Wizara ya habari, TFF na Bodi ya ligi Mpira wanatakiwa kujipima kama bado wanastahili kuwepo kwahili la Game ya Simba vs Yanga

Street Hustler

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,140
4,189
Wizara ya habari na utamaduni kwa kushirikiana na TFF kupitia Bodi ya ligi Tanzania wanatakiwa kujipima kwamba bado wanastahili kusimamia michezo hasa Mpira kwa kipindi hiki na kuendelea?

Weledi wao umeonekana bado haukidhi mahitaji ya kuendeleza michezo hasa soka kwa kutokuwa na Nia njema kuhusu Mpira wa Leo jumamosi Mei 8 2021 kwenye mchezo naona ya Simba dhidi ya yanga.

Kwann wizara inahusika sababu iliwapa maelekezo TFF ya kusogezwa mbele muda mtanange huo bila kutafakari vizuri kanuni za Mpira.

Kwann TFF waweshindwa kuwaeleza vizuri kwa kuzingatia kanuni kuwa Hilo Jambo haliwezekani na wao wakapeleka ujumbe bodi ya ligi?

Bodi Kama bodi Ni watu yaan kamati hii kamati ilikaa muda gani na muhtasari wao upo wapi? Je walifikiria nn wakati kanuni na Sher zinazowaongoza wanazo na wameshindwa kuzitumia?

Je bodi ya ligi iliwaita viongozi wa klabu zote mbili na kukubaliana dhidi ya muda huo wa dharura wa mabadiliko ya Mpira?

Je vilabu vyote viliafikiana kuhusu badiliko Hilo?

Mie naona kuanzia wizara, TFF na Bodi yaligi na wale viongozi wasimba wote mang'ana wotee wameshindwa kusimamia vizuri michezo hivyo hawastahili kuwepo.
 
Wizara yenyewe ya michezo imejaa wanasiasa! TFF nayo inaendeshwa na mwanasiasa, na kada mtiifu wa ccm! Walistahili kabisa kufanya huu ujinga.
 
Haijalishi muda uliopangwa kama wote walijiandaa kwamba leo kuna Match then Yanga either wanaogopa au hawajajiandaa tuache porojo.
 
LAWAMA ZOTE ZIENDE WIZARA YA MICHEZO!
wizara ndiyo mabosi wa TFF, Wizara ndiyo waliiiamurisha TFF isogeze mbele masaa machache kabla!
Wakuwajibika ni WIZARA
 
Wizara ilipe hasara kwa mashabiki hii siyo haki kabisa wao wanapenda siasa na mambo yao yanayowahusu huko juu ndyo furaha yao,
Sis wengine raha yetu ni kutazama soka kwa hili wamefanya ovyo sana..
 
Hivi kwanini huwezi kutumia akili ndogo Yanga amwogope simba kwa mpira upi hii ni dabi haijalishi majina Yanga ni wasomi wanasimamia sheria
 
Waziri wa sanaa na michezo hatufai ajiuzulu hafai kuendelea kukaa kwenye ofisi ya umma. Haiwezekani awaingizie watu na makampuni hasara kubwa bila sababu.
 
Haijalishi muda uliopangwa kama wote walijiandaa kwamba leo kuna Match then Yanga either wanaogopa au hawajajiandaa tuache porojo.
Sasa nani aliye mwogopa mwenzake?

Yanga nao watasema walituogopa ndio maana wakajishauri na TFF mechi ichezwe saa 1 usiku.
 
Haijalishi muda uliopangwa kama wote walijiandaa kwamba leo kuna Match then Yanga either wanaogopa au hawajajiandaa tuache porojo.
Hapa hatuzungumzii ushabiki au utani wajadi tunazungumzia weledi na utimamu wa kutafsiri Sheria na kanuni za Mpira ndani ya muda sahihi kwa watu sahihi.
 
Hivi hapo hakuna anaetakiwa kufidia hasara kwa waliolipa viingilio na timu. Au boss is always right no matter what..
 
Haijalishi muda uliopangwa kama wote walijiandaa kwamba leo kuna Match then Yanga either wanaogopa au hawajajiandaa tuache porojo.
Unadhani FIFA ni wapumbavu kutaka serikali isiingilie michezo? Unaelewa kwamba michezo inaendeshwa kwa sheria na kanuni?? Unadhani mlivyozoea kusigina katiba ya nchi na kwenye michezo mtaweza?? Nay wa Mitego kawatoa nishai baraza zima la sanaa. Pamoja na kuja Clouds timu nzima ya hilo baraza la sanaa jana kwenye kipindi cha XXL yaani walikuwa wanaongea pumba tupu. Sasa ni zamu ya TFF na huyu Karia kuliwa vichwa...
 
Aliyejiandaa hawezi kususa mchezo huo ni uoga
 
Unadhani FIFA ni wapumbavu kutaka serikali isiingilie michezo? Unaelewa kwamba michezo inaendeshwa kwa sheria na kanuni?? Unadhani mlivyozoea kusigina katiba ya nchi na kwenye michezo mtaweza?? Nay wa Mitego kawatoa nishai baraza zima la sanaa. Pamoja na kuja Clouds timu nzima ya hilo baraza la sanaa jana kwenye kipindi cha XXL yaani walikuwa wanaongea pumba tupu. Sasa ni zamu ya TFF na huyu Karia kuliwa vichwa...

Kuahirishwa mchezo ni kawaida sana. Yanga leo wameonyesha upumbavu wao.
 
Back
Top Bottom