Wizara ya Kilimo yasema Serikali imeruhusu mazao ya kilimo kuuzwa nje ili kuwaimarisha Wakulima kiuchumi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imeruhusu mazao ya chakula kuuzwa nje ya nchi ili kutoa fursa kwa Wakulima kunufaika na mazao mbalimbali wanayoyazalisha.

Imesema kuwa itakuwa ikitoa vibali kwa wafanyabiashara wa mazao.

Hayo alisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya kilimo iliopo mkoani Morogoro, ambapo aliwataka wakulima kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi.

“Serikali kupitia wizara yangu imeamua kufungua fursa kwa wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kulingana na mahitaji ya soko la nchi husika ili kuwapa faida wakulima hao na kuwaimarisha kiuchumi zaidi,” alisema Kusaya.

Kusaya alisema Wizara ya Kilimo inawataka wafanyabiashara wa mazao hasa ya chakula kujitokeza kufanya biashara nje ya nchi kwani serikali itakuwa bega kwa bega kutoa vibali kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza mazao yao nje.

Katibu Mkuu huyu alisema serikali imeruhusu mazao kuuzwa nje nchi ili kutoa fursa ya kuongeza soko kwa wakulima kupata faida zaidi kutokana na kutumia nguvu nyingi katika uzalishaji wa mazao mbalimbali hasa ya chakula.
 
Mhh, mchele ulipobuma Lake, tiyari. Basi iwe endelevu na kwa style moja. Hongera.
 
Walikuwa wapi wakulima tumejinyima mwaka mzimaa, tukitegemea mazao yatapanda bei, tupate ada, hakuna, msimu mpya wa kilimo umeanza, mazao bei chini, hatuna hata hela ya kulimia mwaka huu!

Mi5 tena imeanza na maumivu makali sana kwa mkulima kama mie!

Wanasiasa siyo watu ni viatu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mchele tunakula kwa 1,000 kwa kilo. Naona tutanua kwa 2,000 sasa
 
Hili niendelevu au linaangalia upepo? Kuna haja ya bunge kulitungia sheria hili suala. Unaweza lima ukategemea utapeleka mchele DRC unashangaa wamefunga tena.
 
Duu! Tangu serikali ya awamu ya kwanza tulitangaza kilimo kuwa uti wa mgongo wa taifa letu lakini cha kushangaza ni namna tulivoshindwa kuwa na dira endelevu ya kukuza uchumi wa mkulima! Leo utasikia huku wakulima wamekopwa mazao, keshoa utasikia wakulima wamezuiwa kusafirisha mazao nje ya nchi huku hapa nchini kukiwa hakuna soko!

Kama serikali kweli ina dhamira ya kuwawezesha wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kwa faida nzuri, na ihakikishe inaandaa mazingira rafiki tangu kwenye utoaji wa vibali mpaka kwenye tozo za ushuru!

Kuna wakati kunakuwa na ubabaishaji sana kwenye vibali hivyo na pia tozo nazo zinakuwa nyingi mno matokeo yake faida yote ambayo mfanyabiashara angeipata inazama kwenye gharama za vibali na tozo!
 
IDuu! Tangu serikali ya awamu ya kwanza tulitangaza kilimo kuwa uti wa mgongo wa taifa letu lakini cha kushangaza ni namna tulivoshindwa kuwa na dira endelevu ya kukuza uchumi wa mkulima! Leo utasikia huku wakulima wamekopwa mazao, keshoa utasikia wakulima wamezuiwa kusafirisha mazao nje ya nchi huku hapa nchini kukiwa hakuna soko!

Kama serikali kweli ina dhamira ya kuwawezesha wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kwa faida nzuri, na ihakikishe inaandaa mazingira rafiki tangu kwenye utoaji wa vibali mpaka kwenye tozo za ushuru!

Kuna wakati kunakuwa na ubabaishaji sana kwenye vibali hivyo na pia tozo nazo zinakuwa nyingi mno matokeo yake faida yote ambayo mfanyabiashara angeipata inazama kwenye gharama za vibali na tozo!
Mkuu kilimo kimevamiwa na hao hao wanaojiita waheshimiwa, ukisikia mikopo ya 🚜 basi ujue watajikopesha wao wala siyo mkulima, mkulima atakodisha kwao akalimie, na hao huwa hawalipi hata senti!

Ukisikia pembejeo watapeana wao, watatuuzia sisi wakulima, wao wametunga sheria kuhakikisha mkulima mdogo hakopesheki basi akikopa abanwe alipe riba kubwa.

Hakuna sera ya kutusaidia, kilimo ni fani ya mwisho kabisa kupata heshima katika nchi hii.
Ukija kwenye kusafirisha mazao ya nafaka nje ya nchi, kichefuchefu na kwikwi, ndiyo matamko kila uchwao!

Hakuna dira wala muelekeo!

Everyday is Saturday............................😎
 
Back
Top Bottom