Wizara ya Kilimo, ninaomba hii ipite kwenye dawati lenu la maoni

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KWENYE PARETO BADO KUNA UKAKASI, PAMOJA NA MAJIBU YA MH BASHE.....

Na Elius Ndabila.
0768239284

Mh Bashe Naibu Waziri wa Kilimo, pamoja na majibu mazuri kwa Mh Njeza Mbunge wa Mbeya vijijini ( Mh Rais atanisamehe kwa kuwa hapendi kielezi cha Vijijini) bado mimi kuna suala ambalo linanisumbua sana.

Mh Bashe akijibu swali la msingi la Mhe Njeza alisema bei ya PARETO ni shilingi 2500/= hadi 4000/=. Alisema malipo ya awali ni 2500/= na pare PARETO ikipimwa na kuonekana ina sumu nzuri mkulima hulipwa Tshs 4000/=, SAWA.

Hoja yangu inaanzia hapa, tunajua kuwa wakulima wengi ni wakulima wadogo wadogo ambao wakati mwingine ni ngumu kujaza gunia mtu mmoja. Wakati mwingine kutokana na mchumo wa PARETO gunia moja wanatumia watu zaidi ya kumi. Na kwa majibu ya Mh Bashe amesema kuwa mkulima hulipwa malipo ya awali ya Tshs 2500/= na pale PARETO itakapofika kiwandani na kupimwa kuwa inasumu basi mkulima huongezewa fedha na kupewa jumla ya Tshs 4000/=.

Ninataka kujua kama watu waliweka PARETO kwenye gunia zaidi ya kumi utajuaje ni PARETO ya nani ilikuwa na sumu na ya nani haikuwa na Sumu? Hatuoni kama serikali kwamba kuna watu tunawabebesha liability ambayo si ya kwao? Je huko kiwandani wanakoenda kupima kiwango cha sumu Wananchi wanamteua mwakilishi wa kwenda kuthibitisha uhalisia wa sumu? Kama si hivyo kwa nini Sumu isipimwe pale tu mtu anapokuja kuwauzia PARETO? Hamuoni kama wananchi wanaibiwa kwa kuwa mwenye kiwanda anaweza sema PARETO zote hazikuwa na sumu?

Lakini pia nataka kujua, je bei ya 4000/= ni elekezi kwa nchi nzima au nayo ni zoning? Mbona bei halisi ya Ileje hususani kata ambazo zinalima sana PARETO kata za Itale, Ibaba na Ngulilo bei haijafika huko?

Hoja nyingine Mh Njeza ameuliza kwa nini serikali isiondoe ununuzi wa Zoning? Mh Bashe amesema hawawezi kuondoa kwa ununuzi wa Zoning kwa kuwa PCT imefanya uwekezaji hivyo hawawezi kuruhusu competition kwenye ununuzi. Lakini ukienda kufanya utafiti ukweli huo ni mdogo. Wananchi wengi wanajitengenezea mbegu zao kwa kukausha mbegu ambazo zimekwisha kukomaa. Hata suala la vikaushio vimejengwa kwa mawakala wa PCT na si kwa umma.

Ninadhani sasa ni wakati wa serikali kuruhusu wanunuzi kuingia mkataba na wa kulima kuliko ujanja ujanja huu PCT ambao hauruhusu free and fair competition kwenye market. Hii itasaidia kujibu maswali ya wakulima ambao wanaona kama Zoning inawakandamiza. Wakulima wanaona Zoning inafanya PARETO bei zake kuwa chini kwa kuwa PCT amefanya monopolization kitu ambacho wakulima hawana choice. Hata mkigandamizwa mnauza tu.

Lakini pia hii itaondoa urasimu kwenye mauzo. Mkulima akiwa na shida atauza PARETO yake muda wowote kuliko sasa mununuzi mmoja, Wakala anaweza kufungua ofisi muda anaoamua yeye.

Lakini Mhe Bashe anasema anawakaribisha wawekezaji, sasa watawekeza wapi wakati kuna monopolization ya PCT?

Mwisho ni kweli kuwa utafiti unaendelea kuhusu kupata dawa ya viwatilifu vinavyotokana na PARETO, kwenye jibu lako umesema TARI Uyole wanashirikiana na PCT. Hili ni jambo jema, nilitaka kujua hawa Tan Extra ltd wanashirikiana na TARI Uyole? Maana kwenye tafiti zangu niliona harakati zao pia.

Mwisho ninadhani sasa wa serikali kuruhusu final product hapa hapa nchini badala ya kwenda Marekani ili kuongeza munyororo wa thamani kwenye zao letu.
 
Nilidhani utaanza na Korosho maana bado watu hawajapewa hela zao. Unakwenda mbele alafu kuna siku utarudi kwenye malipo.
 
Back
Top Bottom