Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yatuma rambirambi msiba wa Sajuki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yatuma rambirambi msiba wa Sajuki

Discussion in 'Entertainment' started by Bishop Hiluka, Jan 3, 2013.

 1. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #1
  Jan 3, 2013
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 3,874
  Likes Received: 1,136
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, amewatumia
  salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii
  Juma Kilowoko (Sajuki) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali
  ya Taifa Muhimbili.

  Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam, Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo
  imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa
  kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu
  na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.

  “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Sajuki sina maneno ya kuelezea masikitiko
  na huzuni niliyonayo, kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza”
  alisema Dk. Mukangara.

  Dk. Mukangara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati
  wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.

  Sajuki ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na
  kikundi cha Kaole na baadaye kuanza kuigiza filamu. Filamu ya kwanza kucheza ni ile ya Revenge
  ya Kampuni ya RJ.

  Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza
  itwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua
  kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi
  zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase, Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077 nk.

  Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini,
  amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.

  Alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011, ambapo alikwenda kutibiwa nchini
  India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki
  kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na
  furaha kwa Watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa
  katika hatua ya utengenezaji.

  Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti
  ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen

  Imetolewa na:
  Mkurugenzi
  Idara ya Habari (MAELEZO).
  Dar es Salaam.
  2 Januari 2013
   
 2. A

  ADK JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2013
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,042
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Bwana abarikiwe kwa kila jambo
   
Loading...