Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Waziri wetu wa Kilimo ninamjua ni mchapakazi. Alipita nchi nzima kuhamasisha wakulima walime kukabiliana na baa la upungufu wa chakula ulioashiria mwanzoni. Pia ilitangazwa asiyelima hakuna msaada wa chakula toka mamlakani.
Matokeo Kusini mwa Tanzania hasa Ruvuma, Mbeya, Rukwa nk wamefanikiwa kuvuna mahindi mengi. Soko lake linasuasua sana. Bei ni ndogo, siyo ya motisha. Wengi wameamua kuhifadhi hadi bei iwe nzuri. Haijajulikana bei itabadilika lini na kwa msukumo upi!
Baadhi ya wakulima hawana maghala imara pia uharibifu wa wadudu umeanza kwa kasi. Mvua nazo zinakaribia watu waanze msimu mwingine. Nini msukumo wa Wizara kuona soko lenye bei ya motisha linapatikana? Kimya kimekuwa kingi,yawezekana tafsiri ya PM kuwa mahindi yasindikwe,bado haijaeleweka kwa Wakulima. Huenda wanasubiri ufafanuzi zaidi kutoka Wizara yenye dhamana na mazao?