Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Wanahabari Christopher James wa ITV&RADIO ONE na Dickson Billikwija wa Island TV waliwekwa chini ya ulinzi kwa saa 3 kwa maagizo ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, baada ya wanahabari hao kufika kwenye kikao cha wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi Tatu na Mkurugenzi huyo bila mwaliko.
"Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau wa Tasnia ya Habari juu ya DED wa Manispaa ya Temeke,Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi Wanahabari, tunaomba Wanahabari wawe na subira wakati allegations hizi za kusikitisha zinafanyiwa kazi”-BASHUNGWA
Pia soma > Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara