Wizara ya Madini Yaomba Shilingi Bilioni 89.3 kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,893
940

WIZARA YA MADINI YAOMBA SHILINGI BILIONI 89.3

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ameliomba Bunge liridhie na kupitisha makadirio ya shilingi 89,357,491,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Akizungumza Bungeni Aprili 27,2023 Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 amesema Shilingi 23,172,550,000.00 ikiwa ni fedha za maendeleo na Shilingi 66,184,941,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 20,307,498,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi 45,877,443,000.00 ni Matumizi Mengineyo

VIPAUMBELE SITA VYA WIZARA YA MADINI 2023/2024

Wizara ya Madini imetoa vipaumbele vyake kwenye mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye lengo la kuhakikisha sekta ya madini inachangia kujenga uchumi imara na kuongeza pato la Taifa kupitia rasilimali Madini.

Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema Wizara ya Madini imepanga kutekeleza vipaumbele 6 ambavyo ni.

1. Kuimarisha Ukusanyaji wa Maduhuli na Kuongeza Mchango
wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.

2. Kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati.

3. Kuwaendeleza na Kusogeza Huduma za Ugani kwa
Wachimbaji Wadogo.

4. Kuhamasisha Shughuli za Uongezaji Thamani Madini.

5. Kuhamasisha Uwekezaji na Biashara katika Sekta ya Madini

6. Uanzishwaii wa Minada na Maonesho ya Madini ya Vito

7. Kuzijengea Uwezo Taasisi zilizo Chini ya Wizara ya Madini ili
Ziweze kutekeleza Majukumu Yao kwa Ufanisi Zaidi

Waziri Biteko ameyasema hayo wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Madini Bungeni, Dodoma.
 

Attachments

  • Fuvj9LcWcBsvOJU.jpg
    Fuvj9LcWcBsvOJU.jpg
    157.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-27 at 19.20.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-27 at 19.20.40.jpeg
    145.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom