Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 740
- 855
Moja kati ya wizara ambazo kwa kipindi cha kwanza cha awamu ya tano binafsi naona haijaleta mabadiliko basi ni Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo chini ya Dr H Mwakyembe na naibu wake Mh Juliana Shonza.
Wakati wa awamu yao tuliona wazi wamiliki wa tv na radio stations waliitisha press conference na kutoa matamko na kuwataka wafanyakazi wa hivo vituo kutocheza kazi za sanaa za hawa wanasanaa lakini sikuona Mawaziri hawa wakikemea vitendo hivi walikuwa bussy tuu kuhakikisha akina Konk Liquid anatafutiwa tiket iya kwenda kuangalia mechi tuu.
Tunafahamu fika hawa wasanii wengi wao ni vijana waliokosa nafasi katika ofisi mbali mbali na serikali wakaamua kujiajiri katika sanaa sasa kuona kituo X kinatoa tamko la kutocheza kazi za msanii fulani ni sawa na kumnyima nafasi ya kukuza ajira yake.
Leo hii EFM, ETV, CLOUDS FM, CLOUDS TV hawachezi kazi za msanii Diamond na wengine kwa sababu ambazo hazieleweki ila serikali kupitia wizara husika imefumbia macho suala ili kana kwamba kuna sheria inayoruhusu mmiliki wa radio kwa sababu zake mwenyewe tuu kutocheza kazi za msanii fulani.
Ni matumaini yangu kuwa Waziri mpya na naibu wake wakishirikiana katibu wa wizara suala ili hawatalifumbia mdomo wala macho. Kuacha huu uozo kuendelea ni kuruhusu vijana wetu kuendelea kupata misongo ya mawazo tu.