Wizara ya Kilimo yatangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba ametangaza kuwa ofisi yake itahamia Dodoma wiki ijayo.

Uamuzi huo umekuja baada ya Waziri Mkuu kutangaza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwamba ofisi yake itahamia Dodoma ifikapo Septemba na wizara nyingine zitamfuata.

“Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhamia Dodoma kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Magufuli la kila wizara kuhamia makao makuu ya nchi, hivyo wiki ijayo wizara yangu inatarajia kuhamia Dodoma,” alisema Dk Tizeba jana alipokutana na wadau wa mifuko ya hifadhi za jamii na bandari kujadili uwekezaji katika uvuvi wa bahari kuu ili Serikali iweze kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo.


Chanzo: MWANANCHI
 
Sifa sifa sifa
Kichwa maji kweli mbowe angetangaza kuamia dodoma ingekuwa sifa.....!!!
badilikeni watanzania mnataka mtendewe lipi nzuri. Msapoti.
Mpango wa kuhamia Dodoma ilikwepo toka enzi za nyerere. Hata ilani ya chadema na act wazalendo ipo.
Tumepata rais anayetekeleza kwa vitendo mnaleta hoja ya sifa sifa.
Mtazungusha mikono hadi iwazungushe
 
Wizara hii ina majengo zaidi ya moja ya ofisi ni kwa nini isihamie
 
Kwani hawawezi kuhamia Dodoma mpaka watoe hotuba? Sifa sifa tu.
 
Hili jambo la kuhamia dodoma ni rahisi sana. Majengo yaliyopo dar ya ofisi yanapangishwa kwa private au yanauzwa kabisa. Kisha pesa zinapatikana.
 
Back
Top Bottom