Wizara ya Maliasili na Utalii, Iko wapi nguvu yenu katika kanda za Kati, Nyanda za Juu kusini, Kusini na Mashariki?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,227
26,048
Leo napenda kuwauliza Wizara ya Maliasili ya Utalii;

1. Kumekuwa na kupungua Wanyama Mbuga za Mikumi na Saadani kwa kiwango cha kutisha! Leo hii ukienda Hifadhi ya Saadani unaweza tembea saa zima bila kuona mnyama yeyote, hali hii ipo Mikumi pia ambapo imekuwa na hali kwa kasi ya kutisha sasa.

Kwa tuliokuwa tukipita miaka iyo mbugani mikumi ilikuwa ni Wanyama tu sehemu kubwa ya mbuga, hata Hifadhi ya Saadani pia.

Swali langu kwenu, Kwa jitihada hizi anazofanya Mhe. Rais za kukuza Utalii ambazo tayari tumeona zinaanza kuleta matokeo, mmejipangaje kwenye Mbuga hizi mbili? Ile miradi yenu ya kuchimba mabwawa ya maji ili wanyama wasiwe na shida ya Maji kwenye hifadhi hizi imefikia wapi?

Tuliona mkipandikiza wanyama hifadhi mpya ya Burigi chato? Kwa nini hamjaweka uwekezaji wa kupandikiza Wanyama kwenye hifadhi hii pia? Mnataka hadi mtumbuliwe ndo muamke?

2. Kwa miaka sasa imeongelewa kujengwa Barabara ya lami kuelekea hifadhi za Ruaha na Kitulo!
Sasa kipi kinasababisha barabara hizi zisijengwe miaka nenda rudi? Mmeshindwa kujenga hoja Serikalini Barabara hizi kujengwa? Kwa nini?

Nauliza swali hili Kwa sababu kwa Miaka mingi sasa utalii umekuwa Kanda ya Kaskazini, na Watalii wengi wamekuwa wakienda huko kutokana na ubora wa miundombinu. Hili lime kuwa likinufaisha sana Jamii za kanda hizo!

Sasa shida ni nini Kwa Kanda hii ya Nyanda za Juu kusini? Mnataka Jamii hizi ziendelee kuwa nyuma hadi lini Kwa miondombinu mibovu ambayo imekuwa ikisababisha fursa zilizopo kwao zisifikiwe kwa u rahisi??

3. Selous ni Jina kubwa Duniani- Je nini kinawazuia kuhamasisha Serikalini ujenzi wa barabara kuelekea hifadhi ya Selous? Nini kinawazuia kuibrand Selous kiutalii na kiuwekezaji Kama mnavyofanya kwa Serengeti na Ngorongoro?

Kwa ninavyojua Mbuga ya Selous inaweza kuwa na Wanyama wengi kuliko hata Serengeti? Ila kwa nini mmelala? Upo wapi uzalendo wenu? Yapo wapi mapenzi yenu kwa Taifa katika kuhamasisha utalii katika maeneo haya? Leo Selous ikiingiza watalii wengi na kusifika duniani nyie haifai siku? Taifa halifaidiki?

Jamii zinazozunguka Selous ni maskini sana, tofauti na Jamii zinazozunguka Hifadhi Kama ya Mlima Kilimanjaro. Hili limetokana na hela za hifadhi zinazoenda kujenga miradi kwenye jamii hizi( Miradi ya ujirani mwema). Hili limenufaisha sana mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Sasa hamuoni Kuna hata ya kuibrand Selous na kuiwekea miundombinu Mingi ya kiuwezesha kutumika na kufikika ili nayo ipate hela na jamii zinazozunguka mbuga hii zofaidike na uwepo wake?

4. Mwisho ni Dodoma, Kanda ya Kati. Leo hii kuna ujenzi mkubwa wa Mahoteli unaendelea Dodoma! Kusema kweli wanajitahidi sana kuijenga na kuweka miundombinu sawa! Hili linaweka uhakika kuwa Watalii sasa wanaweza Kuja na kufanya maisha yao Dodoma!

Swali langu kwenu. Dodoma kuna mapori ya Swagaswaga na Kuna mbuga iliyopo Kondoa ambayo nayo ina Wanyama wengi sana.

Kutoka Dodoma Mjini hadi Kondoa si zaidi ya Masaa mawili. Kutoka Dodoma Mjini hadi pori la Swagaswaga sidhani Pia Kama inazidi masaa 2 au 3.

Hizi ni fursa za Mkoa wa Dodoma ambapo inaifanya Dodoma kuwa tayari hata kuandaa mikutano mikubwa na matamasha makubwa na kupokea Pia Watalii kwa shughuli za utalii!

Je hamjaona kuwa Kuna haja ya kuhamasisha miradi ya ujenzi wa barabara za Rami kuelekea huko kwenye hizi mbuga? Hamuoni hata Kuna haja ya kufanya mchakato kuzifanya hizi mbuga hifadhi? Kama mlivyofanya kwa Burigi Chato? Nini kinawakwamisha? Mkutano ukifanyika Dodoma si inawezekana kabisa wageni wakaandaliwa hata siku 1 kwenda kufanya game drive kwenye hizi mbuga? Watalii nao si wanaweza kuja Dodoma kwa utalii wa kwenye hizo mbuga?

Leo hii Mhe. Rais kafanya Royal Tour, hamuoni Kuna haja ya kupeleka miundombinu ya barabara kote huko ili nako kukapate keki hii ya Taifa ambayo nchi itaenda kunufaika nayo?

Mwisho napenda kuwaambia Wizara ya Maliasili na Utalii. Nyie ndo kundi la Wizara 4 zinazoubeba uchumi wa nchi hii mkiwa na Wizara na Nishati pamoja na Wizara ya Madini bila kusahau Uchukuzi kwenye Bandari!

Kiuchumi nyie mkikaa vizuri Taifa hili litakuwa mbele sana kimaendeleo! Na Kuna uwezekano hata tukaongoza Africa hii kwa uchumi imara.

Naomba muamke! Nchi hii watu wenye akili wapi wengi na wanawaangalia sana!

Muwe na weekend njema!

Wizara ya Uvuvi mjiandae Kwa makavu yenu pia!
 
Waziri husika aliwahi kutuaminisha watanzania kuwa chato ndiyo kitovu cha utalii hapa nchini.
 
Sijakuelewa!

Nani hawana faida? Unajua sekta inayoingoza kwa kuchangia pato la Taifa hapa Tanzania ni utalii?
Kwa sasa watanzania wa kawaida hawaoni faida ya huo utalii maana kama ungekuwa unaingiza mapato makubwa leo hii serikali isinge tukamua jasho la damu kwa tozo lukuki.
 
Kwa sasa watanzania wa kawaida hawaoni faida ya huo utalii maana kama ungekuwa unaingiza mapato makubwa leo hii serikali isinge tukamua jasho la damu kwa tozo lukuki.
Unajua bila ya icho tunachokipata kwenye utalii hali ya nchi ingekuwaje?
 
Mbona hatunufaiki sasa na utalii wenyewe? Zanzibar hakuna mbunga lakini utalii ndiyo unaingiza zaidi 80% pato la taifa
Kunufaika ni hoja pana sana!
Mishahara ya watumishi ikiwemo madokta na manesi wanaokutibia ukiumwa, askari wanaokulinda, inaweza kuwa ndo inatokana na pesa hizo!
 
Samia unaye msifia ndio huyo huyo anayeangamiza unavyohitaji vifanyike kwa usahihi.
Chochote kibaya au kizuri jua ni design yake huyo Samia.
 
Tatizo watawala wana vipau mbele vyao kwa maslahi yao na siyo nyinyi kina kwangu pakavu
Vipaumbele vyao lazima vizingatie hoja kuu kuwa ni lazima tutengeneze fursa za kupata hela na mapato mengi zaidi kwa faida ya nchi
 
Samia unaye msifia ndio huyo huyo anayeangamiza unavyohitaji vifanyike kwa usahihi.
Chochote kibaya au kizuri jua ni design yake huyo Samia.
Samia ana miezi 6 tu tangu awe Rais! Haya mambo yapo siku nyingi kabla hata hajawa Rais!
 
Kuhusu Selous miaka mingi najiuliza kulikoni, nina swali kwa wenye ufahamu hivi mikumi na Ruaha hazijamegwa Selous? Selous bado mpaka leo ni pori la akiba
 
Kwa sasa watanzania wa kawaida hawaoni faida ya huo utalii maana kama ungekuwa unaingiza mapato makubwa leo hii serikali isinge tukamua jasho la damu kwa tozo lukuki.
Kwani bado mnakamuluwa tozo? Si mnapumua?
 
Kuhusu Selous miaka mingi najiuliza kulikoni, nina swali kwa wenye ufahamu hivi mikumi na Ruaha hazijamegwa Selous? Selous bado mpaka leo ni pori la akiba
Kwa mda mwingi ilikuwa inatumika kama Game Reserve! Saivi wamegawanya upande ni hifadhi ya Nyerere upande mwingine imebaki kuwa Game Reserve.

Ruaha National Park iko Iringa upande wa kulia kuelekea Mbeya. Inapakana na Wilaya ya Mbarali Kama sikosei Kwa Mbeya
 
Back
Top Bottom