Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,763
- 40,992
Mojawapo ya mambo ambayo baadhi ya vigogo ndani ya chama wanajilaumu sana kuwa yalichangia CCM kufanya vibaya ni "uhuru wa vyombo vya habari". Kuna imani kuwa miaka mitano iliyopita vyombo vya habari vimeachwa vikiichafua serikali na CCM na matokeo yake yameonekana kwenye sanduku la kura. Waraka mmoja ambao uliangukia miguuni mwangu unadokeza kuwa jambo hilo haliwezi na halipaswi kuachwa tena.
Ni maoni yangu kuwa tathmini hiyo ya CCM ni sahihi na kimkakati wa vita ni kuwa unamuweka jenerali mzuri mahali ambapo mnataka madhara makubwa yatokeaa. Jenerali ambaye anajua mbinu vizuri, ana uwezo wa kuthubutu kuleta nidhamu kwenye tasnia ya habari.
Hivyo basi, tuangalie kwa makini ni nani/kina nani watapewa kuiongozi wizara hii ambao ninaamini itakuwa ni propaganda mashine ya hali ya juu lakini wakati huo huo itatumiwa vizuri kuwaleta wahariri wa vyombo kadhaa vya habari kwenye mstari na hata baadhi ya waandishi wa habari. Lengo liko wazi sana - not again vyombo vya habari havitaachwa viwe kama vilivyokuwa. The next battleground itakuwa kwenye Habari.
Binafsi naamini kwa asilimia 100 akitangazwa Waziri wa Habari itathibitisha mtazamo wangu huu - wengine watashangaa mimi nitasema Naam, lets the show begin!