Wizara ya maliasili kwa hili mnawaumiza wananchi

Glue

Senior Member
Jan 14, 2011
156
49
Hivi juzi katika pitapita zangu kutoka moja mikoa ya kusini, nilitaka kununua mkaa barabarani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwangu( gunia moja tu).

Kabla ya kununua nialiamua kupita kwanza kwenye moja ya ofisi ya maliasili ili kupata kibali kwani niliambiwa ukikamatwa na hata gunia moja la mkaa ni kesi na fine zake ni mara dufu. Kuingia katika ofisi hiyo nikaambiwa nije na gunia langu la mkaa kwani wanapima kwa kilo hivyo wasingeweza kunikadiria.

Nikarudi kuchukua gunia langu ambalo nililinunua kwa gharama ya shilingi elf kumi na nne za kitanzania. Walipopimba nikatakiwa kulilipia ushuru wa shilingi elfu kumi na nane za kitanzania.

Sasa nikajiuliza, hapa ni nani ananufaika na biashara hii, Muuzaji ambaye anatumia muda na resources zake na mwisho kupata shilingi elfu 14 ama Serikali ambayo inapata zaidi ya garama za uzalishaji wa huduma hiyo????

Nikajiuliza sana, kama lengo ni kudiscourage matumizi ya mikaa je subsidization ya nishati zingine kama gas na umeme imefanyika ili kumwokoa huyu mwananchi wa hali ya chini kabisa ambaye yy tegemeo lake ni Mkaa??? Mimi nilidhani haya maushuru ni kwa wale wanaofanya biashara tu kumbe hata kwa mtumiaji wa mwisho?????

Kwa hali hii sijui kama tutafika tunakokwenda.
 
Duuuh mkuu nimeshangaa kuona mkaa unapimwa kwa kilo hii ni zaidi ya ufisadiila ndo tunaisoma hivo
 
Yani sjajua nini maana ya upimaji huu. Labda wajuzi wa haya mambo waje watufahamishe. Kuisoma namba ni lazima mkuu
 
Minimewahi kushushiwa mkaa wangu pale tinde yaani nimeununua kwa elfu kumi ushuru 18,000
 
Hata wale wanaofanya biashara ya Mkaa kama wakifuata taratibu zote na kulipia ushuru wote stahiki,bei ya mkaa haitakamatika mijini,sema tu ndo hivyo tena vielfu tano tano vya kubrashia viatu vinasaidia gunia linafika mjini kwa bei nafuu kidogo.
Ukitaka kufanya biashara ya mkaa,utaratibu ni kama ifuatavyo;
  1. Unafanya usajili (Registration) 261,000/=Kwa mwaka.
  2. Unanunua gunia la mkaa kutoka kwa mchomaji 14,000/=
  3. Unalipa ushuru wa Halmashauri 1,000/= au 2,000/=Kwa kila gunia
  4. Unalipa ushuru wa serikali kuu 15,000 hadi 18,000/= kwa kila gunia
  5. Unasafirisha (Kutegemeana na umbali) ila kwa maeneo mengi 5,000/=kwa gunia
  6. Unamlipa mpakiaji na mshushaji 1,000/=Kwa gunia
  7. Unanunua mfuko (roba) 750/=Kwa gunia Jumla 40,750/=(Maximum) Weka na faida hapo. Hatariiiiiiiiiiiiiiii!!
 
Ndio maana tunaumizwa huku mijini.Sasa tukimbilie wapi jamani kwani umeme na gesi navyo havishikiki, kuni mijini hakuna. itafikia wakati kupika chakula itakua anasa. Tutajilia vibichivibichi
 
Ni hatari sana mkuu.
 
Hivi juzi katika pitapita zangu kutoka moja mikoa ya kusini, nilitaka kununua mkaa barabarani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwangu( gunia moja tu).

Kabla ya kununua nialiamua kupita kwanza kwenye moja ya ofisi ya maliasili ili kupata kibali kwani niliambiwa ukikamatwa na hata gunia moja la mkaa ni kesi na fine zake ni mara dufu. Kuingia katika ofisi hiyo nikaambiwa nije na gunia langu la mkaa kwani wanapima kwa kilo hivyo wasingeweza kunikadiria.

Nikarudi kuchukua gunia langu ambalo nililinunua kwa gharama ya shilingi elf kumi na nne za kitanzania. Walipopimba nikatakiwa kulilipia ushuru wa shilingi elfu kumi na nane za kitanzania.

Sasa nikajiuliza, hapa ni nani ananufaika na biashara hii, Muuzaji ambaye anatumia muda na resources zake na mwisho kupata shilingi elfu 14 ama Serikali ambayo inapata zaidi ya garama za uzalishaji wa huduma hiyo????

Nikajiuliza sana, kama lengo ni kudiscourage matumizi ya mikaa je subsidization ya nishati zingine kama gas na umeme imefanyika ili kumwokoa huyu mwananchi wa hali ya chini kabisa ambaye yy tegemeo lake ni Mkaa??? Mimi nilidhani haya maushuru ni kwa wale wanaofanya biashara tu kumbe hata kwa mtumiaji wa mwisho?????

Kwa hali hii sijui kama tutafika tunakokwenda.
Tanzania ya viwanda inakuja, kaa tayari.
 
Imeanza lini hii? Nnavyoelewa gunia moja kwa matumizi ya nyumbani inaruhusiwa!
 
Tafadhalini sana.... Msinunue wala kutumia mkaa utokanao na mazao ya misitu yetu...
Mtatuletea jangwa na madhila mengine ya mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change)!
Alafu kwanza kwanini utumie mkaa ambao vile vile unazalisha carbonmonoxide..??
 
Back
Top Bottom