Wizara ya maliasili kwa hili mnawaumiza wananchi

Tafadhalini sana.... Msinunue wala kutumia mkaa utokanao na mazao ya misitu yetu...
Mtatuletea jangwa na madhila mengine ya mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change)!
Alafu kwanza kwanini utumie mkaa ambao vile vile unazalisha carbonmonoxide..??
Tutumie nini sasa?
 
Hivi juzi katika pitapita zangu kutoka moja mikoa ya kusini, nilitaka kununua mkaa barabarani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwangu( gunia moja tu).

Kabla ya kununua nialiamua kupita kwanza kwenye moja ya ofisi ya maliasili ili kupata kibali kwani niliambiwa ukikamatwa na hata gunia moja la mkaa ni kesi na fine zake ni mara dufu. Kuingia katika ofisi hiyo nikaambiwa nije na gunia langu la mkaa kwani wanapima kwa kilo hivyo wasingeweza kunikadiria.

Nikarudi kuchukua gunia langu ambalo nililinunua kwa gharama ya shilingi elf kumi na nne za kitanzania. Walipopimba nikatakiwa kulilipia ushuru wa shilingi elfu kumi na nane za kitanzania.

Sasa nikajiuliza, hapa ni nani ananufaika na biashara hii, Muuzaji ambaye anatumia muda na resources zake na mwisho kupata shilingi elfu 14 ama Serikali ambayo inapata zaidi ya garama za uzalishaji wa huduma hiyo????

Nikajiuliza sana, kama lengo ni kudiscourage matumizi ya mikaa je subsidization ya nishati zingine kama gas na umeme imefanyika ili kumwokoa huyu mwananchi wa hali ya chini kabisa ambaye yy tegemeo lake ni Mkaa??? Mimi nilidhani haya maushuru ni kwa wale wanaofanya biashara tu kumbe hata kwa mtumiaji wa mwisho?????

Kwa hali hii sijui kama tutafika tunakokwenda.

Kununua 14,000
Kodi 18,000
Jumla 32,000.
Hii nchi raha sanaa.
 
Tafadhalini sana.... Msinunue wala kutumia mkaa utokanao na mazao ya misitu yetu...
Mtatuletea jangwa na madhila mengine ya mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change)!
Alafu kwanza kwanini utumie mkaa ambao vile vile unazalisha carbonmonoxide..??
Wewe ni mungu wa dar?
 
Back
Top Bottom