Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji wana cha kujifunza kupitia msomi huyu kubadili maisha ya vijiji vikame nchini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Kijiji cha Hiware Bazar ni kijiji kilichoko wilaya ya Ahmednagar Jimbo la Maharashtra, India. Kijiji hicho kilikuwa na ukame wa kupindukia ambacho watu wengi waliamua kukihama na kukitelekeza.

Kwenye hicho kijiji anapatikana mwenyekiti bora wa kijiji anayesifiwa sana duniani aitwaye Popatrao Bajugi Pawar.Huyu ni msomi mwenye digrii mbili ambaye alipomaliza digrii zake akiwa msomi pekee kijijini aliamua kurudi kukibadilisha kijiji chake mara baada ya kumaliza masomo.

Aliporudi kijijini 1990 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Hiware Bazar kwa kura zote.

Mwenyekiti huyo aliposhika madaraka ya uenyekiti wa kijiji aliamua kuitumia elimu yake kukibadilisha hicho kijiji kwa kuanzisha mradi wa kudaka maji na kuyahifadhi kutoka milimani mvua zinaponyesha na kuyatumia kwa kilimo.Kijiji hicho kimebadilika na kuwa kijiji bora chenye ardhi nzuri na kilimo kizuri na kinapigiwa sifa si India tu bali na watu mbali mbali duniani kama kijiji bora kilichofanya mapinduzi makubwa toka kijiji cha kilofa hadi kuwa kijiji cha watu walioendelea kwa kipindi kifupi.

Huyo mwenyekiti wa kijiji wa India hana digrii ya kilimo ana digrii ya Masters of commerce Kasomea biashara.Na kijijini hakupelekwa na serikali alijipeleka mwenyewe na uzalendo wake na kijiji hakikuwa na mazingira ya kuvutia yalikuwa mabaya si kwa msomi tu bali na kwa wale ambao hawajasoma lakini aliamua kuyabadilisha.

Angalia video ya hicho kijiji

 
Hapa viongozi wa vijiji wanangojea viongozi madhalimu wanajisi uchaguzi ili watangazwe washindi. Hiyo akili hakuna yoyote mwenye madaraka ndani ya nchi hii anayo, akili ya viongozi wengi hapa ni kutumia mbinu ya Magufuli kunajisi uchaguzi..
 
Back
Top Bottom