Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
13,242
2,000
Ni kweli kuna baadhi ya Sheria zina mapungufu na Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea kuzifanyia kazi ikiwemo kuziboresha, kuzifuta na kutunga zinazoendana na wakati.

Kuhusu ubadhilifu wa mali za umma, kosa husika linaweza kuhesabika katika makosa ya uhujumu uchumi (inategemea), na sheria ya uhujumu uchumi ipo pamoja na adhabu zake.

Au unazungumzia sheria ipi mahsusi nguvu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,875
2,000
1.Kuna tatizo kubwa la wanasheria binafsi ukiondoa mashirika ya kisheria kuwachaji pesa wateja wao wakikwepa kuwapa risiti na baadae kuanza kuwasumbua baada ya kupokea malipo, je wizara ina mkakati gani wa kuwadhibiti mawakili wa namna hiyo.
2.Katika hukumu kuna jaji kukosea na mahakama kukosea je iwapo itathibitika jaji amekosea kwa makusudi ni taratibi gani zinatakiwa kufwata ili jaji aadhibiwe?
3.Kuna tatizo la makusudi kwa polisi wa kitengo cha mtandao kudai pesa iwapo umeibiwa simu kutegemea na thamani ya simu yako, kwa sababu vifaa vimenunuliwa na serikali na hao wataaalamu wamesomeshwa na serikali kwanini serikali isiweke kiwango rafiki watu wanaopoteza simu walipe ili serikali ipate mapato na wakati huohuo serikali iweze kufatilia utendaji wao badala ya watu hao kutumia vifaa vya serikali kwa manufaa yao binafsi.
 

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
4,060
2,000
Kwanini upelelezi unafanyika kwa kipindi kirefu mathalani miaka 5 hadi 10?
Tatizo liko wapi au kuna uhaba wa wapelelezi?
 

Atlantis Voyager

JF-Expert Member
Jan 19, 2018
299
500
Ningefurahi na wengi wetu wangefurahi endapo mtasaidiana vyombo vingine husika kutatua changamoto zilizoibuliwa na Wakili Peter madeleka reference hapa kwenye linkamezungumzia mapungufu mengi kwenye uendeshaji wa kesi, uapatikanaji dhamana, mazingira duni ya mahabusu, mpaka Plea bargaining.

Inasikitisha mtu anatuhumiwa anapelekwa police, hakuna ushahidi wowote hapewi dhamana anakuwa mahabusu, anapelekwa gerezani hata miaka 4 ushahidi wa kumhukumu unakuwa bado anaenda anajaza nafasi gerezani pasipo sababu za msingi labda aloyemshtaki anataka kumkomoa tuu baadae anaachiwa, dunia inatushangaa sana kwenye haya masuala. Hata zambia hapo hawafanyi hivi. Tunaonekana watu wa ajabu sana. Kama hakuna ushahidi isimamiwe sheria mtuhumiwa aachiwe maramoja akajenge taifa. Mfano kama kesi ya kina Maimu aliyekuwa mkurugenzi wa nida kama haina ushahidi waachieni msiwapotezee muda na nguvu ya kujenga taifa.
 

AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
2,216
2,000
Swali zuri.

Sheria hii ilizingatia kwamba aliye na taaluma anayo nafasi kubwa ya kuajiriwa tena kutokana na taaluma yake, hivyo bado akawa anaendelea kujazia akiba yake hadi atakapostaafu, tofauti na asiye na taaluma.

Hizi asilimia 33 ni za kumpa unafuu wa kujikimu wakati akifuatilia kazi nyingine.

Asante.
Kwanini mnapangia watu cha kufanya na pesa ni zao?. Nani kawaambia kila mtu anataka kuajiriwa, wengine wanataka watumie hizo pesa kama mitaji kuchakata fursa zilizopo na katika huo mchakato wanaweza toa ajira kwa wengine na hiyo mifuko ikajikuta inakusanya mara dufu kuliko kushikilia pesa za watu tena bila ridhaa yao. Sheria hiyo ni kandamizi, ifutiliwe mbali.
 

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
961
1,000

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na mijadala inayoendelea hapa kila siku kuhusu masuala ya Katiba na Sheria za nchi yetu. Aidha kuhusu haki za binadamu, rushwa, utawala wa sheria na mengineyo.

Kupitia thread hii maalum; tutapokea maoni, ushauri na hata malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message (PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurasa rasmi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapa JamiiForums kupata taarifa mbalimbali kuhusu utoaji wa huduma za Katiba na Sheria nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram: @katibasheria_
Twitter: @sheria_katiba
Facebook: Wizara ya Katiba na Sheria

ANUANI ZETU NI:
Wizara ya Katiba na Sheria
Mji wa Serikali, Mtumba
S.L.P. 315,
Dodoma.

Masijala: barua@sheria.go.tz
Simu: +255 26 2310021
Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz
Tovuti: www.sheria.go.tz
Tunashukuru kwa kutupa nafasi.
Niende kwenye swali moja kea moja.

Wizara ya katiba ni chombo kinachotakiwa kuwa makini na kuangalia madhara yaliyopo na yanayoweza kujitokeza na matatizo vile vile ili kutatua changamoto na matatizo ya wananchi wote, wakiwemo wasomi, wasiowasomi, wavivu, matapeli n.k.

Je hi katiba iliyopo ya mwaka 1977 hamuoni Kama imefanyiwa marekebosho Mara nyingi kiasi Cha kuwapa nafasi matapeli kudanganya wananchi ili wapate mlungula?

Je hamuoni wananchi wengi wamekataa tamaa kuisoma wanaposoma sheria Fulani anajua iko vizuri akikutana na tatizo linalolenga ile sheria anaambiwa ilishabadilishwa? Hamuoni Kama hiyo katiba ndiyo imemshawishi kutenda hilo kosa na kusababisha afungwe?

Kuna ugumu gani kuwepo na katiba mpya na uwepo na muda wake wa kuisha yaani (expare date) kutokana na mabadiliko ya dunia inavyoenda? Kuliko kuwa na katiba ya muda mrefu na viraka vingi. Hata nguo ukiweka maviraka huwezi kutembea nayo barabarani japo ni maamuzi na Uhuru mtu. Tutafakari watu watakavyokufikiria.

Tanzania jinsi ilivyo sio ya kutembea na katiba ya mwaka 1977. Tena mnarudisha akili za vijana wetu nyuma badala ya kwenda na wakati. Saidieni Hilo.

Je mlishawahi kufanya utafiti kwa wananchi mkagundua ni kwa Nini wananchi hawajui sheria au hawasomi sheria hata za Halmashauri?

Mfano mabishano ya Spika na mbunge kuhusu wafugaji na mifugo.

Asante na wengine wataendelea.
 

jogolo

Member
May 11, 2021
48
125
Naomba kujua kwa nini siku hizi Raisi au viongozi wa serikali wanashuhudia mikataba ikisainiwa bila ya kuwepo wanasheria au Waziri wa sheria ili hali yote hayo ni kwa manufaa ya nchi?
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,924
2,000
Nataka ufafanuzi:-

Kugushi nyaraka ni kosa kisheria ,miaka ya nyumba jambazi sabaya alikamatwa kwa kosa la kufoji kitambulisho na kujifana ni afisa usalama wa taifa,alipelekwa mahakamani lakini DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi,swali langu inakuwaje DPP asiwe na nia wakati kuna kosa lipo wazi limetendwa? Je kama DPP hana nia je wazalendo wengine wenye nia ya kutaka kuendeleza kesi wanaruhusiwa kufungua upya?
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,672
2,000

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na mijadala inayoendelea hapa kila siku kuhusu masuala ya Katiba na Sheria za nchi yetu. Aidha kuhusu haki za binadamu, rushwa, utawala wa sheria na mengineyo.

Kupitia thread hii maalum; tutapokea maoni, ushauri na hata malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message (PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurasa rasmi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapa JamiiForums kupata taarifa mbalimbali kuhusu utoaji wa huduma za Katiba na Sheria nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram: @katibasheria_
Twitter: @sheria_katiba
Facebook: Wizara ya Katiba na Sheria

ANUANI ZETU NI:
Wizara ya Katiba na Sheria
Mji wa Serikali, Mtumba
S.L.P. 315,
Dodoma.

Masijala: barua@sheria.go.tz
Simu: +255 26 2310021
Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz
Tovuti: www.sheria.go.tz
zipo sheria nyingi zinaonekana kuwa na mapungu ama zilitungwa kwa mihemuko au kwa mashinikizo kutoka juu. Tunaomba sasa mziangalie na kuishawishi mamalaka zirudi Bungeni kwa marekebisho. Baadhi ni kama

1. Sheria ya wanyama pori ambayo Mh Job Ndugai alishangaa ilitungwa vipi.

2. Sheria ya vyama vya siasa na uchaguzi tuliona mgongano mkubwa usio na tija wakati wa hatua za uchaguzi october 2020

3. Sheria ya Uhujum uchumi na utakatishaji wa fedha. Hii sheria imeweka mianya ya kutumima vibaya na imefanikiwa kutweza utu wa watu wengine.

4. Sheria ya Mifuko ya hifadhi ya jamii.

Tunajua sheria haiwezi kumridhisha kila mtu lakini inapokuwa inalalamikiwa na wananchi wengi tujiulize hizo sheria zinatungwa ili zimfurahishe nani.

Asante kwa fursa hii ya kutoa maoni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom