Wizara ya Maji yawataka Wakandarasi walioacha miradi yao kisa Corona kurudi katika maeneo yao ya kazi kuendelea na utekelezaji wa miradi haraka

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewaagiza wakandarasi wote walioitelekeza miradi ya maji kwa sababu ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona kurudi kwenye maeneo yao ya kazi kuendelea na utekelezaji haraka.
Naibu Waziri Aweso amekasirishwa na utendaji wa wakandarasi wa Kampuni za M/S Nangai Engineering Ltd na M/S Nipo Africa Engineering Ltd wanaosuasua katika utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Vijiji 6 vya Songambele, Mlowa, Majengo, Tambukareli, Zinginali na Itigi katika Halmashauri ya Itigi, mkoani Singida.

Akisema kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 zimeshatolewa kwenye mradi huo na maendeleo ya kazi yakiwa nyuma ya ratiba na kukwamisha lengo la mradi unaotarajiwa kuhudumia wakazi wapatao 31,000 katika vijiji 6 vinavyozunguka mji wa Itigi.

“Kipindi hiki cha Ugonjwa wa Corona, ni haki kwa kila mtanzania kupata huduma toshelevu ya maji ili kulinda afya za wananchi dhidi ya ugonjwa huu, pia Serikali inachukua hatua madhubuti kukamilisha haraka miradi ya maji ili iweze kutoa huduma ambayo ni haki ya kila mtanzania’’, amesema Naibu Waziri Aweso.

“Nawaagiza wakandarasi wote walioitelekeza miradi ya maji kwa sababu ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona warudi kwenye maeneo yao ya kazi na kukamilisha ujenzi wa miradi haraka, ni kweli ugonjwa upo tunachotakiwa ni kuchukua tahadhari lakini kazi zisisimame, atakayekaidi agizo la Serikali tutamchukulia hatua za kisheria kwa kuwa atakuwa anatukwamisha”, ameonya Naibu Waziri Aweso.
Akiwatahadharisha wakandarasi kuacha tabia ya kuitelekeza miradi kwa muda mrefu, na kuonekana kwenye maeneo ya kazi pindi viongozi wa wizara wanapokuwa wakifanya ziara za kukagua miradi hiyo kwa lengo la kutaka kuridhisha viongozi hao.
 
Back
Top Bottom