwa haya kwa kuanza kila siku sisi niwatalii wa ndani
Wadau utalii wapitie hoja hizi mipango ni muhimu, dunia ijayo utalii wa mfumo wa maisha ya jamii ni muhimu sana.
 
Tutengeneze middle income ya kutosha, hawa maskini wataishia kuchafua mazingira tu boss.
Dunia ya leo inahitaji kuchangamana, kupitia kuchangana ndio tunaongeza fursa ,kipato na furaha ya maisha.Furaha ni haki ya msingi kwa binadamu yeyote bila kujali kipato.
 
Theoretically YES lkn huwezi kua furaha wakati huna pesa
 
Back
Top Bottom